Acha kudanganya Wenzako Kijana unaonesha hujawahi kufanya biashara hata ya kuuza nyanya 🍅.
Kama unadhani the trading of public company by share unaweza kuifananisha na biashara ay nyanya, basi Mikia mna safari ndefu sana!!
Umeona wapi biashara au Kampuni kugawana Mtaji?
Wapi nimesema kampuni zinagawana mtaji?! Au nani kakuambia Azam imetoa mtaji?
Ndugu Kampuni au Biashara wanachogawana ni Faida (Net Profit) hivyo unaposema Simba wakipewa Bilioni 60 zinakuwa shared hapo unadanganya kwa kuto kujua uendeshaji wa biashara.
Kumbe unadhani faida inatokana na nini?! Yaani hadi sasa hufahamu kwamba faida inatokana na mapato ambayo kampuni inaingiza?!
Yaani hadi sasa hufahamu kwa biashara kama klabu za soka, haki za matangazo ni sehemu ya mapato ya kampuni?
Labda nikueleweshe tu! Hizo 60B zinaingia kwenye Akaunti ya Timu, baada ya gharama za uendeshaji wa Timu pamoja na Manunuzi ya Wachezaji, Mishahara ya Wachezaji, Viongozi na Watumishi wote wa Simba, kitakachobakia kama Faida ndiyo kinagaiwa kati ya wenye 49% na 51%.
Hivyo upo uwezekano mkubwa wakaishia kugawana hasara na si Mihela kama unavyotaka kudanganya Watu kwani gharama za uendeshaji wa hizi Timu ni kubwa zaidi.
Tulia wewe uelimishwe...
Hadi ninapoandika kuna kampuni kibao za ujanja ujanja zinazohusishwa na Simba, na ukitaka kuamini ujanja ujanja niliosema, soma hapa chini:-
In short, jamaa hapo walikuwa chini ya uchunguzi mzito, yaani hawakuwa na tofauti na Ole Sabaya!!! Na kwa kuzingatia busara ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, ndugu Aden Rage kwamba mashabiki wa Simba ni Mbumbumbu, basi nichukue nafasi hii kuwaelimisha mbumbumbu wote wa Simba kwa apo juu ni tamko kutoka taasisi ya serikali!
Turudi kwenye mada!!
Kibiashara,
Simba Sports Club Company Limited (namba iii hapo juu) ndo kampuni yenyewe, na bidhaa yake kubwa zaidi ni
Simba Sports Club!!!
Simba Sports Club Company Limited ni kampuni inayomilikiwa na Mwamedi kwa 49% kupitia Mo Simba Company Limited, na 51% "zinamilikiwa" na Wanachama kupitia Simba Sports Club Holding Company Limited.
Simba Sports Club Company Limited ambayo 49% ya hisa zake zinamilikiwa na Mwamedi, hawa hawatangazi dini wala kufanya charity work bali wanafanya biashara!!! Moja ya biashara zake ni HAKI ZA MATANGAZO ambazo thamani yake itatokana na better performance ya bidhaa kuu ya
Simba Sports Club Company Limited ambayo ni Simba Sports Club!
Haki ya Matangazo kama ile iliyosainiwa kati ya Yanga na Azam, pesa yake ni MAPATO ya kampuni ambayo ni
Simba Sports Club Company Limited inayomilikiwa na Mwamedi kwa 49%! Sasa wanahisa wa kampuni ndio wanaweza kukubaliana mapatio yatumike vipi!!
Hawa wanaweza kuamua sehemu au yote aitumike kuboresha brand kuu ya kampuni, na brand yenyewe ni Simba Sports Club!! Kama watafanya hivyo, maintaining other factors constant, basi tunatarajia brand kuu itapanda thamani, na hivyo kuifanya kampuni nayo ipande thamani, and eventually, hisa za wanahisa kama Mwamedi nazo zinapanda thamani (assuming wangekuwa tayari washaanza kuuza hisa DSE)
Sasa kama ni sehemu tu ndizo zingeenda kukuza brand, sehemu nyingine inaweza kuwa treated kama mapato ya kampuni, ambayo, kama huu ujanja ujanja ingekuwa umeshatoweka, hayo mapato yangekuwa ndo determinant ya profit! Lakini kwavile bado kuna ujanja ujanja mwingi, usishangae mapato husika yakatumika kutoa gawio kwa wanahisa!!!
Lakini mapato husika ndiyo yawe determinant ya profit, ambayo ndiyo inaweza kutoa gawio, au mapato hayo yatolewe kama gawio, vyovyote itakavyokuwa, Mwamedi ana 49% ambayo ameipata kwa mkopo kutokana na sababu zile zile ambazo alizisema Aden!