Simba robo fainali CAF kukutana na CR Belouizdad, Kaizer Chiefs au MC Alger

Simba robo fainali CAF kukutana na CR Belouizdad, Kaizer Chiefs au MC Alger

Sasa ni rasmi mpinzani wa Simba katika robo fainali ya CAF Champions League ni lazima awe mmoja kati ya timu hizi tatu; CR Belouizdad ya Algeria, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini au MC Alger ya Algeria pia.

Hii ni baada ya mechi za makundi yote manne kumalizika leo na timu hizo kushika nafasi za pili sambamba na Al Ahly ya Misri ambayo hata hivyo haiwezi kukutanishwa na Simba kwa kuwa zinatoka katika kudi moja. Droo ya kumpata mpinzani mahususi itafanyika tarehe 30/04/2021. Misimamo ipo hivi:

View attachment 1748882
Wana pointi 9 tu wajiandae sana kupambana na mwenye pointi 13...
Kwenye ligi zao sasa
Cr belouizdad anashika nafasi ya 10
Kaizer chiefs anashika nafasi ya 9
Mc Algers anashika nafasi ya 11
 
Hongereni simb.. ndani ya misimu mitatu inayofatana mmefika robo fainali mara mbili... esperence ndani ya misimu mitatu hiyo hiyo mliyofika robo ametwaa ubingwa mara 2.. na timu ni ile ile haijabadilika.. why kwenye prediction mtu akiwapa nafasi ya kuwa mabingwa tena wewe unakasirika... kwenye comment ile sijaiponda timu yeyote.. nimeweka prediction yangu. Ila wewe unakasirika huku kuna timu 7 sijazipa nafasi ya ubingwa.. why wewe mmoja ujistukie
msimu uliopita bingwa al ahly uliopita tena bingwa mamelodi

sijui utopolo habari zenu mnaokota wa pi ?
 
msimu uliopita bingwa al ahly uliopita tena bingwa mamelodi

sijui utopolo habari zenu mnaokota wa pi ?

mwaka 2018 bingwa wa caf champions league ni Esperence, mwaka 2019 bingwa wa caf champions league ni esperence tena, mwaka 2020 bingwa wa caf champions league ni al ahly, mwaka 2021 ndio huu timu zipo hatua ya robo..

mamelodi ni mtoto mdogo sana kwa Esperence, kwanza mamelodi amewahi kutwaa ubingwa wa caf champions league mara 1 tu tangu klabu imeanzishwa, ambao ni mwaka 2016 tu ndio mamelodi alibeba kombe, sasa why udanganye ni bingwa wa mwaka juzi..

Mamelodi unaedanganya ni bingwa wa msimu uliopita, labda alitwaa ubingwa wa rede mtaani kwenu

Nimekuwekea list ya mabingwa wa kila mwaka uisome ujue nani muongo kati ya mimi na wewe

Screenshot_20210411-104647_Firefox.jpg
 
Wana pointi 9 tu wajiandae sana kupambana na mwenye pointi 13...
Kwenye ligi zao sasa
Cr belouizdad anashika nafasi ya 10
Kaizer chiefs anashika nafasi ya 9
Mc Algers anashika nafasi ya 11
Mkuu Car champions league ni tofauti sana na ligi za ndani ya nchi husika.sidhani kama ni kipimo sahihi,pata mifano ya As Vita na Mazembe.
 
Sijaelewa kwanini Kaizer Chiefs amekuwa nafasi ya Pili na Siyo Horoya mwenye Goal difference nzuri. Maana game zao zote walivyokutana wamesuluhu kama head to head ni sababu
 
Hongereni simba.. ndani ya misimu mitatu inayofatana mmefika robo fainali mara mbili... esperence ndani ya misimu mitatu hiyo hiyo mliyofika robo ametwaa ubingwa mara 2.. na timu ni ile ile haijabadilika.. why kwenye prediction mtu akiwapa nafasi ya kuwa mabingwa tena wewe unakasirika... kwenye comment ile sijaiponda timu yeyote.. nimeweka prediction yangu. Ila wewe unakasirika huku kuna timu 7 sijazipa nafasi ya ubingwa.. why wewe mmoja ujistukie

Umemjibu vizuri sana,,, Esperance na simba wapi na wapi ni mbingu na ardhi.
 
Bora MC Alger,Kaizer Chief wanaupiga mwingi na kule mbele wapo vizuri.

Kaizer chief anabahati sana 😀 draw ya jana imemsaidia abakie,,,mchezaji wa zamalek kanickitisha mno jana baada ya game kuisha kwa ushindi wa goli 4-1 nilihisi kauliza jambo kama sio matokeo ya Esperance na MC algier , aise mshkaji nilimuona katikisa kichwa walijua tayali washapita.
 
Sasa ni rasmi mpinzani wa Simba katika robo fainali ya CAF Champions League ni lazima awe mmoja kati ya timu hizi tatu; CR Belouizdad ya Algeria, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini au MC Alger ya Algeria pia.

Hii ni baada ya mechi za makundi yote manne kumalizika leo na timu hizo kushika nafasi za pili sambamba na Al Ahly ya Misri ambayo hata hivyo haiwezi kukutanishwa na Simba kwa kuwa zinatoka katika kudi moja. Droo ya kumpata mpinzani mahususi itafanyika tarehe 30/04/2021. Misimamo ipo hivi:

View attachment 1748882

Mkuu Lupweko , salam kwako. Hivi timu iliyoingia robs fsinali ni Kazer chief au Horoya ?

Kibonde hapo ni kaizer chiefs
Kwa uchezaji wa Kaizer chiefs nisingependa tukutane nao kabisa, wings zao zinasumbua sana watatufanya tusishambulie kupitia pembeni.

Mc Algier tumeshacheza nae tukamfunga hadi huko huko kwao Algeria hivyo siyo threat sana kwetu na pamoja na uchezaji wao wanashambulia sana kupitia katikati hivyo kwetu itakuwa advantage kwa sababu tuna defensive midfield nzuri.

CR Belouzdad hawa threat pekee ni Mshambuliaji wao Gasmi nafikri, wanacheza taratibu sana na wanakabia juu sana hivyo kwetu itakuwa uchochoro kwa kina Luis Chama na wengineo.

Mc Algier na CR ndiyo mara yao ya kwanza kuingia quater final hivyo itakuwa vizuri kukutana na mgeni zaidi kuliko timu nyingine yoyote.
 
Kwa upande wangu ningetamani Simba apewe kaizer chiefs, hawa jamaa uwezo wao ni kawaida compared na team zingine zilizovuka stage ya makundi, Kwanza hawana uzoefu kulinganisha na team zingine lakini pia hawana wachezaji hatari kama team zingine, japokuwa walipata ushindi dhidi ya Waydad ila hiyo haiondoi maana ya kwamba wao ndo kila mtu anawatamani

Hatua inayofata hao jamaa wa ngozi nyeupe (warabu) ukitoa mamelodi, warabu ni hatari Sana, wanaijua vizuri sana hii michuano lakini pia Wana mbinu nyingi Sana za kushinda hizi mechi kubwa, Ila Kwa kaizer chief yule Simba anammudu vizuri tu, kuanzia Hali za hewa kwao na bongo, mida ya game za kwao na kwetu almost the same, Simba at least anatakiwa kukutana na mwarabu nusu fainali ila akikutana nae robo kibarua kinaenda kuwa kigumu
CR Belouzdad ameingia quarterfinal kwa mara ya kwanza hivyo ni timu underdog.
Kikubwa ni kuwa hawakuwa na matokeo mazuri hata kwenye uwanja wao wa nyumbani.
 
Kwa uchezaji wa Kaizer chiefs nisingependa tukutane nao kabisa, wings zao zinasumbua sana watatufanya tusishambulie kupitia pembeni.

Mc Algier tumeshacheza nae tukamfunga hadi huko huko kwao Algeria hivyo siyo threat sana kwetu na pamoja na uchezaji wao wanashambulia sana kupitia katikati hivyo kwetu itakuwa advantage kwa sababu tuna defensive midfield nzuri.

CR Belouzdad hawa threat pekee ni Mshambuliaji wao Gasmi nafikri, wanacheza taratibu sana na wanakabia juu sana hivyo kwetu itakuwa uchochoro kwa kina Luis Chama na wengineo.

Mc Algier na CR ndiyo mara yao ya kwanza kuingia quater final hivyo itakuwa vizuri kukutana na mgeni zaidi kuliko timu nyingine yoyote.
Salem mkuu,

Back
Top Bottom