Simba sc wapoteana Zanzibar ,hali tete imejitokeza kwenye benchi la ufundi ,viongozi watoka jukwaani na kuingilia kati

Simba sc wapoteana Zanzibar ,hali tete imejitokeza kwenye benchi la ufundi ,viongozi watoka jukwaani na kuingilia kati

py thon

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2016
Posts
2,476
Reaction score
4,448
Klabu ya soka ya Simba imeyaaga mashindano ya kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa goli 1-0 na URA ya Uganda, mchezo huo ulifanyika uwanja wa Aman

Goli la URA lilifungwa na Bebosi Kalama sekunde chache kabla ya mapumziko. URA wanaungana na Azam hatu ya Nusu Fainali

=====================================================



Klabu ya simba yenye kikosi chenye thamani ya Billion 2 kasoro kidogo inaendeleza wimbi la kufanya vibaya huko Zanzibar.

Ikiwa wametoka kupoteza mchezo dhidi ya Azam siku 2 zilizopita muda huu wapo uwanjani wanachuana na URA ya Uganda na "This is simba" wapo nyuma kwa goli 1 lakini jambo lakushangaza bench la simba limepoteana

Mchezaji kichuya kafanyiwa sabu na mwalimu lakini jambo la kustaajabisha nyota huyo katoka kwa hasira nje huku akiwa amefura na akimpita mwalimu wake mithili ya polisi aliyemuona mwizi na kulikacha benchi la ufundi na kusepa zake

Viongozi waandamizi wa Simba sc roho zipo juu wametoka jukwaani na kwenda kutuliza hali ya sintofahamu mpaka muda huu kimenuka hali sio hali ,kichuya haelewi ,bench Ia ufundi limefura ..vita kubwa inaendelea





4d7352d490edffb4f5ad35ef82ba08a3.jpg


Viongozi wa simba sc waliotoka jukwaani kwenda kutuliza mambo ila kichuya haelewi ,..wakubwa wanaongea yeye kaweka earphone masikioni
 
Ndio maana mpira wa bongo nshaacha kufuatilia . Yaani mchezaji anatolewa kwa maamuzi halali ya mwalimu halafu eti anasusa . Cha kushangaza viongozi wanatoka walipoketi wanakuja kumbembeleza hahaha
Tukitaka tuendelee mpira wetu tuufanye "kisayansi" ........quite unprofessional
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Soka la Bongo bana
 
Back
Top Bottom