Simba SC kwanini haijasajili Mshambuliaji mpaka sasa?

Simba SC kwanini haijasajili Mshambuliaji mpaka sasa?

lwambof07

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2016
Posts
4,643
Reaction score
5,335
Aisee hili ni sikio la kufa. Toka wakati wa dirisha kubwa tuliwakumbusha hapa kuwa Simba haina mshambuliaj namba tisa. Juzi tena kwenye dirisha dogo tumewakumbusha hapa tena kwa kluwaambia kabisa kuwa wafanye maamuzi magumu waachane na mshambuliaji mmoja wa kimataifa walete mwingine aliyekamilika bado hawakusikia.

Badala yake waklete viungo wakawa wanafanyia majaribio kwenye Mapinduzi wakati Simba ndio timu tajiri kwa viungo. Kwa mwendo huu hata ubingwa ni hatihati.
 
Kwa hiyo hata mchango wa mshambuliaji hatari kwa sasa pale msimbazi huutambui! Yaani Profesa Sakho! Bado kuna wakili msomi BM3, mshambuliaji katili Kagere, kiungo hatari aliyeko Afcon Banda, nk!
 
Nadhani pale ndani ya simba, kuna kuoneana haya, yaani hawawezi kumwambia Mgalu mchango wako unatosha sasa ondoka, au wamwambie Boko, inatosha sasa kaa Pembeni. Na hii itaigharimu timu hii msimu huu
 
Katika kitu ambacho sijaelewa hadi sasa hivi SSC inampango gani pale mbele Ina maana wameridhika na kina Bocco,Mugalu,Kagere na Muhilu??

Mimi nilitegemea mpaka sasa imesasajili mfungaji wa kimataifa pale mbele anayeendana na hadhi ya club.

Watasajili lini mshambukiaji hawa jamaa[emoji848][emoji848]
Rekebisha kichwa cha habari basi.
 
Aisee hili ni sikio la kufa. Toka wakati wa dirisha kubwa tuliwakumbusha hapa kuwa Simba haina mshambuliaj namba tisa. Juzi tena kwenye dirisha dogo tumewakumbusha hapa tena...
dah yaan sijui wanafikiria nini hawa jamaa
 
Nadhani pale ndani ya simba, kuna kuoneana haya, yaani hawawezi kumwambia Mgalu mchango wako unatosha sasa ondoka, au wamwambie Boko, inatosha sasa kaa Pembeni. Na hii itaigharimu timu hii msimu huu
kama ndiyo hivyo basi kazi ipo
 
Weakness point ya Simba...inawezekana wana share mshahara na wanaofanya maamuzi..Mugalu,Bocco,Kagere watoke wote apatikane striker mmoja
kabisa tena wakitoka wote hao inabid wawe wawili visu vikali pale mbele
 
Tatizo bado ni Chemistry 😊😊😊
 
Tatizo linaanzia pale tunaposubiri na kuamini Sana ripoti ya kocha wakati mapungufu mengine yako wazi ,hata shabiki asiyejua mpira anaona kabisa kwamba hapa pana mapungufu
 
Katika kitu ambacho sijaelewa hadi sasa hivi SSC inampango gani pale mbele Ina maana wameridhika na kina Bocco,Mugalu,Kagere na Muhilu??

Mimi nilitegemea mpaka sasa imesasajili mfungaji wa kimataifa pale mbele anayeendana na hadhi ya club.

Watasajili lini mshambukiaji hawa jamaa[emoji848][emoji848]
kagere bocco,mugalu ,muhilu,kibu, bado untk mshambuliaji mwngine?
 
Back
Top Bottom