changaule
JF-Expert Member
- Jan 10, 2020
- 6,039
- 10,151
Nakurudisha kwenye mstari maana unasema naleta mada bila kufikiri, na mimi nataka kukuonyesha nilijua mtataja hatua za makundi na vinchi hivyo ambavyo kwa sababu ya njaa vimejiunga jumuiya za kiarabu ila kiuhalisia siyo na ni nchi ambazo hazijawahi kuwa tishio katika mpira wa Afrika. Scars alijaribu kufafanua hoja yangu jana ila ndiyo hivyo uelewa wenu bado ni duni.
Unataka nitumia Google, ukiingia huko Google na Quora utaona waarabu wenyewe wanakwambia sababu za nchi kama Somalia na Djibouti kukubaliwa na kwa nini nchi zingine ambazo zinakidhi hivyo vigezo kuliko hizo nchi kama Chad na Mauritania zimekataliwa. Ndiyo maana nakwambia ukiwa mpole naweza kukupa tuition. Tanzania bila Nyerere kuingilia kati ingekubaliwa huko, bado swali langu liko pale pale, je sisi ni waarabu?
Kumbe hata Scars hukumuelewa, wewe kwa akili yako ulijua anakuunga mkono kwa uzi wako kumbe wala hajakubaliana na hoja yako kuwa Simba ndio timu ya kwanza kucheza away dhidi ya timu ya kiarabu.
Njoo tumalize ubishi kwenye mechi iliyofanyika October 8 mwaka 2022 mechi ya CAFCC kati ya Azam vs Al Al akhdar
Je Azam ilianzia wapi home au away?
Je Al Al akhdar ni timu inayotokea nchi gani?
Jibu swali kama ulivyoulizwa ili uone ulivyokurupuka kuanzisha uzi usiofanya utafiti kabla ya ku post.