Simba kama hatutasajili wachezaji wa maana Januari basi turuhusu Yanga acheze nafasi yetu makundi ya CAFCL

Hiyo nafasi ya 13 halafu azam anakufunga!
Hiyo nafasi ya 13 mbeya city una draw nae yeye wa nafasi ya 340....
Huoni kuwa kuna tatizo katika hizo rankings?

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hebu tupe chanzo kinachoonyesha Simba ipo nafasi ya 13 , kabla sijaweka link yangu
 

Wewe jamaa ni mbumbumbu. Simba iko namba 13 CAF, utopolo hata 40 bora haipo. Hiyo nafasi ya CAF haikuja bahati mbaya. Yes misimu miwili usajili ulikua wa hovyo kwa maana Simba haina kikosi kipana, first eleven ikipwaya kwa msimu huu inakosa mbadala, lakini bado Simba ni bora
 
Nafikiri ulikuwa una mquote mwingine
 
Mzee Rage ,unaitwa huku.
 
Kama huna quality players ubora unatoka wapi
 
Kama huna quality players ubora unatoka wapi
Mkuu ubora ni suala ambalo ni subjective sana, kila team ina standard zake za ubora na anajilingisha na nani? Simba kwa ligi hii ya ndani ina ubora uliokidhi haja, kuwa na mapungufu kadhaa kwenye kikosi haukufanyi Simba iwe chini.


Ubora wa team unapimwa kwa hatua alizovuka katika vipimo, CAF wameset standards za ubora wa team Africa, Simba in five years ameweza kufika hizo standards na kuwepo alipo sasa hv, kumbuka hii si ndondokela ni jitihada. Germany amefungwa na Japan hii haiifanyi German kuwa team mbovu, Simba ni Simba hata anyeshewe na mvua mzee wangu. Kuna muda team anapitia nyakati ngumu kdg, lkn ni za muda.
 
Babu hii timu ni mbovu bila kumumunya maneno
Ubovu wa timu unaletwa na mambo mawili.
1.Kuwa na kikosi kibovu yaani wachezaji wasio na ubora

2. Kuwa na benchi la ufundi bovu.

Tatizo la Simba liko namba mbili wachezaji wa Simba ni wazuri sana tu probably sisi ndiyo tuna timu nzuri kuliko zote ligi kuu.

Kukosa benchi la ufundi la kudumu tangu mwezi May kumeua sana mwendelezo wa timu pamoja na malengo ya timu kwa sababu kila kitu ni temporary tu.

Kingine ambacho naona ni kama vile Simba walimaliza msimu baada ya kuingia group stages Champions League namna timu inavyoendeshwa baada ya kuingia hatua ya makundi ni kama tayari walishamaliza walichokuwa wanakipigania kwenye msimu huu hii hali unaona kwa viongozi na unaona kwa wachezaji.
 
Shida kubwa ya Simba kwa sasa ni benchi la ufundi siyo wachezaji.


Benchi la ufundi halina ufundi na halina malengo makubwa it is like timu inajichezea tu.
 
Kuna mapungufu ya wachezaji kadhaa upande wa kushoto back up nzuri kushoto.

Na Quality namba 8 na wing ya kulia tu.

Ila kwa aina ya kikosi tulichonacho tunaweza compete vizuri tu kama tuna kocha mwenye malengo na ufundi
 
Kabati la makombe limekuwaje ?

Hali ni tete kivipi ?
 
Hiyo nafasi ya 13 halafu azam anakufunga!
Hiyo nafasi ya 13 mbeya city una draw nae yeye wa nafasi ya 340....
Huoni kuwa kuna tatizo katika hizo rankings?

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Bayern Munich anachukuwa ndoo German miaka 9 mfululizo sasa lkn anafungwa na team za kawaida na hata kudraw pia. Man city ambayo ipo kwenye peak yake hv sasa imepoteza kwa Brentford chuma 2..katika mchezo wa mpira wa miguu kupoteza ni kawaida. Lakini ni muhimu ukafahamu ya kuwa Simba hata angefungwa jana na Mbeya City au hata Ihefu magoli 10, bado isingeshusha thamani yake kisoka Africa kwa maana ya uhalisia, kaka ukiwa tayari umejiwekea value inahitaji jitihada zaidi ili kuishusha hy value.

Mfano, leo hii ukiokota noti ya dola 100 jalalani hata kama ina kinyesi, haitopoteza thamani yake chief.

Unachosahau ni kuwa hakuna team yenye haki miliki ya kushinda tu, hy Azam unayosema kwani wewe unaionaje ni team ndogo? nao si title contender pia?
 
Sijasoma ila najua ume andika pumba
 
Naitimisha kwa kusema Simba Ni mbovu msimu huuu na mkitaka kuliona Hilo subirini makundi ndio mtajuwa kuwa mna timu ama litimu
 
Utapata matokeo kwa wydad ukiwa na kibu, bocco, mkude, mzamiru, okwa, akpan, kanoute, Israel, kapama, nyoni, gadiel, sakho, kennedy, onyango, outarra?
Yes unachohitaji ni kocha mwenye mbinu tu
 
Shida ya Simba Kwa sasa sio wachezaji,shida ipo Kwa falsafa za makocha Simba ni kama ina makocha wawili sasa wachezaji hawajui wafuate falsafa ya kocha yupi.Nadhani Simba wabaki na Juma Mgunda tu,ushindi utakuwa back to back ndani na nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…