Simba mmefanikiwa kusonga mbele lakini rekebisheni mapungufu yenu haraka kabla amjakutwa na aibu mbele ya safari

Simba mmefanikiwa kusonga mbele lakini rekebisheni mapungufu yenu haraka kabla amjakutwa na aibu mbele ya safari

Nyie akuna cha ligi ya bara wala nini, mapungufu yenu yapo kote kote mnayo bahati tu mmekuwa mnakutana na timu ambazo zinashindwa kuwapelekea moto, rejea mechi ya geita gold uliona kitu gani ebu niambie, pia rejea mechi na ruvu shooting uliona nini,,,,Kama unauelewa mpira na sio shabiki oya oya utanieleza ulichokiona kwenye izo mechi kiufundi na sio blah blah!
Mind your business

Sent from my LDN-L21 using JamiiForums mobile app
 
Naona utopolo wanajiamini sana kuelekea 11 Dec, ila niwatonye tu kuwa derby huwa haipo kama mnavyodhani, mnaweza kufungwa na msiamini.

Simba katinga makundi ya CAF Confederation CUP nyie mnatamba huko matopeni bila rekodi yoyote ya maana.

Simba inabaki kuwa bora juu yenu kwa rekodi muhimu za kimataifa.
 
Simba rekebisheni makosa yenu mapema vinginevyo msije mkaanza kuwananga wachezaji kuwa wamewahujumu timu yenu bado Sana kiufundi na kibaya zaidi yamekuwa ni mapungufu ya kujirudia rudia ina maana kocha ajaona icho kitu au anasubili aibu tarehe 11
Umeshindwa kuvumilia utopolo wako...
 
Ila kiukweli Jana simba walicheza kijinga Sana n Kama walivocheza na geita inatakiwa wasajili beki wakat wa maana, pia namba nane wakueleweka, na top striker
 
Tungeshauriwa na timu inayoshiriki michuano ya CAF, hapo sawa. Sasa utopolo wanashiriki nini?
Maajabu haya... Utopolo iliyotolewa mashindano ya CAF bila kufunga hata goli moja eti wamekuwa washauri!!
 
... wewe umemeambiwa unakurupuka kujifananisha na yanga, na halafu kila siku mnasema yanga sio saizi yenu
Ni kweli Yanga sio saizi yetu, na ndio maana hattaki ushauri wao. Ni sawa na Musukuma kumshauri Kitila Mkumbo (alaa, kumbe wote ni madaktari, sorry)
 
Umbumbumbu wenu utaonekana iyo trh 11, Kama kocha wenu atakuwa na akili Kama zako tutashuudia viti vikivunjwa kwa Mara nyingine pale kwa mkapa
zuzu kweli.acha kuruka ruka tunajadili mechi ya Simba vs Red Arrows.

Unaijua derby ya kariakoo au ndiyo wale watoto wa leo kujifanya ujuaji.

Unafananisha mechi za kimataifa ambazo wewe ulitolewa mzunguko wa kwanza na derby ya kariakoo!

Kumbuka tu siyo Simba wala Yanga ataenda uwanjani akiwa na uhakika wa kushinda hata km una kikosi kizuri kiasi gani.Ni mechi inayoamuliwa na mambo mengi sana.

Hata simba iwe mbovu kiasi gani,hata yanga iwe hoi kiasi gani na kinyume chake,hiyo Ni mechi ngumu inapokuwa Kariakoo Derby.yeyote ktk mazingira yyte aweza kushinda.

Narudia Ni mechi inayoamuliwa na mambo mengi,mengine hata hayahusiani na ubora au udhaifu wa timu.
 
Paschal wawa muda mwingne wanamuonea.
center back walikuwa wawili, yeye na inonga au muda mwingne onyango au kennedy na juu yao yupo kiungo wa chini...sasa imekuwa kila goli afungwalo simba ni WAWA.

Tatizo mama la simba kwa sasa, ni kupoteza uwezo wa kumiliki mpira au kukaa na mpira.

Simba ya msimu huu haimiliki mchezo..ukishafanikiwa kuposses mpira muda mwingi, magoli huja yenyewe..

Mwaka jana simba ilikuwa na striker mmoja tu, tena na yeye hakuwa mfungaji (mugalu)...magoli yalitoka kwa viungo.

Leo unashangaa hata timu kama Geita sports inatawala mchezo dhidi ya simba kwa muda mwingi kipindi cha pili..

Simba hawajawahi kuwa wazuri wakiwa hawakai na mpira (kupaki) ni lazima wafungike tu..
rejea zile hamsa za as vita na al ahly 2018/19
 
Back
Top Bottom