Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Simba SC yatangaza haitacheza mechi dhidi ya Yanga, Wakidai vitendo visivyo vya kiungwana dhidi yao

Kwa wanaojua kanuni endapo Simba isipocheza huo mchezo itaadhibiwaje? Faini, kukatwa point, kushushwa daraja

Na vipi kuhusu Yanga nao?
Kwanini unakimbilia Simba kuadhiniwa..Kanuni zimekiukwa na mwenyeji wa mchezo
 
Wakati mwingine ujinga sio jambo zuri, hua nikisomaga kejeli za Wana yanga kwenda kwa Simba kua ni wachawi waliloga uwanjani live huko afrika kusini Hadi kupigwa faini na caf..kwamba wao wanajua Mpira sana hawaitaji mambo meusi...kumbe wao ndio wachawi wakubwa na wanaamin upuuzi huo, kama wewe huogopi mambo ya kichawi kutoka kwa timu pinzani kwanini uwazuie kuingia uwanjani, nyinyi si mmeshajizatiti kwa uchawi kama ambavyo Mheshimiwa Awesu aliuambia umma wa WATANZANIA kua Kuna viongozi tena wakubwa wamekua wakirandaranda kwenye Jimbo lake huko pangani kutafuta waganga, Sasa nilitegemea kama uchawi unafanya kazi basi Simba kama.walikua wanakuja kufanya mazoezi basi wangepita free kabisa getini bila bugudha yoyote sababu yanga wameshajizatiti na uchawi kama walikua wanaona Simba wanaingia kuloga badala ya mazoezi
 
Sasa itakuwaje wengi walishajiandaa Leo kwa kushuudia mpambano huo
 
Sasa simba wanaenda uwanjani saa tatu usiku na vizee vimejaa basi zima. Ni ushirikina tuu serekali inatakiwa iingilie kati hawa simba na yanga wamezidi uchawi.
Uliweza kupiga picha ya hao wazee wakiwa ndani ya basi ..utuwekee hapa tuone tudhibitishe hii taarifa yako
 
Simba hawezi kukatwa pointi kwenye tatizo ambalo ametengenezewa.

Anakatwa point akiwa yeye ndio amevunja kanuni. Hawezi kuwajibika kwenye makosa yaliyofanywa na mtu mwingine.

And by records Simba wapo vizuri kwenye sheria na wanajitahidi sana kuheshimu taratibu za kimpira.

Sitaki kuamini kama wamekuwa wazembe wasione hili uliloliona wewe.
Mkuu, mtaji mkubwa wa chama tawala ni watu wenye akili hafifu, akili ndogo, uwezo Mdogo sana kiakili wa kutofikiri kama huyo.
 
Jamaa wamechungulia weee wakaona kushinda tena haiwezekani, wakaamua kutuma bouncers wao. sisi Tupo zetu bunju tunakula daku nyie nendeni mkapige ramli tena
Hahahaaa. Umewaza kama mie Mkuu hawa majamaa walijua na leo wanachezea nyingi. 🤣🤣🤣
 
Meneja wa uwanja ni nani?
Hana boss wake?
Je anapaswa kuambiwa na nani kwamba kikanuni Simba alitakiwa kufanya mazoezi kwenye uwanja kabla ya mechi na muda mechi itakapochezwa?

Baada ya kukataa,hakuna aliyechukua hatua za kumtaarifu?au boss wake naye hajui mpira?

Hao makomandoo wa yanga,wana nguvu kuliko polisi?Kana watu wanaleta vurugu,kwa nini wasikamatwe na kuwekwa ndani?

Hii yanga mnaiendekeza sana,na hawa watu wa siasa wanaolazimisha club iwe ya serikali wanaonyesha upuuzi wa hali ya juu.Wana timu za majeshi lakini hawazipi upendeleo kama huu wanaoipa yanga.

Yanga ni kama vile vikundi vya mazombi kule Zanzibar wakipiga wapinzani halafu serikali nayo inachekelea tu


Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
Hukumsikia kiongozi mmoja mkubwa anayeshuhulikia uchumi wa nchi hii ambapo nilitegemea mtu wa aina yake angekua Yuko bize sana katika kufanya kazi yake ya uchumi wa nchi na WA mwananchi mmoja mmoja, yeye anahoji eti timu kupewa penalty tatu tena kwenye uwanja wenye jina la Waziri mkuu nchini
Wewe hapo mkuu kwa Kauli hii unawaza nini au unaonaje hapo , kwamba refa hatakiwi kufanya kazi yake ya kutekeleza Sheria 17 za soka sababu tu Yuko uwanja wenye jina la Waziri mkuu..hii ni akili ama matope...
 
Kanuni haisemi timu ngeni ikinyimwa kufanya mazoezi iginee

Kanuni haisemi timu ikizuiwa kufanya mazoezi igomee match husika,kanuni ipo wazi Yanga atapigwa faini ya hela au onyo Kali na aliegomea match atakatwa point 3 na magoli matatu.
HIlo lilifanyika mwaka 2021 Yanga walipogoma kucheza?.
 
Allahu Akram.

Hahahaaa. Sa itawezekanaje tena wakati mshasusa Mtani. 🤣🤣
Mechi bado ipo, tunataka tafasiri ya kanuni lakini tutafuata maelekezo ya TFF na Bodi ya ligi.
Kwahiyo kichapo hakiepukiki😂😂
 
Back
Top Bottom