Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Kamwe si dhani, Simba ni taifa kubwa ndio maana timu zote za Tanzania zinapenda kufungwa na Simba ikiwemo Yanga.
Tuache ushabiki hebu tujaribu kuchunguza nini chanzo, tukipata jibu angalau linaelekea tupashane habari. Mkileta habari za watani wa jadi hattajua nini chanzo.
 
Umefika wakati ITV wakatofautisha kazi na mambo binafsi.

haiwezekani kuamua kususia timu bila kutoa tamko la sababu zilizowapelekea kufanya hivyo. hivi akitokea kiongozi mmoja wa Siamba akahamasisha wadau wa timu hiyo kususia bidhaa zote za IPP kwa juma moja tu, nani atakayeathirika?

Kama ITV wangekuwa na busara, wangeweka hadharani sababu za msingi zilizowapelekea kufanya hivyo, ili watu wenye busara waweze kupima nani ni mkosaji.

Kitendo hicho kimenifanya nisisikilize Radio One na ITV kwa miezi kadhaa sasa. Hata kama ningetakiwa kupeleka tangazo la kibiashara huko, ni dhahiri kwamba ningelipeleka kwenye vyombo vinavyosikilizwa zaidi.
 
Kwani ni lazima kila station itangaze mpira? sio kila mtu yuko itrested na mpira wa kibongo wa kurogana.
 
Ni kweli kwenye kipengele cha Michezo wakati wa Taarifa ya Habari ya saa mbili usiku ITV haikutangaza matokeo siku ile Simba ilipotwaa ubingwa, na pia haikutangaza habari yoyote ya matokeo ya mechi ya Jumapili baina ya watani hao wa jadi.

Hiyo juzi Jumapili 18/04/2010 kwenye kipengele cha michezo wakati wa Taarifa ya habari ya saa mbili usiku, ITV ilitangaza taarifa za michezo zifuatazo:
1. Matembezi ya hisani Dar,
2. Matembezi ya hisani ya mazoezi ya viungo Zanzibar,
3. Kutimiza mwaka mmoja tokea kuanzishwa kikundi kimoja cha wasanii wa filamu (kinaitwa Jakaya),
4. Matokeo ya timu ya Tanzania iliyoko Kenya kwenye mashindano ya vishale (darts),
5. Matokeo ya mashindano ya U-17 ya Copa Cococola yanayofanyika Dar.

Mwisho...
 
Kituo cha televisheni cha ITV hakikutangaza kabisa mchezo wa watani wa jadi juzi usiku. Hata timu hizo zilipokutana kwa mara ya kwanza na Simba kutoka kidedea, ITV haikutangaza mchezo ule. Nauliza tatizo ni nini, au kwa kuwa mmiliki wa kituo hicho ni mshabiki wa Yanga?
semeni nyieeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Sababu anazijua Katibu Mkuu wa Simba ustaadh kaduguda. Ni yeye aliyeikataza ITV isitangaze kamwe Mechi za Simba za ligi kuu, licha ya ITV, kuruhusiwa na TFF kufanya hivyo....na kama katazo hilo siku hiyo pale uwanjani kaduguda angelifanya kiungwana kusinge kuwa na kasoro hiyo...lakini alikataza kwa matusi ya nguoni na kejeli kwa crew nzima, na viongozi wao, huku akisistiza kuwa wasitangaze chochote kuhusu Simba. Jamii walipojaribu kujitetea alitishia kuvunja vifaa. Cha kujifunza hapo ni kwa sima kuepuka kuwa na viongozi wasio na mtazamo wa mbali na wanaoendesha mambo kwa jazba bila ya kufikiria athari za mbele.... Ikumbukwe Gumbo naye alishawahi kusababisha msigano kama huo kwa mambo ya kitoto kama hayo.
 
Cha kujifunza hapo ni kwa simba kuepuka kuwa na viongozi wasio na mtazamo wa mbali na wanaoendesha mambo kwa jazba bila ya kufikiria athari za mbele.... Ikumbukwe Gumbo naye alishawahi kusababisha msigano kama huo kwa mambo ya kitoto kama hayo.

Uongozi wa ITV nao unapaswa kujua kuwa 'two wrongs don't make it right' - kisasi hakisahihishi kosa na kuwa ukibishana na mjinga, watu watashindwa kutofautisha mwerevu kati yenu...
 
Ugomvi wa IPP Media na Simba ni wa muda mrefu kidogo; mwanzoni ilikuwa ni Redio One ndio waligoma kutangaza habari zihusuzo timu ya Simba. Tatizo ni kuna kiongozi wa Simba alitoa tamko lihusulo timu yao, baadae kiongozi mwingine nakumbuka ilikuwa ni Gumbo akapinga hilo tamko akiwa Tanga na RO walimweka hewani akiongea kwa njia ya simu, lakini kesho yake Gumbo akakana kwamba si yeye aliyeongea na RO bali huo ulikuwa ni mchezo wa RO kuwagombanisha viongozi wa mnyama, kuanzia hapo RO wakawa kimya na habari za Simba. Hili la ugomvi na ITV nadhani limesababishwa na uswahili wa viongozi wa Simba, ITV walipewa kibali cha kuonyesha mechi za raundi ya pili ya ligi ya Vodacom na mwenye ligi yake (TFF), badala ya Simba kuwasiliana na TFF kujua terms zikoje wakataka kuvunja mitambo ya ITV ya kurushia matangazo live kuanzia hapo ukawa mwisho wa ITV kumrusha mnyama!!!!!!
 
Kwa maana hiyo kampuni za tiGO na Coca cola zinakula hasara kwa kudhamini kipindi cha michezo cha RO ambacho sasa hakisikilizwi na mamilioni ya washabiki wa Simba. Halafu ukifuatilia kwa makini utagundua hata wale wadau wanaohojiwa katika kipindi hicho wanakuwa wamefundishwa namna ya kujibu ili wasilitamke neno 'Simba'. Utakuta wakati mwingine Simba inabidi itajwe tu, lakini jamaa wamewaambia watumie neno lingine. Nilishangaa hata wadhamini wa ligi kwa sasa wanawatii RO kukwepa kuitaja Simba katika kipindi hicho ! TIGO na COCA COLA angalieni hela zenu za udhamini pale RO, mnaliwa bure!!!
 
kwanza nianze kuwapongeza Star Tv na Radio Free Africa kwa namna walivyo lihandle sakata zima ambalo kwa ITV/Radio One wakaamua kususa.
ni kwamba ITV kwakushirikiana na Radio One waliamua kuonyesha mpira wa ligi kuu Tanzania Bara bila kukubaliana na vilabu husika, hii ilipelekea malalamiko toka kwa wadau wa vilabu hivyo kuwa vituo hivyo kupitia maomyesho yake ya Television yanapunguza Idadi ya mashabiki uwanjani. Hii inaweza kuwa kweli ama laah.
Yanga walilalamika , Simba walilalamika.....lakini vituo husika vilikua viziwi.
sasa Ikaja Game moja pale Taifa , sikumbuki ilikua Simba na nani, ila iliihusisha Simba S.C ya mtaa wa Msimbazi.
Katibu Mkuu, ndugu Mwina Seif Kaduguda Simba wa Yuda, hakukubali, akawaendea watangazaji wa TV STATION hizo pale uwanjani na kuwaamuru kuzima MITAMBO yao....lakini wakakaidi. Kaduguda ni mpambanaji asiechoka, akawafuata na kwenda kuzima mitambo ile pale uwanjani yeye mwenyewe, ikaana vurugu.
Baada ya matukio hayo ITV management ikaamua kuisusia Simba katika kila mechi ambayo itakua inacheza.
Kinyume chake Star TV ikaonyesha Ukomavu na Uanamichezo/Fair play, wao wakarudi nyuma wakajipanga , wakaendelea na program zao kama kawaida.
kwa sakata zimahili ITV IMEKOSA HESHIMA mbele ya wadau wa soka, imejivua nguo mbele ya wapenda ustawi wa vyombo vya habari, hakika ITV badilikeni, lazima mjue kua mnahudumia UMMA.....na katika kuhudumia UMMA kuna changamoto za kila namna.
 
Sababu anazijua Katibu Mkuu wa Simba ustaadh kaduguda. Ni yeye aliyeikataza ITV isitangaze kamwe Mechi za Simba za ligi kuu, licha ya ITV, kuruhusiwa na TFF kufanya hivyo....na kama katazo hilo siku hiyo pale uwanjani kaduguda angelifanya kiungwana kusinge kuwa na kasoro hiyo...lakini alikataza kwa matusi ya nguoni na kejeli kwa crew nzima, na viongozi wao, huku akisistiza kuwa wasitangaze chochote kuhusu Simba. Jamii walipojaribu kujitetea alitishia kuvunja vifaa. Cha kujifunza hapo ni kwa sima kuepuka kuwa na viongozi wasio na mtazamo wa mbali na wanaoendesha mambo kwa jazba bila ya kufikiria athari za mbele.... Ikumbukwe Gumbo naye alishawahi kusababisha msigano kama huo kwa mambo ya kitoto kama hayo.

Wacha bwana! Kinachoonekana hapa ni kutopevuka kimaadili ya kazi Kwa ITV. Hivyo Habari zinakuwa na mwenyewe? Biashara ya habari ndio inakuwa na mwenyewe kwani kama ITV walitaka kutangaza mpira mojakwamoja walipaswa kukubaliana na wahusika kwani walichotaka kufanya ni biashara kwani si kweli kuwa wasingepata mapato kwa kutangaza michezo ya Simba.
Sasa ITV inapoamuwa kugoma kutangaza habari inayohusu Simba ina maana gani? Kuikomoa Simba au kuwakosesha habari Watanzania? Naamini waandishi wa ITV wanakwenda kwenye mechi za Simba kwa koti la uandishi wa habari na hii ni sawa na ule msemo wa Kiswahili wa Baniani mbaya kiatu chake dawa.
Ushauri wangu ni kuwa ITV iachane na tabia zisizo za kiuandishi na waige wenzao wanaojeruhiwa kwenye vita na wakaendelea kutowa habari. Simba haikomoki kwani hucheza mpira uwanjani sio ndani ya ITV na ndio maana wakachukuwa ubingwa mbali ya mgomo wa ITV
 
Ugomvi wa IPP Media na Simba ni wa muda mrefu kidogo; mwanzoni ilikuwa ni Redio One ndio waligoma kutangaza habari zihusuzo timu ya Simba. Tatizo ni kuna kiongozi wa Simba alitoa tamko lihusulo timu yao, baadae kiongozi mwingine nakumbuka ilikuwa ni Gumbo akapinga hilo tamko akiwa Tanga na RO walimweka hewani akiongea kwa njia ya simu, lakini kesho yake Gumbo akakana kwamba si yeye aliyeongea na RO bali huo ulikuwa ni mchezo wa RO kuwagombanisha viongozi wa mnyama, kuanzia hapo RO wakawa kimya na habari za Simba. Hili la ugomvi na ITV nadhani limesababishwa na uswahili wa viongozi wa Simba, ITV walipewa kibali cha kuonyesha mechi za raundi ya pili ya ligi ya Vodacom na mwenye ligi yake (TFF), badala ya Simba kuwasiliana na TFF kujua terms zikoje wakataka kuvunja mitambo ya ITV ya kurushia matangazo live kuanzia hapo ukawa mwisho wa ITV kumrusha mnyama!!!!!!

Hivyo hujangalia BBC, NN, Aljazira na wengineo wakionyesha habari za pande zote ndani ya Vita? Habari ni habari na zinataka kutangazwa na hakuna mtu atakaezizuia lakini uhapotaka kufanya kitu ALIVE basi ni jambo jengine ni lazima kuwepo na makubaliano maalu. Hivyo unahisi TFF inahaki zaidi kuliko timu zinazocheza? Hivyo katika ulimwengu wetu kumkiuka muhusika mkuu si jambo la makusudi kukimbiza majukumu? TFF Vs ITV bila ya timu zinazohusika si upungufu huo?
 
Bottom line: ITV + Radio One ni wapuuzi.
 
Sababu anazijua Katibu Mkuu wa Simba ustaadh kaduguda. Ni yeye aliyeikataza ITV isitangaze kamwe Mechi za Simba

Nyie mnaowasema ITV/RO, mmesoma hapo juu kwa makini???
Binafsi yangu sioni tatizo lolote, kuna redio zaidi ya 200, ambako unaweza kusikiliza habari za simba sports, na si lazima kwa hao jamaa, labda kama kuna malipo yoyote yanayotolewa kwa kuwasikiliza!!!!:smile-big:
 
kirahisi huwezi kuona athari za vyombo vya habari kutokutimiza wajibu wao......
 
ITV walitangaza mechi ya Simba na ndipo mnyama alipotaka malipo. Ubishi, utoto, ubabe, ufinyu ndio umewafikisha hapo.
 
ITV walitangaza mechi ya Simba na ndipo mnyama alipotaka malipo. Ubishi, utoto, ubabe, ufinyu ndio umewafikisha hapo.

KWANI wewe unafikiri Simba wanaendesha klabu kwa kupokea sadaka, eeeh Jafar ? kwani unadhani ITV ILIKUA INASHURA BILA KUWA NA UHAKIKA WA WADHAMIN ? Kweli wavunje vipindi kwa zaidi ya dakika 90 bureee.
ITV walipaswa kuzungumza na viongozi wa vilabu kabla ya kurusha zile game.
 
Sababu anazijua Katibu Mkuu wa Simba ustaadh kaduguda. Ni yeye aliyeikataza ITV isitangaze kamwe Mechi za Simba za ligi kuu, licha ya ITV, kuruhusiwa na TFF kufanya hivyo....na kama katazo hilo siku hiyo pale uwanjani kaduguda angelifanya kiungwana kusinge kuwa na kasoro hiyo...lakini alikataza kwa matusi ya nguoni na kejeli kwa crew nzima, na viongozi wao, huku akisistiza kuwa wasitangaze chochote kuhusu Simba. Jamii walipojaribu kujitetea alitishia kuvunja vifaa. Cha kujifunza hapo ni kwa sima kuepuka kuwa na viongozi wasio na mtazamo wa mbali na wanaoendesha mambo kwa jazba bila ya kufikiria athari za mbele.... Ikumbukwe Gumbo naye alishawahi kusababisha msigano kama huo kwa mambo ya kitoto kama hayo.

Lakini swali ni kuwa kwanini kaduguda alifanya hivyo? Alikuwa ni chizi yeye wa kufanya hayo yote bila sababu?
 
Kwa kuanzia siku hizi sihangalii ITV kabisa na kitakachofuata sitakunywa maji ya Kilimanjaro na Coke products...isnt it simple?
 
Back
Top Bottom