kwanza nianze kuwapongeza Star Tv na Radio Free Africa kwa namna walivyo lihandle sakata zima ambalo kwa ITV/Radio One wakaamua kususa.
ni kwamba ITV kwakushirikiana na Radio One waliamua kuonyesha mpira wa ligi kuu Tanzania Bara bila kukubaliana na vilabu husika, hii ilipelekea malalamiko toka kwa wadau wa vilabu hivyo kuwa vituo hivyo kupitia maomyesho yake ya Television yanapunguza Idadi ya mashabiki uwanjani. Hii inaweza kuwa kweli ama laah.
Yanga walilalamika , Simba walilalamika.....lakini vituo husika vilikua viziwi.
sasa Ikaja Game moja pale Taifa , sikumbuki ilikua Simba na nani, ila iliihusisha Simba S.C ya mtaa wa Msimbazi.
Katibu Mkuu, ndugu Mwina Seif Kaduguda Simba wa Yuda, hakukubali, akawaendea watangazaji wa TV STATION hizo pale uwanjani na kuwaamuru kuzima MITAMBO yao....lakini wakakaidi. Kaduguda ni mpambanaji asiechoka, akawafuata na kwenda kuzima mitambo ile pale uwanjani yeye mwenyewe, ikaana vurugu.
Baada ya matukio hayo ITV management ikaamua kuisusia Simba katika kila mechi ambayo itakua inacheza.
Kinyume chake Star TV ikaonyesha Ukomavu na Uanamichezo/Fair play, wao wakarudi nyuma wakajipanga , wakaendelea na program zao kama kawaida.
kwa sakata zimahili ITV IMEKOSA HESHIMA mbele ya wadau wa soka, imejivua nguo mbele ya wapenda ustawi wa vyombo vya habari, hakika ITV badilikeni, lazima mjue kua mnahudumia UMMA.....na katika kuhudumia UMMA kuna changamoto za kila namna.