Simba leo mmetia aibu kuomba viatu kwa wachezaji wa Sevilla

Simba leo mmetia aibu kuomba viatu kwa wachezaji wa Sevilla

Video inaonyesha jamaa anaulizwa unataka kulamba viatu vyangu ama kunibusu miguu, bahati mbaya hawaelewani lugha.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Duh watu mnachekesha saana..hicho ndo mlichokiona makwasukwasu
 
Mkuu kumbe ulidhani makwasukwasu wanatumia akili kufikiria???
Just kama kumbu kumbu tu, sio kwamba wanaomba kisa umaskini.

Wakati mwingine tutumie vichwa vyetu kureason not otherwise!
 
Mkuu nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa, lakini hali anayopitia Yanga na vilabu vingine vya Tanzania ni jambo la kawaida hii inatokana na mfumo wa soka letu kutotaka kubadilika.

Ukiachana na Azam, Kagera na Mtibwa hivi vilabu vingine vyote hali zao zinafanana.

Yanga tumekubali, tumejikubali kuwa sisi ni maskini hivyo hatuna vyanzo vingine vya mapato zaidi ya kutoka kwa wanachama wetu wenye mapenzi mema na timu yao.

Hii hali ni kawaida hata kwenye makampuni binafsi hata serikalini mambo yanavyoenda kombo kunakupunguza mishahara ama kupunguza wafanyakazi....sio swala la aibu.

Tatizo ni pale inapotokea kwenye club ambayo imechukuliwa kuwa mfano kwenda kwenye soka la kisasa.

Simba kwa sasa ina mwekezaji ambaye alitangaza kuingiza zaidi ya bilioni 20 kwenye uendeshaji wa club.

Lakini kinachoonekana ni kama kiinimacho tu, Mo ni tajiri ila Simba ni Maskini tu.

Salamba wakati anaomba viatu alionyesha kabisa anashida ya viatu vya kuchezea na si kwa ajili ya kumbukumbu..

Hitimisho ni kwamba Simba na Yanga haziitaji kuchekana kuhusu umaskini na utajiri wote tuko sawa.....

Wote tunahitaji mabadiliko ya kweli kufika kwenye soka la kisasa.

Mkuu aya mbili za mwisho umenema vema. Hayo ya nani kafanya nini hayana msingi.
Mkuu, sina lengo la kutaka kujionyesha kuwa nimebahatika kutembelea huko nchi za wenzetu, ila nataka nikujuze tu kuwa kitendo cha Salamba si kwamba ni kipya huko duniani mpaka unasema ni aibu kwa taifa. Ni kipya kwetu kwa maana ya kukosa exposure. Ni la kawaida sana ila kwa vile sisi ndiyo mara ya kwanza kuona na tukichanganya na ushabiki basi tunamaliza maneno mpaka mengine ya kebehi.

Nilishawahi kushudia mwenyewe kwa macho yangu jamaa aliombwa siyo viatu tu bali hadi soksi. Haikuwa gumzo kama unavyowaaminisha watu kwa mada yako hii mkuu.

Sisi wabongo tuko almost addicted na ushabiki na pengine ushamba wa exposure. Nakumbuka kuna wakati mchezaji mmoja wa Taifa hapa bongo nusura alipishwe jersey ya taifa pale alipobadilishana na mchezaji mwenzie wa nje, sikumbuki nani vile, ila ilitokea hivyo. Ilionekana ni jambo la makosa kama unakumbuka. Hivyo Ni sawa sawa na wewe uliyeanzisha uzi huu, nadhani ni mara yako ya kwanza kuona. Huna makosa kwa hilo. Ila nadhani umejifunza kwa mfano wangu na baadhi ya picha zilizowekwa kama mfano hapo juu. Siku nyingine usikurupuke.

Samahani, mimi mwenzio wa hali zetu za bakuli, wala si dhambi kuchangishana. Ila kuelimishana ni bora zaidi kuliko umoja wetu wa ushabiki au upenzi.
 
Video inaonyesha jamaa anaulizwa unataka kulamba viatu vyangu ama kunibusu miguu, bahati mbaya hawaelewani lugha.
Wenzenu wameweka kumbukumbu we unapi Soga humu.. Hv Zahera amewaambia nini kutoka kapa mwaka huu?
 
Nadri Haroub (Canavaro) amewahi kubadilishana jezi na Etoo wa Cameroon lakini ilizua kasheshe akaambiwa akate tiketi aifate.. ilikuwa timu ya taifa
Haya mambo ni ushamba wetu tu ila ni mambo ya kawaida mno kwa wachezaji
 
Nadri Haroub (Canavaro) amewahi kubadilishana jezi na Etoo wa Cameroon lakini ilizua kasheshe akaambiwa akate tiketi aifate.. ilikuwa timu ya taifa
Haya mambo ni ushamba wetu tu ila ni mambo ya kawaida mno kwa wachezaji
Umenikumbusha mkuu. Mtoa mada nimempa mfano huo (sikukumbuka hili jina la mchezaji) ingawa ni mshabiki mwenzangu.
 
Yiu
20190422_195534.jpeg
 
Back
Top Bottom