Admins nimeweka hii ahadi kuwa ikitokea bahati mbaya. Maana si rahisi. Simba akamfunga yanga natuma picha humu nimekalia moto nikiwa uchi. Na naomba members wawili au watatu wawepo kama mashaidi. Nikishindwa nipigwe ban mwezi mzima.
Simba ni team mbovu kwa Yanga. Simba haiwezi mfunga Yanga. HAIWEZEKANI. NI RAHISI NGAMIA KUPITA KWENYE TUNDU LA SINDANO KULIKO SIMBA KUMFUNGA YANGA TAREHE 23.
Kwanza ujiulize mara ya mwisho kumfunga Simba kwenye ligi ilikuwa lini?
Pili ukumbuke kikosi kitakachocheza siyo kile cha ngao ya jamii cha Zoran.
Manula, Zimbwe, Israh, Hinonga, Onyango, Mzamiru, Kanoute, Chama, Phiri, Okra na Sakho. Kina Banda, Gadiel, Kenedy wataingia kipindi cha pili.
Tatu, unapaswa kujua kuwa Simba wana uwezo wa kuwafunga goli la mapema na kuongeza zaidi wakati mkitafutana.
Nne kwa sasa hakuna hadaki Kakolanya, Outara hataanza, Kibu hatacheza na mna bahati Kapombe ni majeruhi.
Tano kikosi chenu kinaongozwa na kipa aliyefungwa magoli sawa na mechi alizocheza msimu huu, mnaye Mwamyeto atakayemkaba Chama kwa macho, Mnaye Morrison asiyesaidia timu kukaba, Mnaye Aucho mwenye kilo 800, mnaye Kibwana anayesubiri tu huruma za Okrah, Mnaye Aziz ambaye anakuwa busy kuvuta pumzi kwa mdomo kuliko kucheza mpira. Mnaye Biringanya ambaye nina hakika hawezi kucheza hiyo siku. Mnaye Lomalisa ambaye anaweza kumpa Phiri assist na mnaye Kisinda anayekimbia kama ngiri bila malengo.