Simba Queens ni mfano wa kuigwa namna taasisi imara inavyoendeshwa kwenye mpira!

Poker

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
5,445
Reaction score
14,828
Simba queens imekuwa timu ya kwanza ya wanawake kutoka Tanzania kwenda kushiriki ligi ya mabingwa Africa.

Hapo unaona uwekezaji mkubwa unaofanywa na mo dewji ukisimamiwa na mwanamama babra Gonzalez ambaye ni moto wa kuotea mbali kwenye usimamizi wa taasisi ya mpira. Simba kwa sasa sio level tena za yanga, na ikiwapendeza watani zetu waje wakae mezani na sisi wajifunze namna ya kuwa taasisi bora katika kila nyanja!

Hii simba queens itafika mbali ikiwemo kutinga fainali na hapo bado mo dewji ameahidi kuwapandishia mishahara wachezaji wote ambapo opah clement atakuwa akipokea milioni 5 kwa mwezi huku corazone akivuta milioni 4 kwa mwezi.

Hongereni simba sc hakiks mnajua namna ya kuendesha club tofauti na wapiga porojo wa jangwani!

20220828_120323.jpg
20220828_120218.jpg
20220827_215422.jpg
20220827_211041.jpg
 
Hawa Queens siku moja wapewe match na Yanga kubwa.
Msimu uliopita walifungwa na Yanga princess, halafu Yanga unayoingelea hapa mayele katoka kukubong'oa mara 2 hata wiki 2 azijapita, sasa hao queen wenu mayele atawabong'oa hata mara 100
 
Siku zinaenda Kasi sana. Kumbe baada ya kuona huku kwenye soka la wanaume tunapigwa gape na hawa Utopolo basi tumeona tuhamishie nguvu huku kwenye soka la dada zetu.. sio mbaya tutafika tu
 
Msimu uliopita walifungwa na Yanga princess,halafu Yanga unayoingelea hapa mayele katoka kukubong'oa mara 2 hata wiki 2 azijapita,sasa hao queen wenu mayele atawabong'oa hata mara 100
Sasa mkuu mbona unapovuka kiasi hiki?

kumbuka mpira ni mchezo wa kimbinu na wa kimakosa.

ninayempiga mimi wewe anakupiga vizuri tu na wakati huo huo wewe unanipiga.

hebu acha mafokeo!
 
Hawa Queens siku moja wapewe match na Yanga kubwa.
Eti timu inaitwa simba Queens! Halafu kocha wake ni wa jinsia ya kiume!!!
Yaani wameshindwa kabisa kutafuta kocha mwenye jinsia ya kike kama yule wa Yanga!!
Imagine alifanikiwa kuiongoza timu yake kuifunga hiyo simba Queens kwenye mechi ya mwisho kukutana kwenye ligi!!

Hata hivyo nawapongeza kwa kuwa Mabingwa wapya wa CECAFA. Maana wanajitahidi kuwafuta machozi kaka zao, ambao msimu mzima wanaishia kuambulia like kombe pekee la bonanza (Kombe la Mapinduzi).
 
Yanga mkiacha kuroga mtaanza kuona mafanikio ya kweli. Hivi hivi mtaishia kujisifu kuifunga Simba tu tena kwa ndumba.
 
Eti timu inaitwa simba Queens! Halafu kocha wake ni wa jinsia ya kiume!!!
Yaani wameshindwa kabisa kutafuta kocha mwenye jinsia ya kike kama yule wa Yanga!!
Imagine alifanikiwa kuiongoza timu yake kuifunga hiyo simba Queens kwenye mechi ya mwisho kukutana kwenye ligi!!

Hata hivyo nawapongeza kwa kuwa Mabingwa wapya wa CECAFA. Maana wanajitahidi kuwafuta machozi kaka zao, ambao msimu mzima wanaishia kuambulia like kombe pekee la bonanza (Kombe la Mapinduzi).
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] utalia sanaa huu mwaka, na badooooo.

Ndo kwanza maumivu yameanza. Poleeeeeeeh
 
Unamfahamu Edna Lema wewe! a.k.a Mourhino? Kama humfahamu basi subiri Ligi ya wanawake ianze
 
Back
Top Bottom