Simba na Yanga: Viingilio ni Sababu, ila kuna kubwa zaidi ya hilo

Simba na Yanga: Viingilio ni Sababu, ila kuna kubwa zaidi ya hilo

Best Daddy

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2019
Posts
950
Reaction score
1,672
Nianze kutoka credit kwa wadau wasoka, mpira wa miguu ni industry pekee yenye muamko na ushawishi mkubwa kwa jamii, nchini Tanzania. Lakini, kama hujaliona hili, basi angalia nyanja ya siasa mfano, watu wengi sasa wanahisi yanayotokea huko basi hayawahusu, ni kama mambo yanatokea kwa jirani vile, wana-feel disconnected kabisa na siasa. Hii kuonesha watanzania tupo nyuma nyuma (hatuna muamko) kwenye mambo mengi. Ndio maana hata Nchi yetu huko duniani haifahamiki pamoja na kuwa na kila kitu kinachoweza i-brand nchi hii.

Turudi katika Soka sasa, I love soccer, lakini sio kila mtu anapenda soka. Sasa wanasaikolojoa wanasema kwamba, mapenzi ya kitu fulani mara nyingi huendana na investment ya muda, hisia, pesa.

Mfano, Nina jirani yangu hapa, anapenda sana Mbwa. Yupo tayari hata kutoa 500k aweze kupata hybrid ya mbwa fulani, lakini mimi mfano hata 5k siwezi toa, sababu sipendi mbwa kabisa.

"Kwanini nayasema haya, Nimeona Waandishi wakubwa, hasa wachambuzi wa soka, akiwemo Edo Kumwembe "The Living Legend" anasema yaani mtu anaweza tumia let's 200k per day(alitaja vitu) lakini huyo huyo anasema kiingilio cha 10k katika match ni kubwa."

Kwa akili ya kawaida unaweza ona huyo jamaa ni mshenzi kweli iIa kuna sababu kubwa ndani ya hiyo kauli. nakuomba urudi kwenye mfano wangu mbwa hapo juu. Utapata jibu.

Wakaenda mbali na kutoa mifano ya mashabiki ulaya, sitaki kugusa issue ya uchumi wao. Ila nataka nizungumzie issue ya mindset.

Swali: Je mashabiki wa ulaya na watanzania tupo sawa katika mindset zetu, hasa yanapokuja masuala ya kisoka?

Hapa ndipo jibu utalipata: Kuna shabiki wa Tanzania yupo tayari kujitoa kwenye timu? Kuna shabiki wetu yupo tayari kushuka daraja na timu yake?
Okay wanaweza kuwepo ila wachache sana.

Sasa ni nini changamoto? Ni kweli maybe viingilio vinaweza kuwa ni vikubwa, ila tusiishie hapo, Vilabu vya Tanzania kiukweli vina LOYAL FANS wachache sana. Wale mashabiki wanaosema tutakua na wewe "evermore" ni wachache sana. Na hapa ndipo wenzetu England wamefanikiwa. Ndio maana hayo mengi tunayozungumza yanayotokea kwao bila nguvu, ila sisi sasa wasemaji na wahamasishaji wa Timu wanakazi sana, vispika vitapita barabarani...alooh.

( Uzi naona umekua mrefu sana. Tutazungumza kwenye comment)

Ila vilabu wajitahidi sana kutengeza loyal fans, wasione kama wana mashabiki wengi, wengine wapo ku-mingle tu, hata wachezaji wao hawawajui. Ukiwa na loyal fans mambo mengi yataenda vizuri sana.

Huo ni mtazamo wangu, je upi mtazamo wako? Kipi kinakufanya usifike uwanjani? Ningependa tusijifiche kwenye kichaka cha viingilio tu.

Wakati wako wa kuzungumza sasa.

N.B. Nashukuru Mungu ile kauli ya "Nilikua nakuheshimu na kukuona mwenye akili, kumbe na wewe ni wale wale mashabiki wa Simba na Yanga"
 
Kusema ukweli mazingira ya viwanja yenyew sio rafik kuna jamaa mwaka jana alinunua tickets ya elfu 30 ameenda zake uwanjani akakuta vile viti vya elfu 30 vimejaa alafu watu waliokalia ni wale walionunua tickets za elfu 5 kuuliza akaambiwa amechelewa, kwahiyo jamaa akaenda kujichomeka level ya chini kabisa tangu siku hiyo jamaa ameapa haendi tena uwanjani haiwezekani anunue ticket ya elfu 30k alafu akasimame level ya elfu 5
 
Kusema ukweli mazingira ya viwanja yenyew sio rafik kuna jamaa mwaka jana alinunua tickets ya elfu 30 ameenda zake uwanjani akakuta vile viti vya elfu 30 vimejaa alafu watu ...
Shukrani Mkuu. Naona umekuja na sababu mpya yanye mfano ndani yake.

Hii itasaidia kutanua mjadala huu kuliko kuishia kwenye suala la viingilio tu.
 
Na kuna akina sisi tunaoweza kununua jezi ila sio kwenda uwanjani kuangalia mechi aisee. Zile fujo na kelele siwezani nazo.
 
Cha muhimu uanzishwe mfumo wa kimtandao ambao utatoa utaratibu wa kununua seasonal tickets (za msimu mzima) au za gemu moja moja mapema tangia msimu unapokaribia kuanza na kuwe na discount kwa wale wanaonunua mapema. Mfano mtu anaweza leo msimu haujaanza anunue tiketi ya mechi ya Simba vs. Mtibwa ambayo labda inategemewa kuchezwa mwezi wa 10.

Tiketi za mapema ziwe na discount ila kwa jinsi gemu husika inapokaribia, bei ya ticketi zilizobaki inaweza kupungua au kuongezeka kulingana na sababu mbalimbali ikiwemo performance ya timu wakati huo.

Timu zitaweza kupata mapato mapema yasaidie katika kuendesha timu lakini pia mashabiki wanaweza kujipanga mapema kifedha. Hili suala la juzi la tamasha la Yanga lingeweza kuepukika kirahisi tu kama tiketi zingeanza kuuzwa miezi 3 hadi 6 iliyopita. Kama tumeamua mpira ni burudani, hii ndiyo njia ya kwenda maana matamasha makubwa ya muziki na hata michezo, tiketi zake huwa zinaanza kuuzwa mapema sana.
 
Kusema ukweli mazingira ya viwanja yenyew sio rafik kuna jamaa mwaka jana alinunua tickets ya elfu 30 ameenda zake uwanjani akakuta vile viti vya elfu 30 vimejaa alafu watu waliokalia ni wale walionunua tickets za elfu 5 kuuliza akaambiwa amechelewa , kwahiy jamaa akaenda kujichomeka level ya chini kabisa tangu siku hiyo jamaa ameapa haendi tena uwanjani haiwezekani anunue ticket ya elfu 30k alafu akasimame level ya elfu 5
Haka katabia kameanza kuota mizizi inakera sana jitu linamnyia security buku mbili linazama upande wa 30k...!
 
Haka katabia kameanza kuota mizizi inakera sana jitu linamnyia security buku mbili linazama upande wa 30k...!
Wenzetu walioendelea ticket zao zinakua na seat number kabisa hata uchelewe vipi seat yako unaikuta wazi , lakin bongo ni kama mbuzi wanavyoingia bandani utakapowai kukaa ndo hapohapo ukichelew imekula kwako , wengine wanatoka majumbani saa 4 asubuh sio kwamba wanapenda ila wanawai seat
 
Alooooooooo.
afrika bado sana
 
Na kuna akina sisi tunaoweza kununua jezi ila sio kwenda uwanjani kuangalia mechi aisee. Zile fujo na kelele siwezani nazo.
Kabisa Mkuu. Nimekuta na hizi kauli kwa watu wengi. Unakuta badala ya kwenda kufurahia, inabaki kuwa ni kero.
 
Wenzetu walioendelea ticket zao zinakua na seat number kabisa hata uchelewe vipi seat yako unaikuta wazi , lakin bongo ni kama mbuzi wanavyoingia bandani utakapowai kukaa ndo hapohapo ukichelew imekula kwako , wengine wanatoka majumbani saa 4 asubuh sio kwamba wanapenda ila wanawai seat
Sure!
 
K
Cha muhimu uanzishwe mfumo wa kimtandao ambao utatoa utaratibu wa kununua seasonal tickets (za msimu mzima) au za gemu moja moja mapema tangia msimu unapokaribia kuanza na kuwe na discount kwa wale wanaonunua mapema. Mfano mtu anaweza leo msimu haujaanza anunue tiketi ya mechi ya Simba vs. Mtibwa ambayo labda inategemewa kuchezwa mwezi wa 10.

Tiketi za mapema ziwe na discount ila kwa jinsi gemu husika inapokaribia, bei ya ticketi zilizobaki inaweza kupungua au kuongezeka kulingana na sababu mbalimbali ikiwemo performance ya timu wakati huo.

Timu zitaweza kupata mapato mapema yasaidie katika kuendesha timu lakini pia mashabiki wanaweza kujipanga mapema kifedha. Hili suala la juzi la tamasha la Yanga lingeweza kuepukika kirahisi tu kama tiketi zingeanza kuuzwa miezi 3 hadi 6 iliyopita. Kama tumeamua mpira ni burudani, hii ndiyo njia ya kwenda maana matamasha makubwa ya muziki na hata michezo, tiketi zake huwa zinaanza kuuzwa mapema sana.
Umenena vyema, Mkuu. Suala la ticket nalo lizingatiwe.
 
Back
Top Bottom