Simba ilishawahi kupigwa 9 na Yanga

Kipigo kikubwa cha Dar derby ni Simba 6 Yanga 0. Zaidi ya hapo hakuna, ni uongo uongo
 
Umetumia utaratibu wa kutaja majina ya wafungaji kwa mechi zote ,naomba utaratibu huo huo uendeleze kuorodhesha majina ya wafungaji wa hayo magoli 9 mwaka 1938.
 
Aandike Sunderland basi..
Sio Simba....
Hoja yako hii ni kama ile ya simba kufika fainali ya shirikisho 1993

je ile ni kombe la shirikisho au Abiola cup??

Kama kule mnakubali majina tofauti ila yote ni mashindano ya CAF na hapa hivyo hivyo

Yote ni Simba tofauti majina tu


Labda hoja uletwe ushahidi ikiwemo wafungaji
 
Hii game ya juzi waliokula 5 tuliwaambia wachezaji wetu mvua ya magoli ianze kipindi cha pili baada ya mapumziko,maana zile goli zingeanza half ya kwanza makolo wangekimbia wasingerudi baada ya half time
 
Hii game ya juzi waliokula 5 tuliwaambia wachezaji mvua ya magoli ianze kipindi cha pili baada ya mapumziko,maana zile goli zingeanza half ya kwanza makolo wangekimbia wasinferudi baada ya half time
Sasa ndiyo mlishwe supu ya ng'ombe kibudu jamani?
 
Ni ya kubumba full stop....
 
Hii game ya juzi waliokula 5 tuliwaambia wachezaji mvua ya magoli ianze kipindi cha pili baada ya mapumziko,maana zile goli zingeanza half ya kwanza makolo wangekimbia wasinferudi baada ya half time
Ni kawaida yetu kukimbia tukiona kuna kapu la magoli sababu tulishafanya kama mara 2 hivi hatukuingiza timu kipindi cha pili.

Safari hii Utopolo walituweza
 
Tulikuwa tunaitwa QUEENS.

Sasa kama unakataa tunaposema Simba ilianzishwa mwaka 1936 ni uongo
Mwaka 1936 ilipoanzishwa iliitwa Queens ( yaani malikia ! )
Baadae ilianza kutumia sunderland ingawa haijafafanuliwa mabadiliko hayo yalikuwa lini, huenda 1938 ilishaanza kutumia sunderland
 
Jana jumapili nilimsikia Mahmoud Zuberi wa Azam Tv anakataa kuhusu hiyo 9-0 akisema ni uongo hakuna rekodi hiyo.

Je kuna mwenye rekodi au kumbukumbu hiyo? Maana 1938 sio mbali kiivyo hadi rekodi zisiwepo.
Kwa Africa ni mbali sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…