KUPANGA NI KUCHAGUA.
Unaweza kuwanunua waandishi na wachambuzi ili kuwaaminisha watu kila unachofanya wewe ndio kuzuri na kila wanachofanya wenzio hakina maana yoyote ni kila kinachofanywa na wengine na sio wewe basi hicho kitu ni kitu cha hovyo.
Unaweza kuwadanganya watu wachache kwa muda mfupi ila kumbuka huwezi kuwadanganya watu wengi tena kwa muda mrefu.
Unaweza kutengeneza bahasha nyingi sana ili kuwatuma chawa wako wakawaaminishe watu mtaro ni mkubwa kuliko mto. Au kwa kuwa unatoka mkoa wa Kilimanjaro basi utake watu waamini bwawa la nyumba ya Mungu lina samaki wengi kuliko ziwa victoria.
Unaweza kuwahadaa watu kwa kuacha kuzungumzia ukubwa wa tukio na kubuni kitu cha kuhamisha ujenzi wa ujenzi wa daraja kubwa la mto rufiji ili tu kufanya anayejenga daraja hilo aonekane ni mdogo kuliko kuliko anayejenga daraja la mto ng'ombe kwa kuwa tu nia yako ni kudogosha mambo makubwa yanayofanywa na walio sio wa upande wako. Au ukabeza nyumba inayojengwa ila ukazisifu nondo zinazojenga nyuma.
Ukifanikiwa leo kuwahadaa watu kwa kuwatuma chawa wasifu kila unachofanya na kubeza kila wanachofanya wengine kuna siku watu watajua na utajikuta uko uchi na utashindwa kuificha aibu yako.
Kuna uzi mwembamba sana umebaki kwa waandishi na wachambuzi kujitenga. Wapo watakaobaki na heshima na wapo watakaovuna aibu.
View attachment 2289378