Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Kihoro kinawasumbua simba; wameogopa kichapo. Pamoja na kuwa Uwanja wa mkapa unatumiwa na Yanga pamoja na Simba kama uwanja wa nyumbani, wao siyo wamiliki wa uwanja huo. Mmiliki ni serikali ya tanzania.

Kusema walikuwa mabaunsa wa yanga, ni kisingizioa kischo na mashiko yoyote kisheria.

Woga wa kichapo unawasumbua sana Simba wakati huu..
Pamoja na yote yaliyotokea, kimsingi Simba hawaruhusiwi kugomea mechi. Wanachotakiwa kufanya ni kuwasilisha malalamiko yao kwa Wasimamizi wa Mpira Tanzania ambao ni TFF.
 
Naunga mkono hoja hakuna kucheza na Yanga huu upuuzi ukifumbiwa macho tunatakuwa na mpira wa kihuni,wapelekeni hata FIFA hawa Yanga kule kuna rungu kali sio hawa FFF
Mtacheza tu na mtakula Chuma nyingi sana leo shenzitaipu
 
Sasa simba wanaenda uwanjani saa tatu usiku na vizee vimejaa basi zima. Ni ushirikina tuu serekali inatakiwa iingilie kati hawa simba na yanga wamezidi uchawi.
fukuza wazee wote walioko simba na yanga, wanafanya nini huko wakati hawachezi mpira? Unakuta timu ina baraza la wazee, hao wazee wanacheza? Wazee wenyewe ni vikongwe hasa pale yanga wamejaa tele, hawa wazee ni washirikina wafurushwe vilabuni ni uchuro mtupu. Sasa kama yanga ina makomando simba haina? Mkono ungepigwa tu, haiwezekani simba iondoke kinyonge uwanjani kisa makomando wa yanga wamewazuia kufanya mazoezi uwanjani hapo
 
Katika taarifa kwa Umma waliyoitoa saa 7 na dakika 46 usiku wa 8/3/2025 klabu hiyo imesema haitoshiriki mchezo huo wa Derby uliopangwa kufanyika majira ya saa 1 usiku 8/3/2025 kutokana na kuzuiliwa kufanya mazoezi uwanja wa Benjamin Mkapa na Wanaojiita Makomandoo wa Yanga

Nini maoni yako?

soma zaidiView attachment 3263095

Pia soma:
Simba inafanyiwa figisu
 
Tukisema timu zitafute viwanja vyao unayasikia yanajibu "Mbona AC Milan na Inter Milan hazina viwanja?"

Sasa lini Milan na Inter zilishindwa kufanya mazoezi?

On a serious note.
Hiki siyo kigezo cha kugomea mechi, hii timu ilikua na mpango wa kufanya mazoezi ya aina gani kwa siku moja ambayo yangewahakikishia kushinda? All over the world kuna timu ngapi zilipofika ugenini walifanyiwa vituko ikiwemo kupigiwa kelele muda wa kulala, kugewa viwanja vya shule ili washindwe kufanya mazoezi au kulazwa airport hata kwa siku moja?

Mpira wa Bongo ni mfu. Ngumu sana kushabikia huu mpira
 
Simba hawezi kukatwa pointi kwenye tatizo ambalo ametengenezewa.

Anakatwa point akiwa yeye ndio amevunja kanuni. Hawezi kuwajibika kwenye makosa yaliyofanywa na mtu mwingine.

And by records Simba wapo vizuri kwenye sheria na wanajitahidi sana kuheshimu taratibu za kimpira.

Sitaki kuamini kama wamekuwa wazembe wasione hili uliloliona wewe.
Naomba nisaidie record za Simba na Yanga kutumia uwanja unaotarajiwa kuchezea mechi kwa kufanyia mazoezi ya mwisho
 
Bora mkuu umesema ukweli, mashabiki wenye mihemko mkubwa na Hoya Hoya wanasema kua timu ya Simba imefika saa tatu usiku tena ikiwa na basi limejaa wazee ,, Sasa najiuliza na kipindi huku Kuna simu za kila aina walishindwa nini kudhibitisha hata Kwa video na picha kuonesha basi linaingia saa 3 usiku na picha nyingine waipige ndani ya Basi tukioneshwa hao wazee,,tena tunaambiwa kwa mihemko mkubwa kua walikua wamevaa nguo nyekundu ..kumbe basi linaondoka saa 3 wao ndio wanasema ndio muda walioingia, ujinga mzigo.
simba walitaka kuroga sababu wanaijua yanga isingewaacha salama hivyo baada ya mbinu Yao ya uchawi kufeli wakaona wakimbie mechi🤣🤣🤣🤣
 
Ndio maana huwa sifuatiliagi ligi ya bongo, sio professional kabisa bado ipo enzi za zana za wawe
 
Hili tatizo linatengenezwa na TFF wenyewe kwasababu ya wepesi wa adhabu wanayotoa kwa wakosaji.

Sasa kama sheria ya adhabu inasema faini ni milioni 1 hadi 5.

Kwa Club hizi ambazo mchezaji analipwa zaidi ya milioni 20 basi milion 5 haiwezi kuwa kikwazo wala adhabu ya kuwafanya wajiulize mara mbili pindi wanapofikiria kufanya huu ujinga.
Ndio maana Simba wameamua kutoa adhabu kubwa ya kuwatia hasara kubwa wahusika
 
Watu wanaoamini mambo ya kishirikina huwa ni wapumbavu sana, na hukwamisha mambo kusonga mbele.
 
All TFF idiots are in Dar. Why didn't they consult them to resolve the Kerfuffle? Why didn't they consult the owner of the pitch or police?
Mbuzi tu na ushirikina
 
Simba kagoma, hivyo adhabu ni kupewa Yanga point 3 na Simba kupigwa faini kulingana na sheria za TFF za kukwepa kucheza mechi bila sbb za msingi.

Simba wanaogopa sana Yanga, kama vile Panya kwa Paka.
 
Kwa wanaojua kanuni endapo Simba isipocheza huo mchezo itaadhibiwaje? Faini, kukatwa point, kushushwa daraja

Na vipi kuhusu Yanga nao?
Nadhani hiyo kanuni haito apply , kama kuna kanuni ilivunjwa about uwanja huo. Hii kitu ttf iite pande zote mbili wakae mezani
 
Back
Top Bottom