Simba sc mpaka sasa ina vikombe vitatu ndani ya kabati, hakika hii ni timu ya mfano na timu ya kuigwa katika ligi ya Nbcpl

Simba sc mpaka sasa ina vikombe vitatu ndani ya kabati, hakika hii ni timu ya mfano na timu ya kuigwa katika ligi ya Nbcpl

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Ukitoa mafanikio ya kufungua wasap channels, Manzoki kuja kwenye uchaguzi, KIbu denis kuikanda Yanga Sc mara mbili mfululizo pamoja na kuishia Robo klabu bingwa Afica kama ilivyozoeleka Simba sc wametwaa kombe linguine la Muungano kwa kuichapa Azam Fc goli moja kwa nunge goli lilio fungwa na kiungo mkabaji kutoka mataifa ya juu Babacasar.

Hivi sasa Simba Sc ina makombe matatu ndani ya kabati Kombe la MASHABIKI kutoka kwenye michuano ya AFL, kombe la NGAO YA JAMII na MUUNGANO, kiufupi Simba sc imebeba TREBLE
Hii ni timu ya kuigwa na timu ya mfano katika ligi yetu hiii ya NBCPL , na bado ina ndonto za kufukuzia ubingwa wa ligi za ndani.

MAONI YANGU ; uwekezaji bora katika timu,uongozi bora na utekerezaji thabiti ndiyo ngao kubwa iliyowafanya simba sc kupata TREBLE hakika timu zinapaswa kuiga mfumo huu kutoka katika timu ya simba sc
 
Mbona midomo mtalala wazi na vidole vitaota sugu kwa kutype??? Maana si kwa kasi hii kila dkk uzi....
 
wewe acha tu aisee tunwaonea wivu mnoo tena mo dewj asiondoke aendeee kubaki kwa kweli jamaaa angu
Huo ndo ukweli wivu husda roho mbaya na mitima nyongo itawaua...sisi hizo za Mo sio shida zetu naona nyie ndo anawakera...
 
Kumbe mlikua mnalitaka? Mkiamini mnyama hatalichukua? Kalichukua limekua baya..kabla ya hapo mkasema Azam atatupiga…
imewafariji sana mashabiki nasikia lina thamani ya milioni 900 hakika simba wamelamba dume
 
Huo ndo ukweli wivu husda roho mbaya na mitima nyongo itawaua...sisi hizo za Mo sio shida zetu naona nyie ndo anawakera…
ila umeandika kwa hisia sana hahhahhaahahahahhah
 
imewafariji sana mashabiki nasikia lina thamani ya milioni 900 hakika simba wamelamba dume
Hata lingekua na thamani ya laki...as long as ni official....hayo mengine ni nyie endeleeni kutafuta faraja kwa kuwa mmepigwa na kitu kizito...
 
Back
Top Bottom