Simba Sc tuna mengi ya kujifunza kutoka Yanga

Simba Sc tuna mengi ya kujifunza kutoka Yanga

Hakika aliyewaita utopolo alitafakari mbali sana
Kwanza nikiri kwamba nitazungumza bila unafiki na kwa nia ya dhati kabisa naomba nitoe mtazamo wangu kwamba tukiwa kama moja ya klabu inayokuja kwa kasi nadhani wanasimba tuna mengi ya kujifuñza kutoka kwa watani zetu Young Africans wanaofanya vizuri nyumbani na kimataifa.

1.Mpira ni uwekezaji
Wenzetu wamewekeza vyema kwa kununua wachezaji mahiri na kocha makini na ndiyo sababu wanafanya vyema katika michuano ya nje na ndani.

2.Mpira si uchawi
Hua nakereka sana kuona katika karne hii ya 21 bado tunaamini katika ushirikina jambo linalotuangusha sana na kuwafanya wenzetu wawe bora zaidi yetu, Kwani mpira umebadilika!

3.Tujikite katika kutafuta vikombe na mataji sio sifa
Kila siku klabu yetu ni kelele tupu mitandaoni na kupeana vichwa lakini ukiuliza tuna makombe/mataji mangapi? Hakuna! Taji ni kuifunga Yanga/Wydad [emoji1] hii ni aibu, tofauti na Yanga wanaopambana kwa malengo ya kutwaa ubingwa

4.Yanga anaongoza kwa kila kitu dhidi yetu, Amechukua ubingwa Ligi kuu mara nyingi zaidi yetu, Bado anaongoza ligi,Ameongoza kundi lake CAF,amechukua vikombe vyote vya ndani wakati huo tukipongezana kuwafunga watanì [emoji1]

5. Nitarudi kuendelea..........

Guvu moya
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hakika ujinga wa uzeen lazma utakufa nao tu pole sana
Naunga mkono hoja, Chama yupo slow sana kufanya maamuzi, tofauti na mtu kama Bakari Nondo.Baleke ndiyo kabisa bila mipira ya kubahatisha hakuna kitu, huwezi mlinganisha na mtu kama Moloko pale Yanga, kuanzia kimbinu kiuchezaji morali yaani kiufupi Sioni Simba tukishinda huko ugenini tungeweza tungemuazima hata Mayele lakini ndiyo hivyo tena, Haiwezekani.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Bila shaka umetumia mechi za yanda dhidi ya rivers na dhidi ya mazembe kusema simba ana la kujifunza kwa ynaga; ni vema kwa kuwa umeliona hilo lakini jiulize yafuatayo

1. Yanga kaongoza kundi akiwa na monastir aliyetolewa na ahly CAFCL, alikuwa na mazembe aliyetolewa na vipers CAFCL, na alikuwa na bamako mgeni wa makundi. Sasa angalia mbabe wa mazembe CAFCL kafanywa nin na simba? ukiachana na yangawenyewe aliyetolewa na al hilal CAFCL

2. Robo fainal yanga kashinda ugenin dhidi ya rivers aliyetolewa CAFCL na wydad AC. Hapo ndo unagundua kuwa kwa kigezo cha kuongoza kundi, karibia wote ni loosers wa CAFCL na kwa kigezo cha kushinda ugenini ni kutokana na udhaifu wa timu hizo (kwa sasa)

3. Simba robo fainal alitakiwa akutane na mmoja kati ya Wydad, Mamelod au Esperence, hawa wote wako ndani ya vilabu bora vitano africa na akaangukia kwa wydad ambaye ni wa pil kwa ubora afrika, ulitegemea simba ashinde kama yanga alomfunga rivers aliyeko nafas ya 31?

Yanga amewekeza kwa kias chake na sidhani kama kamzid simba maana hata mashindano wanayoshiriki hawa wawili ni tofauti na ndio maana simba akiishia robo alaf yanga akaishia nusu fainal ndipo watakuwa wamevuna point sawa CAF kwa msimu huu

Kwa taarifa yako, kombe la shirikisho lina ahueni na linatoa fursa ya kusogea mbele zaidi lakini CAFCL kuna hatua ukifika utakwama tu maana akina Wydad, Ahly, Raja na Esperence bado vilabu vingine vya afrika havijafika hatua ya kushindana nao kisoka akiwemo huyoamelod lakin shirikisho yeyote anatoboa ndio maana akina pyramids hawatak CAFCL badala yake wanakomaa na CAFCC ili wapate ubingwa kirahs wakijua kuwa CAFCL ina wenyewe
Mkuu angalia sana afya Yako Simba hii ni mbovu kabisa ila Bado mnalazimisha ukubwa, kuwa makini unaweza kupata magonjwa ya Moyo! Ijumaa Mkishakandwa week (7-0) na Wydad na kutolewa mashindano ya klabu bingwa CAF utapata hisia kuwa Simba ni debe tupu linalovuma sana na wala si timu ya mpira bali genge tu la mashabiki mbumbumbu na viongozi wahuni! Ijumaa mtaumaliza mwendo na Kwa uwazi kabisa mtaona mmevuna mabua msimu huu , uwekezaji mkubwa Mbet umepoteza pesa nyingi bure kwa timu kushindana bila kupata kombe hata la kugombea kuku!! Samahani yakhe nimekumbuka Ami yangu mna Mapinduzi cup ATI !!

Ijumaa hii baada ya Simba kukandwa week (7-0) na Wydad, Msimbazi hapatakalika, Simba mtafukuza makocha, wachezaji, mashabiki, madaktari wa timu, hasira zikizidi mtaenda Lupaso mtango'a viti uwanja mzima na kuomba TFF mletewe mikeka, baadae mtafukuza hadi Rais wa heshima, mtafukuza msemaji, mtakataa hadi chama tawala na Bimkubwa, Kila kitu kitakuwa kibaya!! Utazuka ugomvi mkubwa! Moto mkubwa utawaka!

Haya njoo sasa huku utopoloni, Sisi Yanga Eng Hersi jeshi la mtu mmoja General wa soka amesema juzikati ligi yoyote hata ya kufukuza kuku au kugombea mbuzi Yanga tukiingia tunapambania kombe tu sisi hatuweki kichwani mawazo ya kijinga sijui ya tunacheza na wakubwa basi tuishie robo fainali, Yanga tukitolewa kwenye ligi yoyote na timu yoyote iwe Lipuli, Faru Dume, Abajalo, Brazil, Bayern Munich, Al Hilal, Denmark, Manchester City au hata iwe AS Vita tunarudi home tunajipanga, ukitufunga poa tu tunajipanga upya si utarudi kwenye 18 tutakubutua tu, yaani hii Yanga ya Sasa ni chuo kikuu Cha mpira!
 
Dah povu la Inonga na Kibu D.Kunywa maji kaa dakika 2 isiposaidia nunua kamba kwa Mangi nitalipa.
Simba tumeipiga kwenye ligi kama ngoma tangu 2019.

Juzikati mikia mmeshinda kwa mizengwe , kona isiyo halali ( wapi VAR) kona iliyopigwa bila filimbi ya Refa , Kona iliyopigwa kwa kuvizia wachezaji wa Yanga hawajajipanga!! Goli likawatoa Yanga mchezoni maana tunajua kwenye Derby ya kkoo Simba ni underdog!!huu ni ukweli mchungu! Yanga ikishinda ni kawaida , Simba ikishinda Watu wanapigwa na butwaa!!

Simba mnajua hamna msuli kuifunga Yanga kihalali bila makandokando!!

Nyie ushindi wa hila mmeshangilia kwa nguvu zote mkalewa hadi wengine wakapasuka kwa ajali za Barabarani, wanasimba wengi wanatibiwa na magari yako gereji yakinyooshwa na kuthibitisha ule msemo " maskini akipata ma... hulia mbwata"!

Msimu huu mna kombe moja tu la kuifunga Yanga!🤪
 
Kwanza nikiri kwamba nitazungumza bila unafiki na kwa nia ya dhati kabisa naomba nitoe mtazamo wangu kwamba tukiwa kama moja ya klabu inayokuja kwa kasi nadhani wanasimba tuna mengi ya kujifuñza kutoka kwa watani zetu Young Africans wanaofanya vizuri nyumbani na kimataifa.

1.Mpira ni uwekezaji
Wenzetu wamewekeza vyema kwa kununua wachezaji mahiri na kocha makini na ndiyo sababu wanafanya vyema katika michuano ya nje na ndani.

2.Mpira si uchawi
Hua nakereka sana kuona katika karne hii ya 21 bado tunaamini katika ushirikina jambo linalotuangusha sana na kuwafanya wenzetu wawe bora zaidi yetu, Kwani mpira umebadilika!

3.Tujikite katika kutafuta vikombe na mataji sio sifa
Kila siku klabu yetu ni kelele tupu mitandaoni na kupeana vichwa lakini ukiuliza tuna makombe/mataji mangapi? Hakuna! Taji ni kuifunga Yanga/Wydad [emoji1] hii ni aibu, tofauti na Yanga wanaopambana kwa malengo ya kutwaa ubingwa

4.Yanga anaongoza kwa kila kitu dhidi yetu, Amechukua ubingwa Ligi kuu mara nyingi zaidi yetu, Bado anaongoza ligi,Ameongoza kundi lake CAF,amechukua vikombe vyote vya ndani wakati huo tukipongezana kuwafunga watanì [emoji1]

5. Nitarudi kuendelea..........

Guvu moya
Kwanini nyani wa pori la utopolo mnapenda sana kujiita Simba? Pambaneni na hali yenu,hapo mnajiona kama ndiyo mumeshachukua hilo kombe lenu la mbuzi
 
Back
Top Bottom