Simba SC 'tumezubaa' sana, 'tunakomolewa' huku Yanga SC ikitumia mwanya huu 'Kujiimarisha' 'zaidi 'Kimkakati' ili kuwa 'Mabingwa wa NBC Premier League

Simba SC 'tumezubaa' sana, 'tunakomolewa' huku Yanga SC ikitumia mwanya huu 'Kujiimarisha' 'zaidi 'Kimkakati' ili kuwa 'Mabingwa wa NBC Premier League

Acha kulalama, timu yako mbovu tu. Ulishindwaje pale kwa Mbeya City wakiwa pungufu zaidi ya 50 minutes. Utajua hujui.
kuwa na adabu we chura, simba sio team mbovu, bali ni team nzuri inayohitaji marekebisho kidogo ili iwe bora.
 
duh ,najuaga godfrey ni simba damu.kumbe sio?
basi wampe jukumu KD
Mkuu unaamini maneno ya huyu msema ovyo? Aliwahi kusema Kwa kujiamini kabisa kwamba eti Dk Tulia alisoma nje ya nchi kuanzia chekechea Hadi chuo kikuu...

Haya maneno anayo post haoa Ni maneno ambayo ameyasikia kwenye kijiwe cha mshona viatu kilichopo kwao Bunda mjini mkoani Mara karibu na shule anayo fundishia..

Screenshot_20220120-163245.png


Screenshot_20220120-163236.png


Screenshot_20220120-163149.png
 
Hata mm Hilo nimeliona kitendo Cha mwanadad Yule barbarita kuvimba na viongozi wa tpl na tff niliona adhari zake kwa simba indirectly nikiwawambia washabik wa simba wakaniona Kama nachanganyikiwa kwa vile niliwambia ukweli kuwa mpira na siasa za nchi hi Ni za kukomoana tu .mm Ni yanga damu damu nanufaika San na mgogoro wa simba na body ya ligi na ninaomba usiishe had mwandada Yule barbarita kuomba POooo na wakubali mashri za tff na tpbl
 
Kwa masikitiko makubwa Asubuhi ya leo nilianzisha Uzi hapa JamiiForums nikisema kuwa Kitengo cha Umafia Simba SC Kinepwaya na kwamba nipewe Mimi na Wenzangu Sita (6) na Yanga SC hatokuwa Bingwa kwa Mshangao huo Uzi siuoni (kwa Lugha sahihi ni kama vile Umefutwa) kwasababu wazijuazo Walioufuta.

Ni kwamba kwa sasa naona Mapungufu makubwa ya Kimkakati (Kimafia) ndani ya Klabu yangu ya Simba kiasi kwamba Yanga SC wameshaanza kuyatumia Kujinufaisha nayo na wanaelekea Kufanikiwa.

Kitengo cha Umafia ( Mikakati ) cha Simba SC kingekuwa imara kamwe Mchezo wetu na Mtibwa Sugar FC usingepelekwa Manungu ila kutokana na Kuzubaa Kwetu, Kujisahau na Kuridhika TFF (hasa Bodi ya Ligi) kwa Kushirikiana na Yanga SC na Matajiri wao GSM sasa wanatumaliza tu.

Viongozi wa Simba SC waliomba Mechi isichezwe Manungu wamekataliwa kwa Kigezo kuwa Uwanja ni mzuri ila Yanga SC wameomba Mechi yao isichezwe Uwanja wa Ushirika na ikachezwe Sheikh Amri Abeid Kaluta Arusha wamekubaliwa wakati hali ya Uwanja wa Manungu ni sawa na ya Uwanja wa Ushirika.

Walichokifanya Yanga SC ni kupitia kwa Mtu ( Shabiki ) wao mkubwa IGP Sirro ili Kumshawishi ahakikishe Mevhi haichezwi Ushirika na kwa Kuzuga ( Kutuzuga ) Jeshi la la Polisi wakaja na Taarifa ya Utetezi kuwa Mchezo huo umehamishwa Ushirika kwakuwa Uwanja utatumika kwa Shughuli za Kijeshi wakati si kweli ila ni Mpango Maalum wa kuitengenezea Yanga SC Mazingira ya Ushindi.

Viongozi wa Simba SC wasichokijua ni kwamba baada ya Kutunishiana Misuli kwa CEO Barbara Gonzalez na Mwenyekiti wa Simba SC ( Wanachama ) Murtaza Mangungu na TFF pamoja na Bodi ya Ligi ( TPLB ) wametengeneza Bifu Kubwa ambapo Yanga SC na GSM yao wameamua Kutumia mwanya huu ( huo ) kwa Kuwahonga baadhi ya Viongozi wa TFF na TPLB ili waikomoe Simba SC ili iangushe ( ipoteze ) Alama ( points ) na Yanga SC aweze Kutuacha kwa mbali sana na ikiwezekana atangaze Ubingwa mapema mno na kwa GENTAMYCINE ninavyoona na Kuyasikia naliona hili Kufanikiwa.

UMAFIA ninaoumaanisha hapa unahusu Mambo Makuu matatu ambayo ni...

1. Rushwa
2. Uchawi
3. Propaganda

Najua kwa Wageni wa Soka la Bongo hapa mtanishangaa GENTAMYCINE, ila kwa wale Watu wa Mpira naamini wamenielewa na wala hapa tusifichane Klabu za Simba na Yanga Mafanikio yao ya Uwanjani Kitakwimu ni kama ifuatavyo.....

1. Rushwa....45%
2. Uchawi...40%
3. Propaganda....10%
4. Uchezaji...5%

Simba SC mpaka tuje Kushtuka kuwa tunahujumiwa na TFF na TPLB huku Yanga SC na GSM yao wakiutumia mwanya huu ( huo ) Kujinufaisha Kiushindi tayari Yanga SC watakuwa Mabingwa wa NBC Premier League Msimu wa 2021 / 2022.

Simba SC tuendeleeni tu Kuzubaa sawa?
Mhindi wenu wa kuwapa fedha kajisogeza pembeni na hamna ujanja wa kupata pesa sehemu nyingine
 
Sasa simba walipenya vipi kimataifa, nako walikua wanahonga na uchawi??

Hayo kibongo bongo yapo ila ukiwa na kikosi kibovu lazma uumie tu.
Hiyo 5% ni uongo mtupu, mbona tunaona jinsi hizi timu 2 zikiwa form zinavyotandaza soka safi au ni kiini macho kile.??
 
Umafia uendane na kikosi imara ,Sasa umafia kwa fowards Kama kina Bocco na Mugalu!!
Embu mutuache kidogo ,huu msimu tukubali tumeshapoteza hakuna Cha umafia Wala Nini.
CEO wetu hawez pambana na Karia japo Karia Ni Simba damu ila atataka tu amuonyeshe kuwa yeye Ni mwanaume hakojoi akiwa amechuchumaa Kama ilivyo kwa Babra.
Kitendo Cha mbungi kupelekwa manungu Ni moja ya mikakati ,ili Babra aweze shinda hii Vita alipaswa aingie sokoni dirisha dogo kutafuta wachezaji wa maana wa kupambana kiume sio Kama hao mdebedo akina bocco na mugalu .
Mpaka hapa CEO ashapigwa KO hata angefanya umafia gani lakin Hana siraha za maangamiz pale mbele .
GSM Ni mzee wa Msoga huyo Galib sijui injinia Ni chawa tu so Babra Ni mtoto mdogo Sana Kama Msoga akiamua akufanyie fitna na inaonekana kweli Hilo lipo Msoga kakataa hii dharau ya kuzidi akili na Simba miaka minne mfululizo kaingia Kati mwenyew ,nan wa kuruka ? Awe Karia akikarishwa chini atatii tu maelekezo na kibaya Zaid CEO kamtibua basi anachanganya na hasira Mambo yakua km yalivyo.

Ubahil na kuwaonea aibu wachezaji waliochoka ndicho kinaenda kuimaliza Simba huu msimu ,na tusifichane naziona game Kama tatu au nne huko mbelen Simba atapoteza pia .
 
Back
Top Bottom