Tuache ushabiki hebu tujaribu kuchunguza nini chanzo, tukipata jibu angalau linaelekea tupashane habari. Mkileta habari za watani wa jadi hattajua nini chanzo.Kamwe si dhani, Simba ni taifa kubwa ndio maana timu zote za Tanzania zinapenda kufungwa na Simba ikiwemo Yanga.
semeni nyieeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeKituo cha televisheni cha ITV hakikutangaza kabisa mchezo wa watani wa jadi juzi usiku. Hata timu hizo zilipokutana kwa mara ya kwanza na Simba kutoka kidedea, ITV haikutangaza mchezo ule. Nauliza tatizo ni nini, au kwa kuwa mmiliki wa kituo hicho ni mshabiki wa Yanga?
Dalani alimtukana Mengi na vyombo vyake vya habari na Mengi akaapa hatatangaza kamwe habari za Simba
Cha kujifunza hapo ni kwa simba kuepuka kuwa na viongozi wasio na mtazamo wa mbali na wanaoendesha mambo kwa jazba bila ya kufikiria athari za mbele.... Ikumbukwe Gumbo naye alishawahi kusababisha msigano kama huo kwa mambo ya kitoto kama hayo.
Sababu anazijua Katibu Mkuu wa Simba ustaadh kaduguda. Ni yeye aliyeikataza ITV isitangaze kamwe Mechi za Simba za ligi kuu, licha ya ITV, kuruhusiwa na TFF kufanya hivyo....na kama katazo hilo siku hiyo pale uwanjani kaduguda angelifanya kiungwana kusinge kuwa na kasoro hiyo...lakini alikataza kwa matusi ya nguoni na kejeli kwa crew nzima, na viongozi wao, huku akisistiza kuwa wasitangaze chochote kuhusu Simba. Jamii walipojaribu kujitetea alitishia kuvunja vifaa. Cha kujifunza hapo ni kwa sima kuepuka kuwa na viongozi wasio na mtazamo wa mbali na wanaoendesha mambo kwa jazba bila ya kufikiria athari za mbele.... Ikumbukwe Gumbo naye alishawahi kusababisha msigano kama huo kwa mambo ya kitoto kama hayo.
Ugomvi wa IPP Media na Simba ni wa muda mrefu kidogo; mwanzoni ilikuwa ni Redio One ndio waligoma kutangaza habari zihusuzo timu ya Simba. Tatizo ni kuna kiongozi wa Simba alitoa tamko lihusulo timu yao, baadae kiongozi mwingine nakumbuka ilikuwa ni Gumbo akapinga hilo tamko akiwa Tanga na RO walimweka hewani akiongea kwa njia ya simu, lakini kesho yake Gumbo akakana kwamba si yeye aliyeongea na RO bali huo ulikuwa ni mchezo wa RO kuwagombanisha viongozi wa mnyama, kuanzia hapo RO wakawa kimya na habari za Simba. Hili la ugomvi na ITV nadhani limesababishwa na uswahili wa viongozi wa Simba, ITV walipewa kibali cha kuonyesha mechi za raundi ya pili ya ligi ya Vodacom na mwenye ligi yake (TFF), badala ya Simba kuwasiliana na TFF kujua terms zikoje wakataka kuvunja mitambo ya ITV ya kurushia matangazo live kuanzia hapo ukawa mwisho wa ITV kumrusha mnyama!!!!!!
kirahisi huwezi kuona athari za vyombo vya habari kutokutimiza wajibu wao......Sababu anazijua Katibu Mkuu wa Simba ustaadh kaduguda. Ni yeye aliyeikataza ITV isitangaze kamwe Mechi za Simba
Nyie mnaowasema ITV/RO, mmesoma hapo juu kwa makini???
Binafsi yangu sioni tatizo lolote, kuna redio zaidi ya 200, ambako unaweza kusikiliza habari za simba sports, na si lazima kwa hao jamaa, labda kama kuna malipo yoyote yanayotolewa kwa kuwasikiliza!!!!:smile-big:
ITV walitangaza mechi ya Simba na ndipo mnyama alipotaka malipo. Ubishi, utoto, ubabe, ufinyu ndio umewafikisha hapo.