Simba na Yanga ni uchawi unaotumiwa kupumbaza akili za vijana Watanzania

Simba na Yanga ni uchawi unaotumiwa kupumbaza akili za vijana Watanzania

Unakaa Nyagwa wewe,yaani balala mpiganie klabu zingine zije kuwa na fanbase kubwa kama hii klabu kubwa na zicheze mpira wa kuvutia kama Simba, eti unataka ifutwe,tutwa wewe kwanza

Shubaaat
Kwa hiyo wakicheza vizuri ww unaambulia nini!?
 
Sasa si Bora tushabikie mpira wewe unataka tujadili siasa za mamluki wa CCM
Mi nakuhakikishia kama kelele za kupinga mambo maovu yanayoendelea ndani ya nchi zingekuwa kubwa kama zinavyopigwa kelele za mpira nchi hii mambo maovu mengi yangekuwa yamekwisha kabisa
 
Madhumuni ya uanzishwaji wa Club ni kuwapa wanachama furaha na sio kuwapa profits, so hiyo furaha kama unaweza iweke in monetary form na kuitax ndio mapato yao hayo.
 
Kama ilivyo, kwenye jamii tuna daktari, Mwalimu, nesi, msusi, mfanyabiashara, rubani, askari, dereva n.k basi kuna watu wanapenda mpira, siasa, uchumi, ngumi, riadha n.k.
Ww wapend siasa, tuache siai tupende mpira. Waase wenzako wapenda siasa mpigane vikumbo huko na sisia huku kwa yanga na simba tupigane vikumbo maana tunaoata raha.

Ni bahati iliyoje nchi yetu kua na hivi vilabu viwili vikubwa. Kenya wanatamani wangekua na yanga na simba lkn ndo hawawezi.
Mkuu hebu tofautisha hobi na ishu ya maslahi maana unaweza ukawa na hobi ya kucheza au kupenda mpira then serikali ya ccm unamiliki viwanja vyote na haitaki kuviboresha unategemea utakidhi haja ya hobi yako?
Mfano mwingine unapenda mpira lakini marefa wanakula rushwa ili kuisaidia yanga ishinde kwa namna yoyote hauoni kwamba unahitaji serikali imara kudhibiti rushwa!?
 
mleta mada hoja yako ni ya ukweli kabisa hasa kwa miaka hii ya 2015 kuja mbele ,kutokana na kuzuiwa mikutano ya siasa kwa vyama vya upizani,bunge live kutokurushwa ambapo hoja mbalimbali zinazohusu taifa zilikuwa wazi ,viongozi (whistle blowers ) kufungwa au kufanyiwa figusu za za makusudi wanapokosoa,imefanya vijana wengi kutokujadili siasa kama hapo nyuma.2005 hadi 2015 kujadili siasa ni mada zilikuwa zikitrendi katika mikusanyiko yeyeto hapa tz tofauti na sasa .Media zilikuwa huru kukosoa ,sasa wamefungwa midomo kwa sheria mbalimbali mambo ambayo ni huru kujadlili ni michezo na ndio maana unaona kizazi hichi kipo hivyo
 
Mijadala ya mpira ni huru na hakuna hofu ya mtu kukamatwa kwa kumtukana ama kumsema vibaya kiongozi wa Yanga/Simba, mvhezazajinwa Yanga/Simba ama kiongozi wa TFF.

Wakati huku kwenye siasa, kiongozi wa awamu ya tano alianzisha kampeni ya kuwaweka ndani wale wote wanaomsema vibaya.


Kampeni hii mbovu ya kuwakamata watu wanaomkosoa jiwe ndiyo iliyosababisha watu kujiepusha na mijadala ya siasa.

Awamu ya nne mambo yalikuwa fire kweli kweli. Jiwe akaja akaharibu nchi
Mpk Leo hii Kuna makovu makubwa ambayo yalisababishwa na huruka za jiwe kudhibiti mijadala.

Siku zote tumesema kuwa jiwe angeendelea kuwa hai nchi ingetumbukia shimoni
 
Mkuu kila mtu hawezi kuongelea siasa, ushabiki wa mpira upo kwa kiwango cha juu hata uingereza lakini hakujazuia watu kuhoji mambo ya msingi kutoka kwa wa-twawala.....
 
Naona umefura sana ndugu ila nataka uelewe kwamba kwenye stratejia ya siasa moja ya kete muhimu ni kuona unaowaongoza wanatumia muda mkubwa kujadili mambo yasiyogusa majukumu yako hii inakupa wewe nafasi ya kulialia kiti kwa amani sana. Kuwa shabiki sio dhambi lakini kutumia robo tatu ya muda wako wote kuwaza na kujadili mpira ambao haukuingizii hata mia lazima kuna tatizo!
Uko sahihi, kuna watu ambao hawajui ht mlo unaofuata utatoka wapi lakini utawakuta wamekaza mishipa ya shingo wakitumia nguvu kidogo walizo nazo kubishania Manara, Mo na timu zao, pathetic.
 
Mkuu kila mtu hawezi kuongelea siasa, ushabiki wa mpira upo kwa kiwango cha juu hata uingereza lakini hakujazuia watu kuhoji mambo ya msingi kutoka kwa wa-twawala.....
Wazungu huwa wanashabikia mpira kwa mbwembwe wakiwa viwanjani au wanaangalia mechi tu baada ya hapo wanajikita kufanya mambo mengine ya maendeleo, sio kuendelea na mijadala isiyoisha ya mpira kila mahali.
 
Ni jambo la fedheha mpira wa Simba na Yanga huwa unajadiliwa hadi bungeni!
 
Kabisa mleta, Magufuli ndio aliondoa mijadala ya wananchi kujadili maisha yao bali wajadili mpira tu wa simba na yanga. Alihakikisha mijadala pekee ni ile ya kumsifia, na mingine iwe ni ile isiyoenda kinyume na utashi wake. Aliwageuza wananchi kumuamini yeye bila kuhoji, na ukihoji au kukosoa sio mzalendo. Na vyombo vya habari vilikuwa salama kumsifia, ama kujadili mpira.

kwa hili Magufuli alifanikiwa. Kwa sasa watu wanajadili zaid mpira kuliko hata kukosekana kwa maji au umeme! Na viongozi wanafurahi maana hawapati pressure.
Msipende kumsingizia kila kitu Magufuli. Why mpaka leo mnaishi kwa kivuli chake wakati mtu ameshajifia zake. Watu wameacha kujadili siasa baada ya kuona ni ulaghai mtupu.

Unakuta mwanasiasa wa upinzani anaipinga Serikali kila siku, lakini akipewa nafasi yeye hata ya ubunge tu, hakuna lolote analolifanya zaidi ya kujineemesha yeye na familia yake. Wengine tumewaona wamepata nafasi za kisiasa wanaweka ndugu na mahawara wao huku wananchi wakiendelea na shida zao. Ndo maana watu wameona ni bora wajadili vitu vinavyowapa furaha kama mpira kwasabbu wanasiasa siyo wakweli bali ni wachumia tumbo tu.
 
Msipende kumsingizia kila kitu Magufuli. Why mpaka leo mnaishi kwa kivuli chake wakati mtu ameshajifia zake. Watu wameacha kujadili siasa baada ya kuona ni ulaghai mtupu.

Unakuta mwanasiasa wa upinzani anaipinga Serikali kila siku, lakini akipewa nafasi yeye hata ya ubunge tu, hakuna lolote analolifanya zaidi ya kujineemesha yeye na familia yake. Wengine tumewaona wamepata nafasi za kisiasa wanaweka ndugu na mahawara wao huku wananchi wakiendelea na shida zao. Ndo maana watu wameona ni bora wajadili vitu vinavyowapa furaha kama mpira kwasabbu wanasiasa siyo wakweli bali ni wachumia tumbo tu.

Wapi ww, Magufuli ndio aliyezuia watu kujadili siasa ili awatawale kwa shuruti. Unasema watu wameamua kujadili mpira maana wameona wanasiasa ni waongo na wanafaidika na familia zao. Kwani huko kwenye mpira ndio wanagawana pesa na wachezaji? Acha Utetezi dhaifu kwenye ukweli.
 
Kwasehem naungana na mtoa mada,ukienda Mbeya-Uyole,NJIA panda wanapouza magazeti,utakuta vijana KWA wazee tangu sa nne asubuh hadi sa nne usiku wapo wanajadiri mpira,celebrities kama diamond,Alikiba,Harmonize n.k Wengi wao ni jobless.Kinachoumiza zaid Wengi wao ni vijana ukiwauliza sera ya vijana kitaifa inasemaje?hawajui!Panahitajka elimu pana ktk hili
 
Mkuu kila mtu hawezi kuongelea siasa, ushabiki wa mpira upo kwa kiwango cha juu hata uingereza lakini hakujazuia watu kuhoji mambo ya msingi kutoka kwa wa-twawala.....
Sio lazima iwe siasa lakini kwa nini mbona tuna changamoto lukuki ambazo wala hazizungumzwi mfumo mbovu wa elimu uhaba wa ajira kupanda bei za bidhaa haya ni baadhi ya mambo ambayo ninadhani yakishupaliwa kwa hisia kali kama ilivyo kwa mpira viongozi wetu lazima wataona kwamba vibarua vyao viko mashakani
 
Ndugu wanabodi naweza nisiekewke kirahisi kuhususiana na hii hoja yangu, lakini nimekaa na kutafakari mambo kadhaa:

Mijadala inayohusu mpira wa miguu hapa nchini imekuwa mingi na inachukua muda mwingi sana, ina wafuatiliaji wengi na wachangiaji wengi.

Na kwa kulifahamu hilo ndio maana zimeibuka media nyingi sana zinazojihusisha na mambo ya kuchambua na kuuzungumza mpira wa miguu.

Hata hivyo uchambuzi wote unakuwa na maana au kukolezwa na uwapo wa simba na yanga. Kwa maneno mengine ukifanya uchambuzi ama utangazaji wako kama hautazungumia simba ama yanga basi jua dhahiri mjadala wako utakudodea.

Wapenzi na mashabiki wa vilabu hivi huvizungumzia kwa hisia kali sana ni kana kwamba vinawasaidia kupata kipato chochote kumbe ni mapenzi tu.

Na ukitaka kushuhudia uchizi na nguvu ya hawa wapenzi wa hivi vilabu, basi patokee jambo wasilolitaka pale clabuni, yaani utawashuhudia wanafura kana kwamba mtu kaibiwa hela yake.

Yaani wana nguvu ya kumtoa yeyote na kumuweka yeyote wamtakaye ilimradi tu wafurahie wawe na cha kumnanga mtani.

Jambo hili lina athari hasi sana kwa vijana wetu kwani kwa kadri wanavyotumia muda mwingi kujadili mpira wanatengeneza ombwe kwenye mijadala inayohusu mustakabali wa taifa letu na changamoto zake.

Amini usiamini kusipokuwa na presha ya kutosha ya mijadala inayotoka kwa umma, watawala na viongozi wanabweteka hawaumizi vichwa juu ya namna bora ya kutatua changamoto za watu wao!

Maana kiongozi akfungua redio anasikia simba wanalia "mrudisheni chama" ikiisha hiyo atasikia tena "huyu mayele ni zaidi ya mesi"

Alafu watu wanabishania hayo tangu asubuhi jioni . Wengine wanaishia kupigana. Unadhani huyo kiongozi atapata tabu ya kuumiza kichwa juu ya vitu kupanda bei?

Kama hiyo haitoshi niliwahi kuwa na rafiki yangu Kutoka nchi ya Uganda alishangaa sana kuona muda wa kuongelea yanga na simba unavyotuchukulia akili nyingi na muda mrefu badala ya kujadili matatizo yetu.

Napendekeza kama ikiwezekana hivi vilabu vifutwe ili watu wajadili maendeleo na sio kutwa kucha kujadili mpira.
Mahali popote kulipowahi Kutokea mageuzi yoyote, ni kwamba yale mageuzi yaliletwa na mijadala mingi ya umma.
Watz wengi wamekuwa na wajinga saaana hasa vijana kwa ajili ya mambo ya mpira yasiyo na majibu ya maisha yao.

Hii naiona sana hapa Tz,mambo wanayopaswa kuyafanyia mjadala na kuchukua hatua wanakaa kimya
 
Kwa hyo kuacha kushabikia mpira ndo hizo changamoto zitaisha?ebu tumia approach nzur ya kufikisha ujumbe wako..mm nlidhan ungekuja na strategies za ni namna gani vjana tufanye ili kuweza kuipa challenge serikali iliyoko madarakan na c kuwakataza kitu wanachokipenda ili uwaforce unachokipenda ww....vile vile ingetakiwa ujue kila mtu ana hobbies zake kama ilivyo ww kupenda siasa wengine wanapendelea ushabik wa mpira...tusipangiane namna ya kuish
Mapenzi mengine ni ujinga tu,mapenzi na mpira ni umbumbumbu na ulevi mbaya sana
 
Kwa hyo kuacha kushabikia mpira ndo hizo changamoto zitaisha?ebu tumia approach nzur ya kufikisha ujumbe wako..mm nlidhan ungekuja na strategies za ni namna gani vjana tufanye ili kuweza kuipa challenge serikali iliyoko madarakan na c kuwakataza kitu wanachokipenda ili uwaforce unachokipenda ww....vile vile ingetakiwa ujue kila mtu ana hobbies zake kama ilivyo ww kupenda siasa wengine wanapendelea ushabik wa mpira...tusipangiane namna ya kuish
Kama unaishi maisha ya kijinga na ya ulevi wa kushabikia mpira kila siku lazima uambiwe kuwa unapotea,huwezi kujua kwa urahisi ila athari ni kubwa kiakili...ni kama nyeto tu
 
Back
Top Bottom