"Simba nguvu moja." Tujadiliane namna ya kuwaua Waarabu na kuongoza Kundi D

"Simba nguvu moja." Tujadiliane namna ya kuwaua Waarabu na kuongoza Kundi D

Huna lolote, simba kwenye hili kombe lazima tuvuke group stages ndio strategy namba moja ya club kama hujui ndio nimekwisha kukujuza.
.
Hapo hakuna timu ya kuitisha simba zaidi ya vita club ya kongo ambao ni majirani zetu wanapanda hata basi hao kuja Tanzania, Al ahly na Js cha mtoto sana kwenye mechi zetu za kwa mchina.
Kujua kwako kwingi muda mwingine kuna kufanya usifikirie nje ya BOX.
Simba akipata points 2 kwenye group lake nipigwe ban wiki2.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ban ya maisha kabisa ufungue ID mpya nawaalika Moderator waone commitment yako

Inaonekana ID hii unaichukia mno kama siyo sana tu. Hii ID itatoweka hapa pale tu nikifa ila kwakuwa nipo hai itaendelea kuwepo na kama unaichukia nakushauri tafuta Sumu ya Panya uinywe huku ukiitaja hii ' Brand ID ' ya GENTAMYCINE utakuwa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.
 
Vipi na Yanga nasikia mmefuzu mmeingia kwenye hatua ya 16 bora ligi ya mabingwa ndondo cup..kutokana na droo iliyochezeshwa Group Z kuna timu za Yanga,Mashujaa,Lipuli na Tukuyu stars...kila la kheri wawakilishi wetu wa kimataifa yanga

Leo hii GENTAMYCINE amekuwa Yanga SC? Kwakuwa tu nimesema ukweli na uwazi bila Unafiki kama mlionao wengi wenu?
 
Tukiwa na umoja Simba hafungwi kwa mchina...Simba ambayo inafungwa kwa mchina au zamani shamba la Bibi in mgogoro au Haina mshikamano...ila tukiwa katika ubora wetu Mzee dalali aunganishe matawi ya Simba tuwe kitu kimoja kwa mchina hatoki mwarabu Wala mwafrica mwenzetu Kama kufia tutafia ugenini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaonekana ID hii unaichukia mno kama siyo sana tu. Hii ID itatoweka hapa pale tu nikifa ila kwakuwa nipo hai itaendelea kuwepo na kama unaichukia nakushauri tafuta Sumu ya Panya uinywe huku ukiitaja hii ' Brand ID ' ya GENTAMYCINE utakuwa umefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.
Umekurupuka mkuu nilim_quote frank kwa maneno yake aliyoyasema simba tukivuna point 2 apewe ban ya wiki mbili
 
Ni Popoma / Mpumbavu tu ndiye atabisha na kujifanya anajitutumua kwa kusema kuwa Simba SC itafanya vizuri mbele ya Wapinzani wake katika Makundi Klabu Bingwa Afrika akina JS Saoura ya Algeria, AS Vita Club ya DRC na Al Ahly ya Misri ambalo Kwangu Mimi ndiyo naliona kama Kundi la Kifo ( au la Mauwaji kabisa )

Mtanisamehe wana Simba SC wenzangu najua ukweli wangu huu utakuwa mchungu Kwenu na utawaumeni mno ila mnivumilie tu na muupokee kama ambavyo huko nyuma nilikuwa nawapeni ukweli na matumaini katika mechi za ndani na hata ile ya Nkana Red Devil.

Hapa hatuna chetu tena kwa 100% ila nawaomba Simba SC waitumie hii michezo na hizo Timu kama sehemu ya Kuwatangaza vyema Wachezaji wetu ili basi waanze Kuonekana na Vilabu vikubwa ama vya Afrika hapa hapa au vile vya Ulaya kusudi tuwauze, tuingize Pesa na tusajili Wachezaji wapya wakubwa na wazuri.

Kwa sasa hivi hii Michuano tuichukulie kama sehemu yetu ya Kujifunza mambo mbalimbali na hasa kupata Uzoefu zaidi ili basi kama na Msimu huu tutabahatika Kuchukua Kombe la Ligi basi Michuano ijayo ya Klabu Bingwa tuingie huku tukiwa tumeshajikamilisha na kujiandaa kwa kila Kitu.

Tusidanganyane Simba SC ya sasa haina ubavu wa Kupambana na hizo Timu zote hapo juu hasa kutokana na sababu Kuu za Kiufundi. Kwa Simba SC ya Beki Pascal Serge Wawa, kwa Simba SC iliyokurupuka Kumsajili Beki Zana Coulibaly, kwa Simba SC yenye Kiungo kama James Kotei ambaye huwa anakata Upepo ( anaishiwa Pumzi ) haraka, kwa Simba SC ambayo ina Kipa Aishi Manula ambaye anafungwa aina ile ile ya Magoli ya Kizembe kabisa kama si ya Kitoto, kwa Simba SC ambayo Kipa wake wa akiba Deogratius Munishi ambaye hajielewi anafanya au anataka nini, kwa Simba SC ambayo ina Winga Shiza Kichuya ambaye Siku hizi Ushamba wote wa Morogoro umemtoka na Kumbi zote za Starehe za Dar anazijua, kwa Simba SC ya Mshambuliaji kama John Boko ambaye kama Mshambuliaji akikabwa tu njiani huwa hana Plan B na kwa Simba SC ambayo hadi hivi leo Kocha Patrick Aussems hana bado First Eleven yake na wala Msaidizi wake kamwe tusitegemee kufanya vyema katika Makundi.

Tunaoujua mpira vyema, Watoto wa mjini, Wazee wa Fitna na tuliocheza mpira kidogo hata kama huko Ligi Kuu hatukufika kwakuwa tulikuwa na Majukumu mengine ya Kimaisha na Kimtazamo kwa CAF kutupangia hizo Timu Nne ( 4 ) tusidanganyane wala kupeana Moyo ' Kingumbaru / Kijinga ' bali hapo ni rasmi Mbuzi ( SSC ) kafia kwa Wauza Supu Watatu mmoja wa Algeria ( Mwarabu ) , mwingine Mkongo na mwingine Mmisri ( Mwarabu )

Akili zetu sasa tuzielekeze mno katika Ligi Kuu ambayo nayo kwa jinsi ninavyoona kama tusipokuwa makini basi Yanga SC au Azam FC watachukua Kombe kwani Kimpira, Kimbinu, Kimkakati na hadi Kisaikolojia wapo vizuri sana kuliko Sisi Simba SC ambao muda mwingi tunakuwa tupo tu katika Presha na tusipotulia Msimu ujao kama kuna Kombe ambalo tutashiriki basi litakuwa ni la MBUZI MAPINDUZI CUP na UPUUZI SPORTS PESA CUP.

Yangu GENTAMYCINE ni hayo tu na mtanisamehe kwa wale ambao ukweli wangu huu utawaumiza ila muuchukue tu!

Nawasilisha.
Unfortunately, wana Simba wenzako watakataa kuona ukweli ulio dhahiri.

Uchambuzi wako hasa kuhusu backline ya Simba kausema Chambeshi, kocha wa Nkana. Kausema King Kibaden mwana Simba kindakindaki.

Ni kundi gumu mno kwa Simba. Kuna watu wanadai eti point tisa kwa Mchina. At most point tano kwa Mchina.
 
Yah kama kawa wa kimaitaifa Leo tumeshapangiwa group letu ambazo zna team kutoka uarabuni moja na wakongo moja .toa ushauri wako tufanyaje tuweze songa mbele katika hatua ya robo final nusu na kulichukua kombe zima tulilete msimbazi karibuni wana SIMBA note YANGA huhusiki hii ni kwa kimaifa tu



Sent using Jamii Forums mobile app
Yanga itahusika vipi huko mnako Jafiliana?
 
Shida yenu uwaga hamtaki kuambiwa ukweli, mleta mada amewasilisha hoja zake kiufundi sana, ameongelea vizuri mapungufu ya club/timu kiufundi kabisa, hata alipozitaja Yanga na Azam fc ametumia jicho lake vizuri kuona mbali.hatukatai Simba inao wachezaji wakubwa, na wako vizuri ukiangalia mchezaji mmoja mmoja, Ila kitimu, kisaiklogia, na kimbinu naungana na mleta Uzi kwamba Azam na Yanga japo wengi hamtaki kusikia hill wako njema bro, sana malengo flani wawapo uwanjani, hata kama timu zao zikiwa zimezidiwa uwanjani, bench I lao LA ufundi uja na plan nyingine ambazo huleta matokeo chanya, hill ndilo halichoona mleta Uzi kwa jicho lake LA kimchezo. Kama Simba atawezi kufanyia mapungufu take ambayo watu wa mpira wameyaonyesha wazi akiwemo mleta mada, basi walau itaambulia hata point 5 kwenye kundi lake wakati ikijipanga vilivyo kwa ajili ya msimu ujao. Otherwise muwatoe kafara wapenzi na mashabiki wenu si chini ya kumi kila mechi kama mlivyozoea. Nakupongeza sana mleta mada maana pamoja na kuwa Simba kindakikindaki, ila ukweli umeuona na umeueleza wazi. Simba Nguvu Moja in pamoja na kukubaliana na mapungufu uliyonayo na kuyarekebisha kwa ajili ya kuboresha, siyo kupinga tu bila akupaye changamoto. Ni hayo tu. Alafu mkuu Genta Sikh nyingine usiwape mbinu za kushinda hao jamaa zako uone watakavyoooga nyingi hapo hapo kwa mchina, ushauri wako ulioutoa kwa Nkana, nilikuvulia kofia, so kwa ulozi hule.
unajiona unajua mwenywe kumbe takatakata tupu.
et unasema yanga na azam wapo vzr kuliko simba..
yani umeongea upuuzi apo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu tunashukuru kwa maoni yako, haya uliyoandika yote yanafanyiwa kazi

kuanzia kipa hadi staker, maana tuna nafasi zaidi ya tatu kwenye usajili

so atapatikana kipa, beki 1 wa kati na straker, pia simba wana lengo la kuchukua kiungo wa kusaidiana na jonas mkude

hadi hapo unaweza kuona kwamba mipango ya simba si ya kuishia hatua ya makundi
 
Afrika husiposhinda nyumbani husitegemee kushinda ugenini hii inatokana na fitina za ugenini tofauti na wenzetu ulaya.

Hivyo kwa uwekezaji wa simba ilionao na aina ya wachezaji ilionao robo itafika kwa kushinda mechi zote nyumbani,kumbuka ni timu pekee ukanda huu kufika makundi.
Hata last year timu iliyoitoa simba shirikisho ilikuwa ni bora ndiyo maana nayo ilitolewa nusu fainali
 
Back
Top Bottom