Uongozi wa klabu ya Simba umetangaza rasmi kucheza na timu ya Asante Kotoko ya Ghana katika tamasha lake la Simba Day, Agosti 8 mwaka huu.
Kupitia kwa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Sunday Manara, amesema Simba itachuana na timu hiyo kongwe ambayo inashiriki Ligi Kuu Ghana kwa ajili ya kuitambulisha timu yao.
Manara amewatangaza Kotoko kucheza nao baada ya hapo awali kuenea kwa taarifa kuwa Simba imewaalika wapinzani wakubwa wa Gor Mahia FC, AFC Leopards kutoka Kenya lakini amezikanusha akisema hazikuwa na ukweli.
Katika msimamo wa Ligi Kuu Ghana, Kotoko wamecheza mechi 15 wakiwa kwenye nafasi ya 4 huku wakijikusanyia alama 24 na Ashanti Gold iliyo nafasi ya kwanza ina alama 27 ikiwa imecheza michezo 15 pia