Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Pamoja na yote yaliyotokea, kimsingi Simba hawaruhusiwi kugomea mechi. Wanachotakiwa kufanya ni kuwasilisha malalamiko yao kwa Wasimamizi wa Mpira Tanzania ambao ni TFF.
 
Naunga mkono hoja hakuna kucheza na Yanga huu upuuzi ukifumbiwa macho tunatakuwa na mpira wa kihuni,wapelekeni hata FIFA hawa Yanga kule kuna rungu kali sio hawa FFF
Mtacheza tu na mtakula Chuma nyingi sana leo shenzitaipu
 
Sasa simba wanaenda uwanjani saa tatu usiku na vizee vimejaa basi zima. Ni ushirikina tuu serekali inatakiwa iingilie kati hawa simba na yanga wamezidi uchawi.
fukuza wazee wote walioko simba na yanga, wanafanya nini huko wakati hawachezi mpira? Unakuta timu ina baraza la wazee, hao wazee wanacheza? Wazee wenyewe ni vikongwe hasa pale yanga wamejaa tele, hawa wazee ni washirikina wafurushwe vilabuni ni uchuro mtupu. Sasa kama yanga ina makomando simba haina? Mkono ungepigwa tu, haiwezekani simba iondoke kinyonge uwanjani kisa makomando wa yanga wamewazuia kufanya mazoezi uwanjani hapo
 
Simba inafanyiwa figisu
 
Tukisema timu zitafute viwanja vyao unayasikia yanajibu "Mbona AC Milan na Inter Milan hazina viwanja?"

Sasa lini Milan na Inter zilishindwa kufanya mazoezi?

On a serious note.
Hiki siyo kigezo cha kugomea mechi, hii timu ilikua na mpango wa kufanya mazoezi ya aina gani kwa siku moja ambayo yangewahakikishia kushinda? All over the world kuna timu ngapi zilipofika ugenini walifanyiwa vituko ikiwemo kupigiwa kelele muda wa kulala, kugewa viwanja vya shule ili washindwe kufanya mazoezi au kulazwa airport hata kwa siku moja?

Mpira wa Bongo ni mfu. Ngumu sana kushabikia huu mpira
 
Naomba nisaidie record za Simba na Yanga kutumia uwanja unaotarajiwa kuchezea mechi kwa kufanyia mazoezi ya mwisho
 
simba walitaka kuroga sababu wanaijua yanga isingewaacha salama hivyo baada ya mbinu Yao ya uchawi kufeli wakaona wakimbie mechi🤣🤣🤣🤣
 
Ndio maana huwa sifuatiliagi ligi ya bongo, sio professional kabisa bado ipo enzi za zana za wawe
 
Ndio maana Simba wameamua kutoa adhabu kubwa ya kuwatia hasara kubwa wahusika
 
Watu wanaoamini mambo ya kishirikina huwa ni wapumbavu sana, na hukwamisha mambo kusonga mbele.
 
All TFF idiots are in Dar. Why didn't they consult them to resolve the Kerfuffle? Why didn't they consult the owner of the pitch or police?
Mbuzi tu na ushirikina
 
Simba kagoma, hivyo adhabu ni kupewa Yanga point 3 na Simba kupigwa faini kulingana na sheria za TFF za kukwepa kucheza mechi bila sbb za msingi.

Simba wanaogopa sana Yanga, kama vile Panya kwa Paka.
 
Kwa wanaojua kanuni endapo Simba isipocheza huo mchezo itaadhibiwaje? Faini, kukatwa point, kushushwa daraja

Na vipi kuhusu Yanga nao?
Nadhani hiyo kanuni haito apply , kama kuna kanuni ilivunjwa about uwanja huo. Hii kitu ttf iite pande zote mbili wakae mezani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…