Simba kufungwa na Raja tumestahili, tujipange msimu ujao

Simba hakuna team pale. Wanajazwa ujinga wa historia ya kwa Mkapa. Km walishindwa kushinda ya Horoya iliyokuwa haki Yao, basi tena. Eti Kila mtu ashinde kwake nyooooo.
 
Ndio football mzee sio kila siku utashinda wewe tu..
 
umeongea pointi tupu
 
Kwa mkapa hatoki mtu..... Huu msemo wakipumbavu sana unawadanganya mashabiki wanajiona wana timu isiyo fungika kumbe ni timu ya kawaida tu.
Lakini kama ni mshabiki wa mpira kweli, ungeweza kutoa kasoro zilizojidhihirisha kwenye mchezo wa leo kwanza kabla ya kuanza kuhukumu historia!

Timu haina short on target ya maana, mipira inapotea kati, Saido anapoteza mipira ovyo, anaesaidia na Kapombe hajulikani, Boko na Baleke hakukuwa na tofauti.

Kongole kwa Shomari kwa kila hali.

Kimsingi, tatizo ni waalimu kwanza, kisha umri wa wachezaji na mwisho makuzi ya wachezaji, kuwa mpira sio jambo lao la kwanza, ni baada ya kufeli shule!
 
Chifu ukisema tatizo ni walimu kwangu mm naona sio sawa na ni kama kuendelea kutetea upuuzi wa viongozi wa simba bila sabau.

Viongozi hawapo serious kwenye uwekezaji na scouting ya wachezaji. Asilimia 80 ya wachezaji wa simba ni flopy au viwango vidogo. Wengi wamesajiliwa kiujanja ujanja na ufaza mwingi.

Manzoki tuu iliyohitajika ml 400 viongozi waliingia mitini wakaleta kyombo, kapama na the likes ambao ni bei chee na viwango duni. Pale simba kwa squad hii hata umlete mzee wenga hatoboi.
 
Wale hata game irudiwe Simba anafungwa tena kwa kifupi jamaa wamewazidi Simba uwezo
 
Simba imefungwa Kwa sababu
1. Kukimbizana na ahadi ya Raisi
2. Kutowaheshimu Cassablanka na kuamua kukimbizana nao huku ukijua wale madogo Wana uwezo wa kuhold mpira na dogo mmoja anauwezo wa kuwapita watu watatu bila was was kabisa , lakini bado unakimbiza mpira mbele ,na wachezaji wako ni wepesi kupoteza

Kwa haya yote kocha alaumiwe ,
 
Kwahiyo ulitaka apaki basi na sio kutafuta point tatu? Kocha hana cha kulaumiwa wacjeza wazee unategemea wakupe nn?
 
Mgunda alishaiweza timu
Mimi ni shabiki wa mnyama pure.... ila hii ya leo hata umlete pep guardiola original hachomoi.

Hiyo quality ya waarabu umeiona? Umecheki wanavyokimbia? Umecheki wanavyojiamini wakipata mpira?umeona pass accuracy yao?

Men tukubali raja ina wachezaji quality kuliko simba leo hakuna wa kulaumiwa hata mmoja.
 
Hii ya ahadi ya Rais hata mimi niliiona mapema nikasema inaweza kuwa tatizo la Simba kupoteza match
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…