dakika ya 29 wamesawazisha hapa dah!!! Simba mnatuangusha
 
kipindi cha kwanza kimeisha wekundu 2 wafunga buti 1
 



[h=5]Kiungo wa Simba, Amri Kiemba (kushoto) akijaribu kumtoka kiungo wa JKT Oljoro, Emmanuel Memba katika mechi ya Ligi Kuu
iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba ilishinda 4-1. Picha na Michael Matemanga[/h]
 
....wana Simba mpo....tunaka msimu huu kuchukua ubingwa wa ligi ya Vodacom mapema mno kuliko kawaida.
 
....wana Simba mpo....tunaka msimu huu kuchukua ubingwa wa ligi ya Vodacom mapema mno kuliko kawaida.
Ili tuchukue ubingwa kirahisi inabidi tushinde mechi zote sita zilizobaki za round ya kwanza.
 
Ili tuchukue ubingwa kirahisi inabidi tushinde mechi zote sita zilizobaki za round ya kwanza.

Yees! mechi na Kagera, Simba akiibuka na ushindi: na kama apatajitokeza majeruhi basi uhakika wa kushinda mechi zilizosalia za round ya pili ni mkubwa.
 
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Rushwa yashika hatamu Ligi Kuu [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Friday, 19 October 2012 10:42 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

*Simba, Yanga, Azam zadaiwa kupanga matokeo
Mwandishi Wetu
KASHFA nyingine imezikumba klabu za Simba na Yanga zikidaiwa kuanzisha kampeni ya kutoa fedha kuhakikisha Azam haipati ubingwa msimu huu ambayo inaitwa 'kampeni didimiza Azam'.

Azam inaonekana kuwa tishio katika harakati za Simba na Yanga kuendelea kutawala soka ya Tanzania kwenye miaka ya karibuni.

Habari ambazo Mwananchi ilizipata zinadai kuwa viongozi wa Simba na Yanga walifanya kikao mwezi uliopita kwenye Hoteli ya Kempinski na kukubalina kwamba watahakikisha Azam haichukui ubingwa msimu huu.

Chanzo hicho kilidai kuwa viongozi hao walikubaliana kutumia mbinu zote kuhakikisha Azam haipati ubingwa, pia waliafikiana kutofanya michezo michafu katika michezo yao.

Mwananchi ilipomtafuta Katibu wa Simba, Evodius Mtawala kujibu tuhuma hizo alisema hana taarifa za kikao hicho cha pamoja na kwamba ndiyo kwanza anazisikia habari hizo.

"Sijawahi kusikia kikao kama hicho ndiyo kwanza nasikia kutoka kwako, sijui lolote," alisema Mtawala.

Naye Katibu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema, "Sielewi taarifa hizo kwani ni siasa ambazo nimekuwa nikizisikia kila wakati hivyo sishangazwi nazo zaidi ya kuangalia majukumu yangu ya kazi yanayonikabili."

"Hivi hizo habari mnazipata wapi? Kikao kama hicho ndiyo nakisikia kwako, hakuna taarifa hizo na wala sijasikia tuhuma kama hizo ambazo mimi naziita ni siasa za soka, acha timu zicheze, ni mapema sana kuanza kuzungumza mambo kama hayo ambayo mimi binafsi siyapi nafasi," alisema Mwalusako.

Hata hivyo chanzo chetu cha habari kilidai kuwa,"Kampeni hiyo imeingia dosari hivi karibuni baada ya viongozi wa Simba kudaiwa kutoa fedha kwa Kagera Sugar walipokuwa wanacheza na Yanga ili wawafunge."

"Tumebaini baada ya hapo viongozi wa Yanga nao wameapa kulipiza kisasa kwa Simba kwa kuhakikisha wanapitisha mikono yao kwa kila mechi watakayocheza ili wasiweze kutetea ubingwa wao," alisema kiongozi huyo aliyedai kuwa alishiriki katika kikao hicho ambaye ndiyo chanzo chetu cha habari hii.

Katika hatua nyingine chanzo hicho kilidai kuwa Azam katika kujihami imeingia katika mchezo mchafu wa kutoa fedha ili watwae ubingwa wa ligi baada ya msimu uliopita kuishia katika nafasi ya pili.

Yanga wanadaiwa walitoa ahadi ya Sh10 milioni kwa wachezaji wa Kagera Sugar kama wangeifunga Simba juzi, lakini kwa sare hiyo vijana wa Kagera walikabidhiwa Sh5 milioni huku Azam wakishutumiwa kutoa Sh7milioni kwa waamuzi wa mchezo huo ili kuwakandamiza Simba.

Akizungumzia tuhuma hizo, mratibu wa timu ya Azam, Patrick Kahemela alisema hawajawahi kutumia fedha ili kuharibu mechi ya Simba.

"Hatuna taarifa zozote juu ya kufanyiwa fitina hizo zaidi ya kuangalia malengo yetu ya kutwaa ubingwa kwa kucheza soka la uwanjani," alisema Kahemela.

Hivi karibuni Kocha wa Kagera Sugar, Abdallah Kibaden aliilamikia TFF kwa kushindwa kuchukua hatua ya kupambana na rushwa michezoni.

"Kutokana na baadhi ya waamuzi kuhongwa fedha na kupindisha sheria za soka, siku zote matokeo huwa mabaya na yasiyotarajiwa," alisema Kibaden. [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Muda si mrefu mtanange wa mnyama Simba na Mgambo JKT uwanja mkwakwani mjini Tanga
 
Leo Simba imemchezesha beki wa mwisho kinda wake Hassan Khatib akiwa weka bechi Pascoal na Keitta
 
simba mechi zilizobaki round ya kwanza fanyeni kweli hizi point moja2 zitatuweka nafasi mbaya katika kutetea ubgwa
 
simba mechi zilizobaki round ya kwanza fanyeni kweli hizi point moja2 zitatuweka nafasi mbaya katika kutetea ubgwa

mkuu bemg kaa ukijua round ya 1 ishaisha hiyo maana ina gemu 13 na sasa hivi ni mshacheza 9 bado nne nusu nzima ishaisha..
 
Last edited by a moderator:
Kikosi cha Simba kitakachoanza dhidi ya Azam: Kaseja, Maftah, Ochieng, Hatib, Mkude, Kihemba, Kazimoto, Sunzu, Ngassa na Okwi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…