DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Ni kweli, njia ambayo Simba imetumia kufuzu ni ngumu sana. Baada ya kuona goli la ugenini halipatikani, badala ya kuendelea kulilazimisha ilitakiwa kujihami zaidi ili walau irudi ikiwa na deni la 0-1. Yote kwa yote, yaliyopita si ndwele. Sitaki tena kuangalia kilichotokea kule Misri.
Hizi mechi za kushika roho mkononi lakini kuondoka uwanjani kama vile umetoka kutunukiwa na binti uliyemuhangaikia muda mrefu ndiyo zinaitofautisha Simba ni timu zingine zozote nchi hii na hata Africa.
Inawezekana ingeshinda kule Misri au kufungwa kwa ushindi mwembamba au kupata goli la ugenini, Simba ingerudi imerelax yakatokea yale ya Jwaneng Galaxy. Maumivu yale hatuyataki. Inawezekana kurudi ikiwa na deni la 0-2 ni jambo jema sana kwa Simba.
Simba inaenda kufuzu kwenda nusu fainali vizuri tu kwa ushindi wa heshima na itapiga mpira mkubwa sana siku hiyo.