Pamoja na kutanguliza kejeli, I doubt ikiwa hata wewe unaelewa unachosema!!
Kuna vitu 3 katika hili ambavyo hutakiwi kuchanganya madesa!
1. Broadcasting Rights... hii ndiyo unayoisema wewe hapo juu!! Azam tayari wanayo Broadcasting Rights waliyosaini na TFF, na kuiwezesha Azam kurusha matangazo ya VPL. In most cases, Broadcasting Rights zinamilikiwa na vyama vya michezo kwa sababu ndio waendeshaji wa ligi husika!
2. Advertizing Rights... Hizi umilikiwa na Klabu! Hapa ni pale unapoona timu kama Arsenal inapiga uzi wa Emirates kwa sababu wameingia mkataba wa kuwatangazia bidhaa zao.
3. Contents Rights... Hii ndiyo wameingia Yanga na Azam, yaani Haki za Maudhui. Mfano mzuri chukulia msanii kama Diamond ambae kila anakoenda anaambatana na wapiga picha wake, na yake matukio anayarusha YouTube!!
Sasa leo hii ukiingia mkataba wa Haki za Maudhui na Diamond, yale matukio yake (sio ngoma anazo-release) badala ya kuya-post kwenye YouTube Channel yake, utayachukua wewe na kuyapeleka unakokujua! Kama nawe utayarusha YouTube, sawa! Kama una TV stations ambako unataka ndo uyarushe; utajua mwenyewe!!
Kwa maana nyingine, yale matukio (sio mechi wala matangazo) ya Yanga, hivi sasa yatakuwa yanarushwa na Azam! Kwa mfano, yale matukio ya wendawazimu wa Yanga kwenda kuwabeba akina Hersi, Azam atakuwa ndo mmiliki wake! Zile interview, mazoezi, na mambo mengine kama hayo; yatakuwa yanarushwa na Azam!!
That's one, and two, hebu weka ushabiki maandazi pembeni unless kama nawe ni mweupe kwenye haya mambo! Unasema:-
Hivi Klabu "iliyouza" 49% ya hisa zake FOREVER kwa TZS 20 Billion, na Klabu iliyokodisha haki zake za maudhui kwa TZS 41 Billion kwa miaka 10, ni nani hapo anayefikiri sawa sawa?!
And guess what?! Hata kama Simba ataingia mkataba wa TZS 60 Billion (compared na 41 Billion za Yanga) bado Yanga atakuwa ndie kafaidikika zaidi! WHY?
Kwa sababu hizo TZS 60 Billion ndani yake kutakuwa na share ya Mwamedi kwa sababu anamiliki 49% ya hisa za Simba!! Na mimi nakuambia hivi! Simba SPORTS CLUB kuwa na faida ile ile sawa na ya Yanga SPORTS CLUB au kuzidi, basi wanatakiwa kuingia mkataba wa angalau Sh. 80 Billion, ili Mwamedi akipata share yake, inayobaki ndo izidi hiyo 41 Billion za Yanga!!