Simba Inahitaji "Msema Utumbo" mmoja, Ahmed hawezi

Makala ndefu umejaza utumbo tu
 
Ili umzidi Haji inabidi uwe mpuuzi kama Haji la sivyo ukiingiia kwenye upuuzi na kiasili huna upuuzi ata kushinda kwakua kwenye upuuzi Haji ni Bingwa.

Licha ya kushindwa kwenda sambamba na Haji bado msemaji wa Simba hajui mambo mengi yahusuyo soka Kwaiyo Haji ana advantage kubwa ku mburuza Ahmedy.
Sehemu pekee Ahmedy ana weza kimzidi Haji ni kwenye utangazaji.
 
Ahmed hayupo kushindana na mtu. Yupo kushindana na job allocation yake Simba Sc. Halafu Haji ni punguani,mpeni dawa badala ya kumshindanisha
 
Ukisoma andiko langu mimi sina shida na Ahmed, na ninaikubali kazi yake mpaka sasa.

Ambacho ninachoshauri kisifanyike ni yeye asijihusishe na mambo ya mipasho, asijibizane na wasema hovyo wengine anaharibu Kaliba yake na mbaya zaidi hafananii kubeza na kukashifu wengine.

Ila tusiache kujibu mipasho na kuendeleza chagizo za hapa na pale kwani haswa hiyo ndio maana ya utani wa jadi...na hili libaki kama jambo letu sisi TZ hatuhitaji kujiuliza sijui mbona kule hawafanyi, wakati wao mechi zao kubwa huishia kuita Derby, sisi kwetu ni Derby na utani wa jadi..

Hata baada ya mechi ya Yanga na Mbeya City namna ambavyo nilikuwa namsikiliza yule Bw wa Clouds anavyoidadavua kikudakuda lile tukio ndio burudani ninayoizungumzia mimi, na ahmed kipaji hicho hana, na akifanya anajilazimisha tu wala haivutii...yeye ajikite tu kwa taarifa muhimu za Timu.

Hivyo ushauri wangu ni tumtumie "Msema utumbo" wetu kujibu mapigo ya utumbo wa upande wa pili, hizi hoja za tulishatoka huko hzina maana, utani wetu ubaki mpaka Mtu akunje ngumi.
 
Tusiige huko, tufanye sisi mpaka wao watakapotuiga sisi...utani ni burudani, Mtu anaielezea penati ya Mayele mpaka unajiuliza ulikuwa unaangalia mechi hiyo hiyo au nyingine?.

Hizi burudani hazina madhara tusiziache.
 
Hilo mimi sipingi.
 
Duuh kule Epl tumezoea kuona Managers ndio wasemaji wa timu.
 
Wengi wanakupinga mkuu lakini nimeelewa ulichokimaanisha.

Wanaokupinga wengi ni makolo wenzio wa " sizitaki mbichi hizi" .
Ila unachoongelea ndio utofauti wenyewe wa ligi yetu na hizo ligi nyingine.

Mfano huyu Masau Bwire, watu tulikua hatumjui kabla lakini baada ya utani wake wa kupapasa (papasa squard) akawa maarufu kwa wafuatilia mpira wengi.
Timu yake japo haifanyi vizuri lakini kwa utani wake ule somehow inafatiliwa imefanya nini coz msemaji wake anabwabwaja sana ( na omba asikufunge huyu mtu, ana maneno ya kero mno).

Ndicho mleta uzi alichokimaanisha anaweza kua hajaajiriwa rasmi na timu lakini akawa na baraka za timu.
Ligi itanoga.
 
Tunao wengi tu.
1.K Mziwanda
2. Mzaramo.
3. Mwakitalima
4. Mzee wa Pass Milioni
5. Na wengine wengi tu wana Simba watawaongezea hapa.
Hawa ndio maalumu kwa ajili ya shombo za kwenye mitandao
 
Sawa kabisa Mkuu umenielewa.

Tatizo la wengi wetu ni kujibu hoja kabla ya kusoma content na kuitafakari.

Sasa Mtu anaishia tu kusema nimeandika utumbo, sijui kama hata ameelewa point yangu.

Hata mimi kuna wakati kebehi na utani wa Manara unanikwaza lakini bado mara kwa mara nitapita page yake nione leo kaja na nini.

Sasa pia si mbaya na upande wa pili nasi tukawa na mfumo wetu wa kuzuia makombora, na hii ndio iwe signature yetu ya ushabiki sio lazima kuangalia Wazungu wanafanya vipi...sisi tudumishe utani wetu wa jadi.
 
Tunao wengi tu.
1.K Mziwanda
2. Mzaramo.
3. Mwakitalima
4. Mzee wa Pass Milioni
5. Na wengine wengi tu wana Simba watawaongezea hapa.
Hawa ndio maalumu kwa ajili ya shombo za kwenye mitandao
Sawa, bado si mbaya tukiwa na mmoja wa kwenye main stream...utani hauna formular maalum yeyote anayewezea si mbaya akachagiza na wote watakuwa na ladha zao tofauti kwa Msikilizaji.
 
Kabisa mkuu sasa hapo juu jamaa anauliza kama kuna vilabu vya ulaya vina msemaji!?
Kama wanaiga ya ulaya waige vyote mbona wanaiga baadhi tu, ulaya kuna ndumba na uswahili kama huku, ulaya kuna kuhonga marefa, wachezaji n.k

Wapunguze ujuaji, huu unaweza kua ubunifu mzuri, ila tu wauweke kisheria ili watu wasivuke mipaka.
 
Usiturudishe enzi za ujima ndugu. Tunachotaka ni professionalism.
 
Umeamua kumpigia debe Mwijaku apewe mikoba ya kumjibu Haji.
Tate Mkuu ukikaidi utapigwa2 CHAMASON-MORISON-SAKHOSON njaakalihatari
 
Ahmed ana Kaliba ya utulivu, Kijana smart ndio maana sitaki kumuona akiongea vijembe kwa Wapinzani...atunze Kaliba yake.

Yeye awe anatoa taarifa muhimu tu za Timu, kama vile timu inajiandaa kwa mechi, Mchezaji fulani bado ni majeruhi...timu inaondoka leo, tumemsajili Mchezaji fulani n.k.

Mwijaku ndio anafaa kukabiliana na Msema hovyo mwenzake wa Uto, ila ni kweli yeye amewazidi kwa ufahamu wa mambo kadhaa kadhaa ya soka...ndio maana nikashauri basi ikibidi Bw Mwijaku awe anapewa briefing na wajuzi kuhusu mambo kadhaa kabla hajaenda kwenye vipaza...ila kule kwenye kusema utumbo apige free style maana kipaji hicho anacho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…