Yaani jana waziwazi mmenunua mechi...hii nchi kila sehemu ni rushwa tu
 
Gang Chomba huku unafanya nini Bana, nenda kachangamshe Jukwaa lenu la Kandambili ikizingatia leo mna Game sioni Jukwaa likuwa updated
 
Gang Chomba huku unafanya nini Bana, nenda kachangamshe Jukwaa lenu la Kandambili ikizingatia leo mna Game sioni Jukwaa likuwa updated


Weweweee!
Gang Chomba ni Fidel Castro,atakukagua shauri yako!!
Hatujanunua mechi bwana!
 


Gang Chomba: Nyie Simba fanyeni kazi yenu vizuri sana na msijaribu hata kidogo kuvuruga akili yangu kwa kuniletea matokeo mabovu,la sivyo nitawanyuka wote na hakikisheni Kanda 2 asiwaguseni hata nukta moja,mmesikia Simba?
 
Raha ya jana hii hapa



Goli la Banka hilo, kipa ni Dihle wa Maximo!



Mgosi akifanza mambo



Ushindi raha bana! Wacha Maximo aende Kaseja aingie Stars kweli unweza kumlinganisha na Dihile au Kado huyu?
 
Simba kuondoka Jumatano,kuivaa Lengthens ya Zimbambwe.
Clara Alphonce

TIMU ya Simba itaondoka nchini Jumatano ijayo tayari kwa mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi Lengthens ya Zimbambwe.

Afisa Habari wa Simba, Cliford Ndimbo alisema kuna siku mbili ambazo uongozi walikuwa wamependekeza timu kuondoka hapa kati Jumatano au Alhamisi.

Alisema wiki ijayo watatangaza idadi ya wachezaji wanaoenda kwa kuwa hawawezi kutaja kwa sasa kwa kuwa wana mechi moja ya ligi mbele yao dhidi ya Azam hapo Jumapili. Aliongeza kuwa maandalizi ya kujiandaa na michuano hiyo inaendelea na leo wanashuka Dimbani kucheza na Ocean View ya Zanzibar ikiwa
 
Ushabiki Simba, Yanga wavuruga ndoa
Pamela Chilongola

USHINDI wa mabao 3-1 ilioupata Simba dhidi ya JKT Ruvu, Jumamosi ulisababisha kizazaa kwenye maeneo ya Manzese jijini Dar es Salaam kati ya wanandoa.

Wanandoa hao ambao mwanaume ni shabiki wa Yanga na mkewe shabiki wa Simba walijikuta hawaelewani.

Mwandishi wa Mwananchi alishuhudia tukio baina ya wanandoa hao wakigombea redio baada ya Simba kushinda.

Wanandoa hao wakisikiliza redio huku ubishi baina yao ukiendelea, uligeuka baada ya Simba kufunga bao la kwanza na ndipo mwanaume ambaye ni shabiki wa Yanga alipoikimbilia redio na kuizima.

Mwanaume huyo ( jina tunalo) alipozima redio hiyo ndipo ugomvi mkubwa uliibuka baada ya mwanamke(jina pia tunalo) akidai mumewe aiwashe redio asikilize jinsi timu yake anayoipenda ilivyokuwa ikicheza.

Mwanaume huyo alikataa na kumweleza mkewe, "Nende ndani ukalale, mwanamke gani unayependa kushabikia mpira kama wanaume, ondoka hapa, la sivyo nitakupiga".

Mwanamke huyo alipoona mumewe huyo kapandwa na jazba na kuzima redio alimwambia," Leo hii ukinipiga na mimi sikupi unyumba tuone nani zaidi."

Kitendo kile kilimudhi mume wake ambaye alianza kumshushia kipigo mkewe huku akimtamkia kuwa atampa talaka. Hadi Mwananchi inaondoka katika tukio hilo, ugomvi mkubwa uliotokana na ushabiki wa Simba, Yanga ulikuwa ukiendelea na kuvuta watu wengi wakiwa na shauku ya kujua kilichokuwa kikitokea.
 
hakuwa na shida ya unyumba jamaa.si angemuacha mke wake ashangilia ushindi wa timu yake tu na baadae hapewe unyumba kwa furaha.
 
hakuwa na shida ya unyumba jamaa.si angemuacha mke wake ashangilia ushindi wa timu yake tu na baadae hapewe unyumba kwa furaha.
Mkuu jamaa alikuwa na jazba ukizingatia yeye ndio baba mwenye nyumba na redio usikute yy ndo kanunua halafu anaona anafungwa......ila alikuwa na jazba tu na bado
 
Ocean View ya Zenji yatoka 3-3 na simba leo dar
 
Nijuavyo leo tunashuka shamba la bibi kuchuana na Azam, kama ada tupeane updates.
Ubingwa umefika jamani!!!
 

Saitama leo hakuna game mwana
 
ngoja tukale vichwa kwa mugabe maana bongo hakuna mpinzani wala nini
 
ngoja tukale vichwa kwa mugabe maana bongo hakuna mpinzani wala nini

kabisa Mkuu, Ngoja tukalitoe Taifa katika Aibu ya kuwa Kichwa cha Mwendawazimu katika Medani za Kimataifa!

Hivi baada ya kukipga na Wazimbabwe ni Hatua Gani inafuata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…