Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Pole mkuu Ivuga,ila mmetusaidia kujua nyie ni wataalam wa rufaa,uwanjani makida2.

Watasingizia kuwa Samatta hakuwepo! Rudini mjipange upya kwa ajili ya Kagame maana Rage alishaanza fitina ili Yanga isishiriki Kagame mwaka huu! Na wasiposhiriki Yanga basi mashindano yatakosa watazamaji maana waatu hawana msisimko na Simba tena baada ya mechi mbili hizi!
 
[TABLE="width: 650, align: center"]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #ffffff"]Kocha wa Simba awatuliza vijana[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #ffffff"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: storyheader, bgcolor: #ffffff"]MICHAEL MOMBURI, KINSHASA
KIPIGO cha mabao 2-0 dhidi ya Motema Pembe kimewachanganya wachezaji wa Simba lakini kocha Moses Basena amewatuliza.

Kocha huyo alisema kuwa hawakustahili kipigo kikubwa kwa kiwango cha soka walichocheza mjini hapa, hususani kipindi cha kwanza.

"Nimesikitika sana kwa hali iliyotokea, tumecheza vizuri na hatukustahili matokeo hayo, tupo nje ya mashindano, imeshatokea tunaendelea na mambo mengine," alisisitiza kocha huyo ambaye hakuwa na raha muda wote.

Baada ya mchezo huo, wachezaji kwenye vyumba vya kubadilishia nguo walikuwa wakiambiana ukweli kuhusiana na kilichotokea huku baadhi wakionekana kuchanganyikiwa, lakini Basena akawatuliza.

"Tulieni, mchezo umekwisha tutakaa tujadiliane kwa utaratibu," alisema kocha wakati akiongea na wachezaji na kufuta zogo lililokuwa limetawala kwenye kikao chao cha siri.

Simba imetolewa kwenye Kombe la Shirikisho na sasa inajiandaa na Kombe la Kagame linaloanza jijini Dar es Salaam wikiendi hii.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
[TABLE="width: 650, align: center"]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #ffffff"]Rage aapa kutokanyaga Kinshasa[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: headline, bgcolor: #ffffff"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: storyheader, bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 51%, align: left"]
[TR]
[TD]
7303.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: mwanacss, bgcolor: #b47c01"]Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
MICHAEL MOMBURI, KINSHASA
MWENYEKITI wa Simba, Ismail Aden Rage, ameapa kwamba timu hiyo haitakanyaga Kinshasa milele na wakipangiwa watajitoa kwani si sehemu salama na amesema watashtaki kwa Serikali ya Tanzania.

Simba ilifungwa mabao 2-0 juzi Jumapili katika mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya DCMP ya hapa na kuondoshwa katika mchezo huo uliogubikwa na fujo za kila aina ndani na nje ya uwanja.

Baada ya mchezo huo, maelfu ya mashabiki walivamia uwanja kwa lengo la kuidhihaki Simba jambo ambalo lilifanya askari wa usalama kuwatuliza wachezaji na viongozi kwenye benchi la ufundi na kuwazunguka kuwaepusha na fujo hizo zilizodumu mpaka usiku.

Dakika chache baadaye wachezaji hao walisindikizwa tena hadi vyumba vya kubadilishia nguo na kutulizwa kwa zaidi ya saa moja hadi hali ilipotulia, lakini hata mitaani askari walitumia nguvu za ziada na vitisho vya hapa na pale kufungua njia ingawa bado walikuwa wabishi.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alisema; "Wametufanyia mambo mabaya sana, hizi ni hujuma ambazo hazivumiliki, ndiyo maana nasema Simba haitakanyaga milele Kinshasa.

"Hatutakuja kucheza mechi yoyote hapa kwa vurugu hizi, tutagawa pointi za bure. Labda Serikali itoe tamko na tupewe ulinzi maalumu au tucheze nje ya hapa. Na tutakwenda kushtaki Wizara ya Mambo ya Nje kuhusu unyama tuliofanyiwa hapa Kinshasa.

"Tungeshinda tusingetoka hapa uwanjani, wangetuua hawa," alisisitiza kiongozi huyo, ambaye amependekeza ianzishwe vita dhidi ya raia wote wa DR Congo wanaoishi nchini kinyume cha sheria.

Simba iliwasili jijini Dar es Salaam jana Jumatatu, saa 12.45 jioni kwa ndege ya KQ.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Simba: Hatuhofii timu za kundi letu Send to a friend Wednesday, 22 June 2011 21:27 0diggsdiggKipa wa Simba, Juma Kaseja.Clara AlphonceKIPA wa Simba, Juma Kaseja na kocha wake, Moses Basena wamesema kuwa kundi lao la michuano ya Kagame ni gumu lakini hawahofii chochote.Simba ipo kundi A la Michuano ya Kagame ikiwa na timu Vital'O (Burundi), Etincelles (Rwanda) na Ocean Boys ya Zanzibar.Wawakilishi hao wa Tanzania, wataingia dimbani Jumamosi kukwaana na Vital'O katika mchezo wa kwanza wa michuano hiyo. Simba ndiyo inayoongoza kwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo mara sita.Kaseja alisema kuwa pamoja na kuwa timu yao imepangwa katika kundi gumu, lakini hicho ndicho kipimo kizuri kwa timu yao kuona kuwa wamejiandaa kiasi gani.Alisema michuano hiyo lazima itakuwa migumu sana kwa kuwa tila imu imejiandaa vya kutosha mwaka huukuakikisha inachukua kombe.Kaseja aliongeza kuwa michuano hiyo ni muhimu kwao kwani ni maandalizi tosha kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kwa kocha kupima usajili wake kama ulikuwa sahihi au la.''Bado hatujakata tamaa pamoja na kutolewa kwenye mashindano ya kimataifa bado tuna nafasi ya kufanya vizuri mashabiki wazidi kutupa moyo na kutusapoti zaidi ya hapo nyuma,'' alisema Kaseja.Naye Basena alisema kuwa kwa upande wake, haoni kama kundi walilopangwa ni gumu isipokuwa kinachotakiwa ni kujipanga vizuri tu huku akisisitiza mchezaji atakayepewa nafasi kubwa ni yule atakayeonyesha uwezo mazoezini na anayejituma.Alisema kwa wachezaji wavivu wasahau kuanza katika kikosi chake kwani anachotaka katika michuano hiyo ni kufuta makosa yaliotokea hivi karibuni kutwaa kombe hilo mwaka huu.Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Evodius Mtawala alisema kuwa kwa upande wao viongozi wamejipanga vizuri na wametekeleza maombi ya kocha wao kwa asilimia kubwa ikiwemo kuiweka timu yao kambini.Wakati huo huo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limewatangaza wachezaji wa Simba ambao wamemaliza waliomaliza mikataba ni George Owino, Rashid Gumbo, Hilal Echessa. Taarifa ya Simba kupitia TFF ilisema kuwa Patrick Ochan, Mbwana Samata wameuzwa TP Mazembe wakatia Abdullahim Humud wamebadilishana na Azam FC.Wanaokwenda kwa mkopo timu nyingine ni Aziz Gila, Meshack Abel, Haruna Shamte, David Naftari, Juma Jabu na Ahmed Shibori ambaye hata hivyo alikataa kuuzwa kwa mkopo akisema bora arudi PembaKatika hatua nyingine, Katibu wa TFF, Angetile Osiah aliwapa pole wachezaji na viongozi wa Simba kutokana vurugu walizofanyiwa na mashabiki wa DC Motema Pembe katika pambano lao wiki iliyopita.
 
Nawapongeza sana Simba kwa kutinga fainali lakini nimesikitishwa sana na bango lenu '...uwezo tunao hatuhitaji kubebwa'. Hapa mlimaanisha kuwa Yanga ilibebwa dhidi ya Red Sea. Kisheria golikipa hatakiwi kutoka kwenda kwa mbele wakati penati haijapigwa, ukiangalia replay, yule golikipa alikuwa akitoka! Sasa kubebwa kuko wapi? Acheni ushamba watani.
 
DAH! LEO NDIO NIMEELEWA YANGA NI TIMU YA MIJITU ISIYOJUWA KITU AU ELIMU YA FIKRA. MICHUZI BLOG NIMEONA BANGO LA MAANDISHI IMEANDIKA KWA KISWAHILI ILA BADO http://2.bp.blogspot.com/-C33mq0xQQ_E/ThcHxTudEZI/AAAAAAABo9A/aczY4NfHTAE/s1600/IMG_8109.jpg KISWAHILI TU KINAWASHINDA KUANDIKA NA KUELEWA..

IMEANDIKWA KWENYE SIMBA IMEKUWA SIMB ILE A IMEKAA IKITOKA KAA-A, SAWA TUNAWEZA KUSEMA MWANZO WALIANDIKA MWANA MAMA KAA MSUBIRI MUMEO YANGA, MUANDISHI ALITETEMEKA KUANDIKA SIMBA KWA UOGA WA SIMBA TEHTEH. KENGINE NATAKA KUWAFAHAMISHA YANGA MAANA YA MWANA NI "MTOTO" KWA HIYO SIE NI MTOTO WA MAMA HERI YETU SIJUI NYIE SASA MTAKUWA MUME ALIYEGEUZWA SHOGA NA MTOTO WA MAMA WA MNYAMA SIMBA. JUMAPILI HAPO JITAARISHENI NA KIKAO CHA RAISI NAKINA MANJI MJIPANGE VIZURI NA UFISADI WENU.
 
Kwa kutumia mchezo wa leo kati ya simba na yanga,nimebaini kuwa simba ndo timu yenye mashabiki wengi kuliko yanga,kwa aliyekuwa uwanjan atakubaliana na mimi.(nimetumia mechi ya leo kama sample kulingana na msisimko uliokuwepo,naamini mashabiki wa timu zote walikuja uwanjani kwa idadi kubwa)
 
una matatizo ya msingi yan mechi ya leo tu ndo umake conclusion?,pole sana na wingi wa mashabiki nini mmefanya?
 
Kwa kutumia mchezo wa leo kati ya simba na yanga,nimebaini kuwa simba ndo timu yenye mashabiki wengi kuliko yanga,kwa aliyekuwa uwanjan atakubaliana na mimi.(nimetumia mechi ya leo kama sample kulingana na msisimko uliokuwepo,naamini mashabiki wa timu zote walikuja uwanjani kwa idadi kubwa)
Leo ndo nimeamini kuwa Simba ni vibonde vya Yanga. Wachumbaaaaaaaaa!!!!
 
Duh Mkuu umechemka hata historia ya soka hujui, ila navyojua mimi Yanga ni Bingwa wa Kagame au?
 
Sio shabiki wa mpira mimi,nimeenda tu kuangalia angalia baada ya kupata tiket ya bure, nyie vipi?
 
Back
Top Bottom