Simba SC 4-1 Ruvu Shooting | NBC Premier League | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Simba SC 4-1 Ruvu Shooting | NBC Premier League | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Huyu adimin anambwembwe sana, endelea kutuhabarisha anasema nn
Sawa nitakuwa nawaletea burudani
😅😅👇👇

IMG_20220508_195022.jpg
 
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara NBC Premier League kupigwa leo Mei 8, 2022 ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC anamkaribisha Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Takwimu na kila kizuri kinaegemea zaidi upande wa Simba SC kwenye mchezo huu lakini kiuhalisia chochote kinaweza kutokea This is Football.

Ni Vita vya Kocha Pablo Franco kwa System ya 4-2-3-1 na Charles Mkwasa dhidi ya System ya 4-3-3 ni Vita vya kwanza kwenye Flanks kisha kulishinda eneo la Kiungo, unategemea kuwaona Simba SC wakitawala eneo la Kiungo, unategemea kuwaona Ruvu Shooting wakisubiri matendo ya pili (Turn Over)

Ruvu Shooting amezuia vizuri kwenye mechi zao tano za mwisho wamepata cleansheet mbili na mechi nyingine mbili kati ya hizo hawajaruhusu zaidi ya goli moja, ni mchezo mmoja tu waliruhusu goli moja, ambapo ni takwimu nzuri kwa daraja ambalo Ruvu Shooting walipo.

Ni mechi ambayo Simba SC anaitaka ili kurejesha Confidence kwani hawajapata ushindi katika mechi tatu za mwisho kwenye Ligi zote ametoa sare, tutegemee kuwaona Simba muda mwingi wakiingia katika zone ya Ruvu Shooting ili kuifungua safu yao ya ulinzi.

Je ni kipi Ruvu Shooting watakifanya dhidi ya Quality ya mpinzani na kucheza dhidi ya presha ya Simba kwa dakika zote tishini, umakini katika kuzuia, ni ngumu kucheza bila ya kufanya kosa hata moja, ni suala la muda kutupa majibu sahihi ndani ya dakika 90.

Kocha msaidizi wa Simba SC Suleiman Matola, amesema kiufundi mechi haitakuwa rahisi, mechi itakuwa ngumu, lakini wamejiandaa kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi.

Naye Kocha msaidizi wa Ruvu Shooting Rajabu Mohamed, amesema kuwa Mechi itakuwa ngumu dhidi ya Timu Kubwa, Kongwe, lakini wamejipanga kujaribu kushinda mchezo huo.

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku.. Usikose Ukaambiwa

Kulipewa Mwana..Kulitaka Mwana

..... Ghazwat....


Naaam mpira umeanza uwanja wa Mkapa

Ni Vita vya dakika 90 za jasho na damu

Simba SC 0-0 Ruvu Shooting

02' Simba wanapata Free Kick, inapigwa kulee lakini golikipa Makaka anasafiri na kupangua mpira ule na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

07' Ruvu wapo nyuma mapema tu, Nadhani wanasoma mchezo kuona gani watapenya ngome ya Simba

12' Jaribio kwa Simba kupitia kwa Sakho na Kagere linashindwa kuzaa bao, huku Chanongo akijibu mapigo upande wa Ruvu Shooting

15' Abrahaman Mussa yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kupata rabsha

20' Pamoja kumiliki mpira eneo la kati lakini, bado mambo ni magumu upande wa Simba

23' Mkude yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kuumia, huku Abdulswamadu akionyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya.

24' Kona kuelekea Ruvu, inapigwa kulee Wooooooo, Wawa anapiga shutii lakini linatoka nje ya lango

Ametoka Mkude na nafasi yake anaingia Bwalya upande wa Simba SC | Simba SC 0-0 Ruvu Shooting

30' Henock anamvisha kanzu maridadi mchezaji wa Ruvu, huku Gadiel akikosa nafasi ya kutengeneza bao.

Oyaaa, Peter Banda anashindwa kuweka mpira kambani baada ya jitihada zake kuzimwa na golikipa Makaka

35' Ruvu wanakosa nafasi nzuri ya kupiga shuti lango la Simba, Wawa na Henock wapo nyuma kwa ulinzi mkali.

39' Almanusura Simba SC wapate bao, Shuti kali la Kagere linambabatiza beki wa Ruvu

40' Kibu Goooooooooooooaaal gooal

Kibu Denis anaipatia Simba SC bao kwa kwanza baada ya kutokea piga nikupige lango la Ruvu Shooting

Simba SC 1-0 Ruvu Shooting

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko

Kwake Banda, anapiga Krosi kwake Sakhooo, anakosaaaaaa

Haya kwao Ruvu wanakwenda mbele kuleee, lakini wanakosa vile vile, wanao Simba sasa kuleee Bandaaa looo, Mobby anafanya Kazi nzuri kuokoa hatari ile..!

Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wapo mbele ya bao moja kwa bila dhidi ya Ruvu.

HT: Simba SC 1-0 Ruvu Shooting
Simba itaachaje kushinda wakati leo ni siku yao ya KINA MAMA DUNIANI

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app 
 
Game hii ilikua imebalance vizuri shida hapo kati kuna Ellysasii....anaonyesha wazi kabisa ameegemea upanda mmoja
Mchezaji wa ruvu amefanyiwa faul akienda kufunga si.ba wmechukua mpira kanyamaza tu..
 
67' Bwalya Goooooooooooooaaal gooal

Bwalya anaipatia Simba SC bao la pili akipokea pasi murua kutoka kwa Sakho

Simba SC 2-0 Ruvu Shooting
 
John Bocco.

Tukibaki Naye Hana Faida, Tukiuza Hana Faida. Kwanini Hana Faida?

Ni mchezaji Wa Ndani, Hivyo Tukiuza Namba Yake itakuwa Replaced Na mchezaji Wa Ndani… Je Kuna Striker Mzawa Wa Kumfikia John Bocco? Hayupo Hivyo Tuuze Tusiuze Mambo Ni Yale Yale.

Lakini Kiukweli John Bocco Kachoka. Tuzoee Tuu wana Simba. Huenda Msimu ujao Akawa Vizuri
 
81' Bocco Goooooooooooooaaal gooal

John Bocco anaipatia Simba SC bao la tatu akipokea pasi murua kutoka kwa Mhilu

Simba SC 3-0 Ruvu Shooting
 
Mkubwa mkubwa tu..what a goal captain fantastic..Boccooo
 
John Bocco.

Tukibaki Naye Hana Faida, Tukiuza Hana Faida. Kwanini Hana Faida?

Ni mchezaji Wa Ndani, Hivyo Tukiuza Namba Yake itakuwa Replaced Na mchezaji Wa Ndani… Je Kuna Striker Mzawa Wa Kumfikia John Bocco? Hayupo Hivyo Tuuze Tusiuze Mambo Ni Yale Yale.

Lakini Kiukweli John Bocco Kachoka. Tuzoee Tuu wana Simba. Huenda Msimu ujao Akawa Vizuri
Ramli chonganishi hizi
 
Back
Top Bottom