Simba kwanini kiingilio kisingekuwa elfu kumi kama Yanga??

Simba kwanini kiingilio kisingekuwa elfu kumi kama Yanga??

Kipaumbele chetu Kikuu ni Burudani kwa Wote na siyo kuweka Kiingilio Kikubwa ili Kukidhi Njaa zenu tukuka, mpate Fedha za Kumalizia Usajili na nyinginezo za Kulipia Madeni Sugu mbalimbali mnayodaiwa na makubwa yakiwa ni ya Wale Waganga wa Kienyeji Wawili wa Kilosa Morogoro na wa Mwandiga Kigoma.

Na kingine Simba SC ni Timu iliyo chini ya Mwekezaji Bilionea ambaye Afrika na hata Kwingineko duniani wanamjua hivyo ni Aibu Timu kwa Bilionea kuweka Kiingilio Kikubwa kumaliza Shida za Klabu na Kukomoa Mashabiki.

Simba SC ina Mwekezaji Bilionea mwenye Fedha na Utajiri wa halali ila kuna Timu zingine hapa duniani ( siyo Tanzania ) zina zina Matajiri Mafia, Majambazi, wakwepa Kodi, Wahujumu Uchumi, Wauza Dawa za Kulevya, Wadhulumati wa Mali za Watu na sasa Utajiri wao uneongezeka baada ya Mwanamke Mmoja kwa Kushirikiana na Mwanaume wake wa Siri ( sasa hana Kazi Kapumzika ) wamemuunganisha Tajiri huyo kubeba Silaha zote zinazotoka Bahari inayogombewa na Wadubai kwenda Congo DR huku Gari zake zingine zikibeba Madini na Makaa ya Mawe ndani ya nchi ya waliompa hiyo Dili.

Cc: SAGAI GALGANO, cocastic, rodrick alexander etc
Hii ndonga imetulia
 
Kwa sababu simba hatuna njaa, na kwa kukuthibitishia hilo timu imetoka ulaya ilipokua imeweka kambi ya muda mrefu (preseason),, uliza hao ndugu zetu walikua wapi ?
Walikuwa wanashindia ugali kwa sukari hapo gezaulole.
 
Kwahiyo Kila kinachofanywa na Yanga simba nao wafanye hivyo?

Yanga walichagua kutafuta hela ya kumbakisha mayele bado ikashindikana Mashabiki wakasusa kuingia uwanjani.

Simba wamechagua kuwaleta Mashabiki karibu na timu yao kwa kuweka kiingilio rafiki halafu mnataka kuwapangia cha kufanya.Huu ni uzuzu
 
Ni timu mbili tofauti kabisa. Na pia jilani yako akiwa kipele ndio n ww uwe kipele?
Asante.
 
Simba ishaacha kushindana na hawa vyura ,kwasasa inafanya mambo yake,ndio maana Simba inafanya vitu tofauti ili isionekane inashindana na hawa waokota makopo😅😂
 
Kama suala ni hela yafaa nini kuweka kiingilio ambacho hakikupi hela? Kuweka kiingilio cha 10000 sio guarantee kwamba utapata hela nyingi kuliko alieweka kiingilio kidogo.
Yanga iliingiza mashabiki 44000 kwa kiingilio cha 10k. Simba hata mjaze Uwanja full house kwa 5k hamfikii hiyo hela ya Yanga.
 
Mimi ni mwanachama kabisa wa Simba sio Tu shabiki...
Naona kama lengo lilikuwa kuonesha uwezo wa Simba kujaza uwanja ...kulinganisha na Yanga ambao walishindwa ...Simba wangeweka kiingilio sawa sawa na Yanga ..... kiingilio cha elfu 10 minimum....

Hapo sasa ingekuwa nafasi nzuri ya kuonesha watu Simba ina mashabiki wa kujaza Uwanja bila kujali kiingilio....

Nafikiri hata uwanja ukijaa Hadi mwisho kabisa mradi kiingilio ni nusu ya walichoweka Yanga ...sioni kama ni jambo la kujivunia Sana...

Nafikiri ..next time hili swala litazamwe . Uwanja usilazimishwe kujaa Kwa kiingilio cha chini...

Yanga walitest soko Kwa elfu kumi wakashindwa....Simba wawe wa Kwanza Tanzania Kwa kujaza Uwanja Kwa elfu kumi....hili liwe sehemu ya malengo..timu ipate hela pia sio sifa za kujaza Uwanja tu
Ikiwa uwanja ume jaa simba wameingiza bei gani?
 
Yanga iliingiza mashabiki 44000 kwa kiingilio cha 10k. Simba hata mjaze Uwanja full house kwa 5k hamfikii hiyo hela ya Yanga.
Hongera kwa kujifariji. Wapi na lini yanga walitamka wameingiza hao mashabiki?
 
Back
Top Bottom