Simba inahitaji msaada wa kuambiwa ukweli, wataacha 5 dirisha dogo

Hivi ambao tayari kwenye soka (yanga) wamefanya ajabu gani ambalo simba hawajafanya? Hiyo simba mbovu imeishia robo fainali ccl sawa na walio tayari, acheni ujuaji basi.
 
Ya simba hayakuhusu wewe endelea na li UTOPOLO lako.
 
Kama Kapombe, Mzamiru Zimbwe, Koblan na Kibu Bado wanaonekana kwenye first eleven ya kocha ujue Kuna shida ya usajili tayari ya wachezaji wapya. take my words
Kibu ulimuona wapi first 11? Au huelewi maana ya first 11?
 
Msimu huu Simba ni nyepesi kuliko msimu uliopita mbele ya team za kawaida kama Jkt na Namungo watakula Chuma tena za maana huko championship ndio hawatoboi kabisa
Heheheee! Eti CHAMPIONSHIP
 
Mnasemaga hivyohivyo ila ligi ikiisha mnawasajili nyau nyie na ukitaka ushahidi nakupa, pili huyo kibu umemuona lini akiwa first 11 ya Fadlu?
 
Kwahiyo Aziz ki hajaliliwa abaki?
 
Wamemsajili kibu kuogopa ataenda Yanga kumbe Yanga hawakuwa na mpango nae. Simba wanateswa na kivuli cha Yanga TU baasi. Jobe ni Bora kuliko mutare. Sema TU shabiki na uongozi waliua confidence yake.
Kwani mara ngapi simba inaacha wachezaji halafu yanga inawakimbilia? Hii yanga mnayoiona ni bora bado inachukua wachezaji kwenye simba mbovu
 
Walioshinda hawajiamini.....Tulieni tuje tufumue marinda hayo
Kocha mwenyewe hajiamini, wamesajili bila kumhusisha. Kawapa mashariti ya kusajili striker mwingine haraka, alionao hawana uwezo. Mimi siandiki kishabiki bali naangalia mpira.
 
Wachezaji watatu waliosajiri hadi sasa hawawezi kuwatumia sbb ya chupli chupli ktk usajiri. Simba malizeni mchakato wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ili chupli ziishe. Ushauri tu.
Tulisema hapa, kwanini mnasajili bila kuwa na kocha mhusika? Sasa hivi kocha analia na magalasa walioletwa, anataka washambuliaji wengine kabisaaaaaa.
 
Ushahidi ni kitu muhimu kwenye kilà tuhuma; mnao?
 
Zimbwe na shomari hawapaswi kuwa tegemeo..sio wachezaji wabaya ila wapunguziwe tu dk za kucheza uwanjani.
 
Zimbwe na shomari hawapaswi kuwa tegemeo..sio wachezaji wabaya ila wapunguziwe tu dk za kucheza uwanjani.
Mazoezini ndiko kunakotoa wachezaji wa kikosi cha kwanza na wa akiba. Kocha mpya Bado anawaona akina Zimbwe, Kapombe, Mzamiru ni bora kuliko wapya kwenye maeneo hayo. Afanyeje sasa zaidi ya kuwapa nafasi? Hii inaonyesha kuwa timu iliyovunjwa ilivunjwa kimakosa kwasababu ndogo TU ya kufungwa na Yanga iliyotoshana nguvu na mamelods na wakasahau kuwa timu Ile waliyovunja ilicheza robo final CAF championship.
 
Wote simba na Yanga waliondolewa na Africa Top soccer Giants..

Na huenda wangefika zaidi ya walipofika kama ratiba ingewa-favour kwa kutowakutanisha na hao.

Kila nikiangalia marudio ya Mechi ya ufunguzi Simba vs Al ahly Dar, na ile ya marudio cairo.
nakubaliana na ww kwamba Simba haikuwa mbaya kama ilivyosemwa..

Tatizo ni uongozi wa Simba kukubali kuwa driven na hisia za mashabiki.
 
O
Leo hii, kocha Davids Bado anawaona Zimbwe Kapombe Mzamiru na koublan kwenye mazoezi yake. Ina maana makosa makubwa yalifanyika kukipiga chini kikosi ambacho kiliifikisha timu robo final CAF championship. Davids haoni mshambuliaji pale sawa na alichokiona Benchikha, anawadai viongozi wampe mshambuliaji.
 
this is true.
 
Simba ni timu nzuri sana!! Iko vizuri sana. Tatizo ni matarajio yasiyokuwa na uhalisia kwa mashabiki. Isilinganishwe na Yanga kwa sasa, ila nina uhakika msimu huu Simba itakuwa bingwa!! Baada ya mechi kadhaa za ligi kuu Simba itaimarika sana!! Itaanza kwa kushinda kila mechi kwa mbinde, baadaye itakuwa inashinda kwa uhakika na hatimaye itakuwa inashinda kwa kunyanyasa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…