𝗩𝗜𝗣𝗜𝗚𝗢 𝗩𝗜𝗞𝗨𝗕𝗪𝗔 𝗭𝗔𝗜𝗗𝗜
Matukio na vipigo vikubwa zaidi kuanzia (5+) kwenye derby ya Kariakoo:
FT: Yanga SC 9-0 Simba SC (1938)
FT : Yanga SC 5-0 Simba SC (1968)
⚽⚽ Maulid Dilunga 18' Pen, 43'
⚽⚽ Salehe Zimbwe 54', 89'
⚽ Kitwana Manara 86'
𝗠p𝗶𝗿𝗮 𝗸𝘄𝗮𝗽𝗮𝗻𝗶:
Tarehe 3 Machi 1969:
Simba SC waligoma kurejea Uwanjani kipindi cha pili baada ya kufungwa (3-0). Yanga SC walipewa pointi (3) na mabao (3) mezani.
FT: Simba SC 6-0 Yanga SC (1977)
⚽ Selemani Sanga OG 20'
⚽⚽⚽ King Kibadeni 10', 42', 89'
⚽ ⚽Jumanne Masimenti 60'
𝗦𝗵𝗶𝗸𝗮 𝗺𝗸𝗼𝗻𝗼:
Mwaka 1988, Yanga SC waliwasaidia watani zao Simba SC wasishuke daraja. Mchezo wa mwisho wa ligi kuu Yanga wakishinda wanatwaa Ubingwa, Simba wakisare au kupoteza wanashuka daraja. Yanga hawakumkaba kwa makusudi, Hamisi Shikamkono ili afunge goli Simba wasalie ligi kuu.
Shikamkono akafunga goli, Simba wakasalia ligi kuu na Yanga wakaukosa Ubingwa. Msimu huo Simba SC walikuwa na mgogoro mkubwa baina ya katibu mkuu, Jimmy David Ngonya na wazee wa klabu hiyo.
Mpaka sasa Simba na Yanga ndio klabu pekee ambazo hazijawahi kushuka daraja ligi kuu Tanzania tangu ianzishwe.
𝗬𝗮𝗻𝗴𝗮 𝘄𝗮𝗮𝘇𝗶𝗺𝗮 𝘄𝗮𝗰𝗵𝗲𝘇𝗮𝗷𝗶 𝗦𝗶𝗺𝗯𝗮 𝗦𝗖:
Mwaka 1998, Yanga SC waliazima wachezaj kutoka Simba SC ili waongeze nguvu kikosini kwao kwenye michuano ya CAF champions league ambapo Yanga ndio walikuwa klabu ya 1 East Africa kuingia group stage.
Wachezaji walioazimwa ni:
- Monja Liseki
- Shabani Ramadhani
- Alphonce Modest
Zamani hawakuwa maadui 🙌
FT: Simba SC 5-0 Yanga SC (2012)
⚽⚽ Emmanuel Okwi 2', 62'
⚽ Felix Sunzu (Penati) 56'
⚽ Juma Kaseja (Penati) 67
⚽ Patrick Mafisango (Penati) 72'
FT: Simba SC 1-5 Yanga SC (2023)
⚽️ Kibu Denis 🅰️ Ntibazonkiza 9'
⚽️ Musonda 🅰️ Yao 3'
⚽️ Nzengeli 🅰️ Aziz Ki 63'
⚽️ Stephanie Aziz Ki 🅰️ Mzize 73
⚽️ Maxi Nzengeli 🅰️ Mzize 77'
⚽️ Pacome (Penati) 86'
©Tom Cruz-Mchambuzi.
View attachment 2812260