Makolo ni watu wa ajabu sana! Ina maana ni jambo jipya kwenu kusikia timu ikitamba kwamba itashinda, au?! Au ni kweli nanyi mlikuwa mnaipa nafasi kubwa Yanga kwa sababu bado mnakumbuka 1-0 ya Ngao ya Jamii huku timu yenu ikionesha wazi bado tia maji tia maji?
Ukweli mchungu ni kwamba, kauli zenu zilizotawala hapa baada ya mechi ni kauli za ki-underdog ambazo hata Yanga tumezitumia sana wakati tulipokuwa tunaingia uwanjani na kuwapa nafasi kubwa Makolo kushinda lakini mwisho wa siku, mechi inaisha sare na hapo kauli zetu zikaw hizo hizo "...si mlikuwa mnasema mtashinda, tena kwa goli nyingi"! Enzi zile mngetoka mmenuna lakini leo "...mbona mmeshindwa! Mliaminishwa ujinga" na bla bla nyingin za ki-underdogo kibao!