Simba Inahitaji "Msema Utumbo" mmoja, Ahmed hawezi

Kwa Wajihi na Kaliba ya kimuonekano ya Bw Ahmed Ally hafananii kabisa na wala hana uwezo huo linapokuja swala la kutaka kutupa dongo, na haswa kama anataka kujibizanana Msema hovyo wa ile Timu Pinzani ya Uto.

Huwa nakunja vidole(cross fingers) kila mara anapozungumza Bw Ahmed Ally kwa kutamani amalize maongezi yake bila kuweka kijembe chochote kisicho na msingi.

Hivyo ninasahuri Ahmed awe tu anajikita kwenye mambo muhimu na ya msingi ya club na suala la kujibizana na Haji au kutoa vijembe vya hapa na pale basi kazi hiyo ifanywe na Mtu mwingine.

Kwa hilo basi Bw Mwijaku aweza kuwa "Msema Utumbo" rasmi wa Club kwa ajili ya kutekeleza jukumu hilo.

Ni dhahiri Bw yule hana ufahamu wa kutosha wa mambo ya Mpira ukimlinganisha na yule Mwenzake wa Uto, hivyo wanachopaswa kufanya Simba ni kutumia Wajuzi wa mambo kuwa wanamuandalia script ya yale mambo muhimu yanayohitaji kufanya rejea....maana bila hivyo mjiandae kusikia akisema mwaka fulani wakati Golikipa wa Simba akiwa Hamisi Kinye n.k...sasa ili kuepusha hayo aandaliwe script alafu kule kunakobaki sasa kwa kuwachamba kina Mayele and co ndio afanye free style maana uwezo huo kikukweli Mtu yule amejaaliwa.

Ahmedy aachane kabisa na vijembe maana hapendezi kabisa.
Makala ndefu umejaza utumbo tu
 
Ili umzidi Haji inabidi uwe mpuuzi kama Haji la sivyo ukiingiia kwenye upuuzi na kiasili huna upuuzi ata kushinda kwakua kwenye upuuzi Haji ni Bingwa.

Licha ya kushindwa kwenda sambamba na Haji bado msemaji wa Simba hajui mambo mengi yahusuyo soka Kwaiyo Haji ana advantage kubwa ku mburuza Ahmedy.
Sehemu pekee Ahmedy ana weza kimzidi Haji ni kwenye utangazaji.
 
Ahmed hayupo kushindana na mtu. Yupo kushindana na job allocation yake Simba Sc. Halafu Haji ni punguani,mpeni dawa badala ya kumshindanisha
 
Ahmed kamwacha mbali sana bwana yule!! hizi nyingine ni propaganda tu!! mlitegemea simba isipate mtu wa kuweza kuziba nafasi ya white lkn dogo kafukia shimo hadi white mwenyewe haamini anachokiona!!

Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
Ukisoma andiko langu mimi sina shida na Ahmed, na ninaikubali kazi yake mpaka sasa.

Ambacho ninachoshauri kisifanyike ni yeye asijihusishe na mambo ya mipasho, asijibizane na wasema hovyo wengine anaharibu Kaliba yake na mbaya zaidi hafananii kubeza na kukashifu wengine.

Ila tusiache kujibu mipasho na kuendeleza chagizo za hapa na pale kwani haswa hiyo ndio maana ya utani wa jadi...na hili libaki kama jambo letu sisi TZ hatuhitaji kujiuliza sijui mbona kule hawafanyi, wakati wao mechi zao kubwa huishia kuita Derby, sisi kwetu ni Derby na utani wa jadi..

Hata baada ya mechi ya Yanga na Mbeya City namna ambavyo nilikuwa namsikiliza yule Bw wa Clouds anavyoidadavua kikudakuda lile tukio ndio burudani ninayoizungumzia mimi, na ahmed kipaji hicho hana, na akifanya anajilazimisha tu wala haivutii...yeye ajikite tu kwa taarifa muhimu za Timu.

Hivyo ushauri wangu ni tumtumie "Msema utumbo" wetu kujibu mapigo ya utumbo wa upande wa pili, hizi hoja za tulishatoka huko hzina maana, utani wetu ubaki mpaka Mtu akunje ngumi.
 
Nilikuwa na Google huko kutafuta msemaji mkuu wa Liverpool lakini najibiwa badilisha search tena hatujakuelewa bado unatafuta nini. Kama na sisi tunataka kufika na kushindana na wenzetu Africa tuondokane na hawa chawa ila kama tunataka kufurahishana humu ndani ni sawa tu tuendelee. Dunia nzima ni Manager tu anaongelea mambo ya team huku kwetu usichangae kuona chawa anatoa tathmini ya team na hali za wachezaji ki afya. Only in Tanzania
Tusiige huko, tufanye sisi mpaka wao watakapotuiga sisi...utani ni burudani, Mtu anaielezea penati ya Mayele mpaka unajiuliza ulikuwa unaangalia mechi hiyo hiyo au nyingine?.

Hizi burudani hazina madhara tusiziache.
 
mpe sifa yake ahmed, amemfanya manara mwakani afikirie "kutupa taulo" na kuachana na mambo ya mpira. nasikia anataka kujaribu siasa.

dogo kaja na approach mpya ya uafisa habari/usemaji wa club za mpira nchini. approach aliyokujanayo imempiga na kitu kizito manara. haamini macho yake.
Hilo mimi sipingi.
 
Duuh kule Epl tumezoea kuona Managers ndio wasemaji wa timu.
 
Wengi wanakupinga mkuu lakini nimeelewa ulichokimaanisha.

Wanaokupinga wengi ni makolo wenzio wa " sizitaki mbichi hizi" .
Ila unachoongelea ndio utofauti wenyewe wa ligi yetu na hizo ligi nyingine.

Mfano huyu Masau Bwire, watu tulikua hatumjui kabla lakini baada ya utani wake wa kupapasa (papasa squard) akawa maarufu kwa wafuatilia mpira wengi.
Timu yake japo haifanyi vizuri lakini kwa utani wake ule somehow inafatiliwa imefanya nini coz msemaji wake anabwabwaja sana ( na omba asikufunge huyu mtu, ana maneno ya kero mno).

Ndicho mleta uzi alichokimaanisha anaweza kua hajaajiriwa rasmi na timu lakini akawa na baraka za timu.
Ligi itanoga.
 
Mimi nazungumzia "UTANI WA JADI", huu ni utamaduni zaidi kuliko formality.

Sipingani na ufanyaji kazi kiweledi lakini si vibaya tukabakiza utani na hicho ndio kitutofautishe na Ligi nyingine.

Inaleta buradani kufanya utani penati ya Mayele ila ninachokitaka ni atumike Mtuanayejua kukera...na kazi hiyo asiifanye Ahmed Ally, kwangu hapendezi au hawezi...ila yule Mwijaku atumike asumbuane na yule wa Utopoloni.

We unafikiri ile penati wangekosa Simba yule Baba angekaa kimya?, angekebehi..sasa hilo ndilo nalozungumzia mimi utani ubaki, ule wa mtaani na wa Watu rasmi tutakaowapa vyeo vya "Wahamasishaji".
Tunao wengi tu.
1.K Mziwanda
2. Mzaramo.
3. Mwakitalima
4. Mzee wa Pass Milioni
5. Na wengine wengi tu wana Simba watawaongezea hapa.
Hawa ndio maalumu kwa ajili ya shombo za kwenye mitandao
 
Sawa kabisa Mkuu umenielewa.

Tatizo la wengi wetu ni kujibu hoja kabla ya kusoma content na kuitafakari.

Sasa Mtu anaishia tu kusema nimeandika utumbo, sijui kama hata ameelewa point yangu.

Hata mimi kuna wakati kebehi na utani wa Manara unanikwaza lakini bado mara kwa mara nitapita page yake nione leo kaja na nini.

Sasa pia si mbaya na upande wa pili nasi tukawa na mfumo wetu wa kuzuia makombora, na hii ndio iwe signature yetu ya ushabiki sio lazima kuangalia Wazungu wanafanya vipi...sisi tudumishe utani wetu wa jadi.
 
Sawa, bado si mbaya tukiwa na mmoja wa kwenye main stream...utani hauna formular maalum yeyote anayewezea si mbaya akachagiza na wote watakuwa na ladha zao tofauti kwa Msikilizaji.
 
Sawa kabisa Mkuu umenielewa.

Tatizo la wengi wetu ni kujibu hoja kabla ya kusoma content na kuitafakari.

Sasa Mtu anaishia tu kusema nimeandika utumbo, sijui kama hata ameelewa point yangu.

Hata mimi kuna wakati kebehi na utani wa Manara unanikwaza lakini bado mara kwa mara nitapita page yake nione leo kaja na nini.

Sasa pia si mbaya na upande wa pili nasi tukawa na mfumo wetu wa kuzuia makombora, na hii ndio iwe signature yetu ya ushabiki sio lazima kuangalia Wazungu wanafanya vipi...sisi tudumishe utani wetu wa jadi.
Kabisa mkuu sasa hapo juu jamaa anauliza kama kuna vilabu vya ulaya vina msemaji!?
Kama wanaiga ya ulaya waige vyote mbona wanaiga baadhi tu, ulaya kuna ndumba na uswahili kama huku, ulaya kuna kuhonga marefa, wachezaji n.k

Wapunguze ujuaji, huu unaweza kua ubunifu mzuri, ila tu wauweke kisheria ili watu wasivuke mipaka.
 
Mimi nazungumzia "UTANI WA JADI", huu ni utamaduni zaidi kuliko formality.

Sipingani na ufanyaji kazi kiweledi lakini si vibaya tukabakiza utani na hicho ndio kitutofautishe na Ligi nyingine.

Inaleta buradani kufanya utani penati ya Mayele ila ninachokitaka ni atumike Mtuanayejua kukera...na kazi hiyo asiifanye Ahmed Ally, kwangu hapendezi au hawezi...ila yule Mwijaku atumike asumbuane na yule wa Utopoloni.

We unafikiri ile penati wangekosa Simba yule Baba angekaa kimya?, angekebehi..sasa hilo ndilo nalozungumzia mimi utani ubaki, ule wa mtaani na wa Watu rasmi tutakaowapa vyeo vya "Wahamasishaji".
Usiturudishe enzi za ujima ndugu. Tunachotaka ni professionalism.
 
Kwa Wajihi na Kaliba ya kimuonekano ya Bw Ahmed Ally hafananii kabisa na wala hana uwezo huo linapokuja swala la kutaka kutupa dongo, na haswa kama anataka kujibizanana Msema hovyo wa ile Timu Pinzani ya Uto.

Huwa nakunja vidole(cross fingers) kila mara anapozungumza Bw Ahmed Ally kwa kutamani amalize maongezi yake bila kuweka kijembe chochote kisicho na msingi.

Hivyo ninasahuri Ahmed awe tu anajikita kwenye mambo muhimu na ya msingi ya club na suala la kujibizana na Haji au kutoa vijembe vya hapa na pale basi kazi hiyo ifanywe na Mtu mwingine.

Kwa hilo basi Bw Mwijaku aweza kuwa "Msema Utumbo" rasmi wa Club kwa ajili ya kutekeleza jukumu hilo.

Ni dhahiri Bw yule hana ufahamu wa kutosha wa mambo ya Mpira ukimlinganisha na yule Mwenzake wa Uto, hivyo wanachopaswa kufanya Simba ni kutumia Wajuzi wa mambo kuwa wanamuandalia script ya yale mambo muhimu yanayohitaji kufanya rejea....maana bila hivyo mjiandae kusikia akisema mwaka fulani wakati Golikipa wa Simba akiwa Hamisi Kinye n.k...sasa ili kuepusha hayo aandaliwe script alafu kule kunakobaki sasa kwa kuwachamba kina Mayele and co ndio afanye free style maana uwezo huo kikukweli Mtu yule amejaaliwa.

Ahmedy aachane kabisa na vijembe maana hapendezi kabisa.
Umeamua kumpigia debe Mwijaku apewe mikoba ya kumjibu Haji.
Tate Mkuu ukikaidi utapigwa2 CHAMASON-MORISON-SAKHOSON njaakalihatari
 
Ili umzidi Haji inabidi uwe mpuuzi kama Haji la sivyo ukiingiia kwenye upuuzi na kiasili huna upuuzi ata kushinda kwakua kwenye upuuzi Haji ni Bingwa.

Licha ya kushindwa kwenda sambamba na Haji bado msemaji wa Simba hajui mambo mengi yahusuyo soka Kwaiyo Haji ana advantage kubwa ku mburuza Ahmedy.
Sehemu pekee Ahmedy ana weza kimzidi Haji ni kwenye utangazaji.
Ahmed ana Kaliba ya utulivu, Kijana smart ndio maana sitaki kumuona akiongea vijembe kwa Wapinzani...atunze Kaliba yake.

Yeye awe anatoa taarifa muhimu tu za Timu, kama vile timu inajiandaa kwa mechi, Mchezaji fulani bado ni majeruhi...timu inaondoka leo, tumemsajili Mchezaji fulani n.k.

Mwijaku ndio anafaa kukabiliana na Msema hovyo mwenzake wa Uto, ila ni kweli yeye amewazidi kwa ufahamu wa mambo kadhaa kadhaa ya soka...ndio maana nikashauri basi ikibidi Bw Mwijaku awe anapewa briefing na wajuzi kuhusu mambo kadhaa kabla hajaenda kwenye vipaza...ila kule kwenye kusema utumbo apige free style maana kipaji hicho anacho.
 
Back
Top Bottom