SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

SIMANZI MOROGORO: Ajali mbili za usiku zasababisha vifo vya watu 32 na majeruhi 37

BIOTOXINS

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2026
Posts
1,091
Reaction score
2,283
Mkoa wa Morogoro na Taifa tumekumbwa na simanzi kubwa kufuatia ajali mbili mbaya za barabarani zilizotokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa, Oktoba 9, 2026, na kusababisha vifo vya jumla ya watu 32 na majeruhi zaidi ya 37.

Ajali ya kwanza na yenye maafa makubwa zaidi ilitokea majira ya saa 4:30 usiku huko Mkambarani kwenye barabara ya kuelekea Dar es Salaam, ikihusisha basi la abiria la kampuni ya Drim Line (T 672 DLT) lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya na lori la Scania (T 902 EGN) lililobeba mbao. Magari hayo yaligongana uso kwa uso na kuwaka moto mkubwa ulioteketeza miili ya marehemu, ambapo watu 28 walipoteza maisha (abiria 27 wa basi na mtu mmoja kwenye lori) huku watu 37 wakijeruhiwa vibaya kwa moto na fractures na kukimbizwa hospitalini baada ya uokoaji wa usiku kucha uliohusisha vikosi vya Zimamoto.

Uchunguzi wa awali wa Jeshi la Polisi unaonyesha ajali hii ilisababishwa na uzembe wa dereva wa lori aliyekuwa akijaribu kuyapita magari mengine bila tahadhari.

Ajali ya pili ilitokea mapema kidogo majira ya saa 12:45 jioni ya Alhamisi huko Miti Bora, Dumila (Wilaya ya Mvomero) kwenye barabara kuu ya kuelekea Dodoma, ambapo gari la Jeshi la Polisi lililokuwa na askari waliokuwa doria liligongana na lori lingine la Scania. Ajali hii ilisababisha vifo vya watu 4, wakiwemo askari polisi watatu na raia mmoja, huku askari wengine kadhaa wakijeruhiwa.

Kwa sasa, majeruhi wote wanapatiwa matibabu ya dharura katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, huku Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, ACP Andrew Kantimbo, akitoa wito wa tahadhari kwa madereva huku uchunguzi zaidi wa kisheria ukiendelea.


 
Nashindwa kuweka picha maana bas limeungua lote,miili imeungua ,imekusanywa Kweny mifuko mieusi,ukweli ni simanzi kubwa sana

Hili gari la polisi lilikuwa doria ,askari wameamka vzr wanaenda kaziin lakin ndo hivyo .

Ukiona ajari ni simanzi kubwa idadi ya vvifo inatisha..

Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani
 
POLE KWA WAFIWA!
Nafikiri tunahitaji express highway (Dar to Morogoro); Ili malori yaachwe kwenye hii nJia ya kwake.
Kwenye Ile njia unakuta lori linatembea km 30 kwa saa huku lori jingine linalotembea km 40 kwa saa linataka kuovetake mwenzake. Halafu basi lipo KMS 85 kwa saa. , HAKUNA NAMNA HILO LORI LITAMALIZA , kabla ya basi kufika.
Tukiambiwa tunajanga la Hesabu, watu huwa hawaelewi!
 
POLE KWA WAFIWA!
Nafikiri tunahitaji express highway (Dar to Morogoro); Ili malori yaachwe kwenye hii nJia ya kwake.
Kwenye Ile njia unakuta lori linatembea km 30 kwa saa huku lori jingine linalotembea km 40 kwa saa linataka kuovetake mwenzake. Halafu basi lipo KMS 85 kwa saa. , HAKUNA NAMNA HILO LORI LITAMALIZA , kabla ya basi kufika.
Tukiambiwa tunajanga la Hesabu, watu huwa hawaelewi!
Magufuli alikuwa anaekekea huko ila tukaanza kumpigia kelele eti hayo ni maendeleo ya vitu sisi tunataka maendeleo ya watu.

Kampeni hiyo ilikuwa inaongozwa na kina Zitto, mwishowe wakamuua kabisa
 
Lakini SISI wa kipato kidogo tunapitia changamoto sana ktk mfumo mzima wa maisha.
*SGR kabla ya safari Kuna ukaguzi unafanyika wa njia

Lakini ukiangalia mfumo mzima wa maisha haupo balance hata kwenye huduma za kijamii watu wa chini tunapata huduma kwa shida mno

Waziri akisafri ana kiqora na ulinzi .hili basi limebeba watu zaidi ya 50 kwa nn dereva peke yake ajiamlie mambo
 
Back
Top Bottom