Simba SC yatangaza kukamilisha usajili wa kiungo nyota Nelson Okwa raia wa Nigeria

Simba SC yatangaza kukamilisha usajili wa kiungo nyota Nelson Okwa raia wa Nigeria

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mnyama Mkali Mwituni, Simba SC kutoka viunga vya Msimbazi jijini Dar es salaam, katika kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya Ligi Kuu, michuano ya Kimataifa msimu wa 2022/23 leo Agosti 3, 2022 imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa kiungo nyota wa Nigeria Nelson Esor Bulunwo Okwa (28) kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya River United ya nchini Nigeria.

Nyota huyu ambaye msimu uliopita kwenye Klabu ya River United ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Nigeria alicheza michezo 24 na kufanikiwa kufunga mabao mawili huku akitoa pasi za mwisho za mabao manne, amekuja kuongeza ubunifu eneo la katikati ya dimba ndani ya Simba SC.

Okwa pia ana uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, lakini kwa klabu ya River United walimtumia kama kiungo wa kati ambapo kazi yake kubwa ni kulinda vema nafasi ya ulinzi, kwani ni mwepesi wa kupora mipira kwa wapinzani na kuanzisha mashambulizi kwa haraka na nguvu.

Kwa usajili huu wa Okwa ni dhahiri kuwa Simba SC wamedhamiria kuimarika zaidi eneo la katikati ya dimba, ambapo Kocha Zaron Maki atakuwa na viungo haswa kuamua kuwatumia nani aanze kulingana na mechi...Mkude, Akpan, Okwa, Mzamiru, Kanoute.

...Kulipewa Mwana Kulitaka Mwana....

20220803_231141.jpg
 
Huyu ni aina ya Ngolo Kante ni mtaalamu wa kuchafua vilivyo pale katikati ya dimba.
Atarogwa na Mkude hadi mtamchukia. Kama Fraga na Lwanga wote wamepotezwa na huyu Dogo Mluguru itakuwa huyo ( huyu ) Okwa wenu?

Mkisikia tu Mkude anaomba Udhuru kwenda Kwao Morogoro jueni Agban na Okwa wanaenda Kupigwa 'Miba' ya maana Kudadadeki zao Wageni hawa wa Kinaijeria.
 
Back
Top Bottom