kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Hakuna timu ambayo inataka mechi yake ya nyumbani ya Simba na Yanga ichezwe saa 8 mchana. Hakuna mdhamini wa timu ambae anapenda mechi ya timu inayoidhamini icheze mechi zake na simba na yanga saa 8 mchana. Mwenye haki ya matangazo asilani hawezi kukubali mechi za simba na yanga zichezwe mchana wa saa 8 au kwenye uwanja mbovu. TFF na bodi ya ligi bila yanga na simba wangeshakufa njaa mchana kweupe. Kutokana na idadi kubwa ya mashabiki na uwekezaji mkubwa unaofanywa na simba na yanga kwenye miundombinu, mabenchi ya ufundi na wachezaji wadau wote kuanzia wauza maji viwanjani, wauza jezi, timu, nk wanazoa fedha kutokana na yanga na simba.
Heshima ya mpira wetu inatokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na simu za simba na yanga na uwepo wa mashabiki wao wengi; wanaingia hasara kubwa kuliko mapato.
Wachambuzi kuna mambo ya kipuuzi ambayo wanahoji kuhusu simba na yanga wakitaka eti hadhi yao kwenye ligi iwe sawa na timu nyingine kwenye kila kitu. Wachambuzi uchwara hawa ambao uwezo wao wa kuwaza ni mdogo sana. Eti wanahoji kwanini Simba na yanga hawachezi mchana, wanabadilishiwa uwanja, wanasikilizwa, wanapendelewa, sijui nini na nini!!!.
Utaifananisha Simba na KMC au Yanga na Tanzania Prisons? Yaani Yanga ikacheze mpira kwenye uwanja wenye magugu, manyasi marefu, mashimo na madimbwi sana na timu ya Geita Gold au Mgambo JKT?
hatuna wachambuzi bali tuna mbuzi.