Sultan MackJoe Khalifa
JF-Expert Member
- Nov 24, 2022
- 6,782
- 14,148
Ukweli mchunguNimeangalia game ya Mamelody Vs Cotonsport. Mamelody wametimia kila idara aisee. Wachezaji wapo sawa kuanzia akili na miili.nimefatilia nikagundua wachezaji wa Mamelody sio wachezaji wa bei rahisi na wa kuokoteza.
Timu masikini azifiki nusu wala fainali CAF, kufika huko ni lazima kwanza kikosi kiwe na wachezaji wenye kiwango ambao ni ghali kuwalipa achilia mbali mishahara yao.
Msemaji wa Simba amesema malengo ya Simba ni kufika nusu fainali, msemaji wa Yanga aliyefungiwa alisema msimu huu Yanga watabeba ubigwa wa CAF.
Wanatudanganya sisi mashabiki kwasababu tunapenda kusikia maneno mazuri na sio kuambiwa ukweli wa mambo namna yalivyo.
View attachment 2520897
Utajiri wa vilabu muda mwingine hutokana na hali ya uchumi wa nchi husika. Kuna vilabu vina thamani kubwa lakini kimichezo viko chini. Nchi za Afrika ya kaskazini na Afrika kusini uchumi wa mataifa yao ni mkubwa ndiyo maana si ajabu kukuta timu mbovu toka huko ikiwa na market value kuliko vilabu vikubwa na maarufu vya Afrika ya kati, mashariki na Afrika magharibi.
Imagine Okwi, Mugalu, Michael Sarpong wako Arabuni wanacheza ilihali hapa bongo hawana nafasi tena.
Mfano kwa sasa timu nyingi za Tanzania zina thamani kubwa kwenye soko kuliko timu karibia zote za Zambia. Lakini likija suala la kiushindani vilabu vingi vya zambia viko juu ( ukiziacha Simba na Yanga).
Hata hivyo hoja yako inabaki kuwa sahihi, Simba na Yanga husajili kwa kuokoteza, hawana ubavu mbele ya giants wa CAF.
Ukiweka 10,000/= utakomea watazamaji 100 tu. Uchumi wetu uko chini kwa maana ya vipato vya washabiki na wafuasi wengi ni masikini.Viingilio kwenye mechi buku tatu,timu itakuaje na hela!?
Hali ya wananchi wenyewe tia maji weka kiingilio elfu 20 uone kama wataingia uwanjaniViingilio kwenye mechi buku tatu,timu itakuaje na hela!?
Na yule mwenye wachezaji wa elfu kumi kumi yeye lengo lake la kufika nusu fainali bado lipo?Huyo Ashura cheupe naona lengo la CAF limeshakufaga kwa sasa limebaki la kumfunga TP mazembe...
Hao wachezaji uliowaona wakija Bongo wanalipwa zaidi kuliko wanapochezea. Kwa taarifa tu ni kwamba hiyo Cotton Sports haina hata mchezaji mmoja anayefikia mshahara wa BoccoTimu masikini azifiki nusu wala fainali CAF, kufika huko ni lazima kwanza kikosi kiwe na wachezaji wenye kiwango ambao ni ghali kuwalipa achilia mbali mishahara yao.