SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Simba walikuwa na mapungufu muhimu ya kiufundi ambayo kwa hatua wanayotaka kupiga hasa huko CAF ilihitaji kuyarekebisha.
Pungufu la kwanza lilikuwa ukosefu wa ubunifu katika kupenyeza mipira katika ngome ya timu pinzani. Hii ilisababisha timu kulazimika mara kwa mara kurudisha mipira nyuma, mara nyingi hadi kwa kipa. Mashabiki wengi hawakuwa wanaliona hili au walikuwa wanalimezea, wao walikuwa wanaona tu boli linatembea ila haya yalikuwa madhaifu.
Pungufu la pili ilikuwa kwenye ukabaji na kujituma. Simba alikuwa anacheza mpira wa taratibu sana na morali ya wachezaji ilikuwa chini. Ndiyo kuna game goli zilikuwa zinakuja wakati mwingine nyingi tu halafu mashabiki wanasahau ila zile mechi ambazo game ilikuwa inakataa tuliona wazi hayo mapungufu na watu waliyalalamikia. Ila angalia game hizi mbili za mwisho, wachezaji unaona wanapambana sana. Morali ya timu iko juu.
Simba ya Robertinho haichezi mpira wa Brazil, Spain wala wa Dubai. Huu ni mpira wa English Premiere League. Nashangaa watu wanaangalia kila siku EPL, wengine wanabeti, wengine wamekuwa mashabiki lia lia wa Arsenal, Man U, Man C, nk. ila wanashindwa kutambua mpira wa Uingereza unaochezwa sasa na Simba ambao ni mpira wa kasi na ni kawaida kucheza mipira mirefu. Tofauti kule wachezaji wana control nzuri ya mpira ambayo Simba kiasi wana mapungufu hasa wakitaka kumaintain kasi ya mchezo.
Wachezaji hasa mabeki wanahitaji kutulia maana naona wanacheza kwa pressure sana na pia timu nzima iongeze uwezo wa kucontrol mpira vizuri hata kama ni kwa kucheza mpira wa kasi. Pia safu ya mbele inabidi kuwa inatumia vizuri nafasi inazopata.
NB. Binafsi siyo mpenzi sana wa style inayotumika EPL.