Waganga wa Kipa wako Aishi Manula na Mshambuliaji wako Mzawa John Boko ni Jirani yangu mkubwa mno na najua ni nini Meddie Kagere kafanyiwa mpaka Kiwango chake Kikaisha mazima.
Hawa ni wa Simba SC yangu ila hakuna Wachezaji ambao sasa Wanarogana kama wa Yanga SC na kuna Beki wao Mmoja Mzawa sasa yuko kwa Mtaalam Zanzibar anamtengeneza ( anamroga ) Beki tegemeo wa Kigeni.
Hakuna Mchezaji wa Simba SC ambaye namjua ndani nje kama Mdogo wangu wa Kinondoni Biafra huku Maskani yake Kubwa ikiwa ni Kijiwe cha Unga Unga Kawe na katika Kaunta ya Juu ya Massae Pub Kawe kama Jonas Gerald Mkude.
Sina shaka juu ya Kipaji chake Kikubwa alichonacho na hakuna Mchezaji wa Simba SC GENTAMYCINE ninampenda na nimepambana mno Kumtetea dhidi ya Maadui zake ( ndani na nje ya Simba SC ) kama Jonas Gerald Mkude, ila Mluguru huyu kwa 'Miba' hana mfano.
Mpira wa Tanzania una 'Miba' mno tu.