Mtawatetea sana viongozi lakini ukweli utabaki kuwa ukweli. Yaani waliacha majembe Okwi, Niyonzima na Kotei kwa mbwembwe wakaleta hao wabrazili ambao hawafiki hata nusu ya uwezo wa wachezaji uliowaacha halafu zigo mnamwangushia Uchebe. Acheni hizo bana mpira unachezwa hadharani uwanja wa taifa na hata Azam TV wanaonyesha live kila week end tunaona. Hivi shughuli ya Okwi utalinganisha na huyo Da Silva wenu. Sasa hivi Boko kawa majeruhi kamuacha Kagere kama yatima hana msaidizi anagombaniwa na mabeki wote wa ligi kuu halafu Uchebe afanye nini aingie yeye kumsaidia Kagere afunge? Kuweni waungwana kubalini Simba ilichemsha kwenye usajili halafu rekebisheni kwenye dirisha dogo maisha yaendelee sio kutafuta mtu wa kumuangushia gunia la misumari. Kwa mtu yeyote anayejua mpira anajua kuwa Uchebe ni mmojawapo wa makocha bora kabisa waliowahi kufundisha soka bongo pamoja na propaganda zinazotumika kwa nguvu kwenye vyombo vya habari kumchafua.