Simba S.C. kwenda Angola siku moja kabla ya mechi ni takwa la kiufundi au bajeti imekata?

Simba S.C. kwenda Angola siku moja kabla ya mechi ni takwa la kiufundi au bajeti imekata?

Comment nyingi zinaonesha jinsi Tanzania ilivyo na wajinga wengi. Majibu yote ni ya kijingajinga tu. Pyramid walishawahi kuja kucheza na yanga Mwanza siku moja ya baada ya mechi wakapanda ndege wakasepa! Nchi nyingi sana zilizoendelea zikishagundua nchi haieleweki, huwa wanaenda siku moja kabla ya mechi. Red Arrows walienda Angola tarehe 16 August wakacheza mechi tarehe 18. Hizi mechi zinaenda kimkakati, sio kama hizo mechi zenu za bahasha!
hahahahaha,tz ina wajinga kweli

ni ndio mbinu za kimkakati ktk soka ,hii mbinu inatumika sana

Sie tuliowahi kushiriki hz hatushangai.huwa inapunguza hujuma kwa timu
 
Na kama ni takwa la kiufundi mwambieni huyo aliyeamua hivi kuwa hii ni hatari na itatugharimu kimatokeo.

Ningewaelewa Simba S.C. (hasa kiufundi) kama wangeenda Angola siku tatu kabla ila hii ya kwenda siku moja kabla ya mechi (yaani Jumamosi na kucheza Jumapili) ni hatari kimchezo (kimaandalizi), na hapa wala GENTAMYCINE nisimung'unye maneno kuwa tumefanya kosa kubwa sana.

Hivi kweli ndani ya siku moja huko Angola wachezaji wa Simba S.C. watazoea hali ya hewa, mazingira kiujumla na kuzoea uwanja ili kuweza kujiandaa vyema kisaikolojia kwa mchezo husika wa siku ya Jumapili? Hii ni kujiua kiufundi kwa Simba S.C. na tutake tusitake ni lazima itatugharimu katika utendaji wetu uwanjani siku ya mtanange (mechi).

Nilikuwa mbishi kuamini kuwa sasa Simba S.C. kuna ukata (bajeti hafifu) na pia mwekezaji Mo Dewji ni kama vile amesusa na kajiweka kando, ila kwa hili la kwenda nchini Angola Jumamosi na mechi Jumapili naamini rasmi kuwa mzigo ndani ya Simba S.C. umekata na wala tusitake kudanganyana juu ya hili.

Ukiwa umecheza mpira, ni mtu wa mpira au ni mdau (mchambuzi na mwaimu) wa mpira utanielewa vyema GENTAMYCINE kwa hiki nilichokiandika hapa, ila ukiwa ni "Ngala ngala' kamwe hutonielewa na utabaki kunishangaa tu.

Kazi ipo tu Jumapili kwa Waangola!
Munachezea "Libolo" tu kama 2013.
 
Uto 🐸 naona mnatafuta pa kuhemea 💨, msijisahaulishe Al Hilal wamekuja na mabomu 💥 mkae kwa passwords
🤣🤣🤣
 
.
2.Kutopata Muda wa kutosha kutatua figisu mfano Vipimo vya Covid nk.
Hata ukikaa wiki nzima kabla ya siku ya mechi, matokeo ya Covid19 yanatolewa masaa machache kabla ya kick-off.
 
Huna hela utaenda kwa ndege ya kukodi? Unaijua gharama ya kukodi ndege? Au Unadhani hiyo gharama ni ndogo kuliko wangekaa huko siku tatu? Akili tu inahitajika kutambua mambo!
 
Alafu wengi si sijui wanaishi kwa mazoea? Team za Ulaya huwa zinaenda a day before mechi katika Uefa Champions league hakuna muda wa kwenda ugenini kukaa siku 5 sjui.

Walishawahi kuja Pyramids na ndege yao hapa siku moja kabla na Wakaikun'guta Yanga kule Mwanza vzr tu! Pia Al Alhy hvy hvy.
Huna hela na unaenda kwa ndege ya kukodi?
Uwahi kuzoea uwanja gani na uwanjani utaruhusiwa siku moja before game?

Hali ya hewa ipi unaenda kuzoea, ikiwa dar ni 30° na Angola ni 26 to 28 ? Kuna tofauti inayohitaji adoptation hapo?

Msimu huu ni cool kwao,
Check ur facts popoma.
 
Tutatumia njia hii kama tulivyofanya South Africa

images.jpeg
 
Hii ya siku Moja Kabla ya mchezo nimeipenda Sana. Hongera uongozi kwa kuliona hilo. Huwezi kwenda kujikabidhi mikononi mwa adui kwa siku 3 au 4 halafu ubaki salama.

Fuatilia mechi ambazo simba ameenda siku Moja au mbili Kabla ya mechi na zile ambazo ameenda siku 3 au 4 Kabla ya mechi ili kuzoea Hali ya hewa ni zipi amepigwa magoli mengi.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Mbona PSG walienda Ureno Jumanne na Jumatano wakacheza? Na ndio wanamapesa chungu nzima.
 
Back
Top Bottom