Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
poleni sanandugu zangu ila tusife moyo mechi za leo ilikuwa kama kurusha shilingi
 
mimi nimeumia sana maana nilitengewa chakula tangia jioni nikashindwa kula tokana na presha ya mechi

lakini sasa hivi ndo kabisa sina hamu ya kula japo njaa yaniuma mbaya
 
Kwani uongo mkuu?????????????

hata mtu anaweza kuwa na mgogoro na mke wake sembuse sisi msimbazi. but hayo ni maneno yako tu mkuu Balantanda.
wewe unafikiri hata Mani atawashikilia hadi lini
 
mimi nimeumia sana maana nilitengewa chakula tangia jioni nikashindwa kula tokana na presha ya mechi

lakini sasa hivi ndo kabisa sina hamu ya kula japo njaa yaniuma mbaya
mkuu mistake kubwa sana tulifanya kwenye mechi na JKT
 
pole sana Crashwise ,ndugu yangu sijui upo kwenye hali gani huko
 
hata mtu anaweza kuwa na mgogoro na mke wake sembuse sisi msimbazi. but hayo ni maneno yako tu mkuu Balantanda.
wewe unafikiri hata Mani atawashikilia hadi lini

Pamoja mtani............Kila la heri
 
Mkuu, hapa kwetu kanuni ni goal difference, hatutumii head to head. Sasa kitakachotokea ni nini? Simba tutamfunga Majimaji 5-0, halafu yanga nao kupitia mobile phones watajua sisi tuna goli 5, kwa hiyo watamwambia John Tegete(baba wa Jery) afanye maarifa na ndipo Toto(makusudically kabisa!!!) wataachia goli 6 na yanga kuwa bingwa kwa goal difference. Then TFF watasema hii haikubaliki, watafuta matokeo na kuipa Azam Ubingwa. Sasa cha ajabu hawatazishusha Simba na yanga daraja.

Kwani matokeo yalikuwaje?
 
Mabingwa wanatua saa 7 mchana jiji dar wapenzi wanachama na wanasimba mnaalikwa kuwapokea mabingwa
 
Inauma sana,basi bwana si bahati yetu.Poleni wapenzi wote.
 
SIKU moja baada ya kukosa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara, uongozi wa Simba umepanga kufumua benchi zima la ufundi pamoja na kuwatimua wachezaji 15.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema uongozi wake unatarajia kufanya maamuzi magumu ya kihistoria katika klabu yao.

Habari ambazo zilizopatikana jana kutoka ndani ya Simba zinasema kuwa klabu hiyo imepanga kuwatupia virago nyota wake kadhaa akiwemo mshambuliaji Musa Hassan 'Mgosi', Meshack Abeil, Mohamed Banka na Kelvin Yondani.

"Mgosi amejisahau sana alikuwa anacheza kwa kuridhika, Yondani kilichomposa ni utovu wa nidhamu aliondoka kambini toka mechi ya Mazembe bila ya kuomba ruhusa na ajaripoti kambini mpaka ligi imekwisha,"kilisema chanzo hicho.

Wachezaji wengine ambao wataachwa kwenye kikosi hicho cha Msimbazi ni wale walioshuka viwango huku baadhi yao wakituhumiwa kujiingiza kwenye mgogoro wa chini kwa chini wa viongozi kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kimesababisha timu hiyo kushindwa kutetea ubingwa wake msimu huu.

"Kutokana na matokeo mabovu ya mechi za mwisho za Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar, JKT Ruvu na Majimaji uongozi unatarajia kukifanyia mabadiliko makubwa kikosi chetu kwa kuwatema baadhi ya wachezaji, kutokana kushindwa kuzingatia majukumu yao na kujihusisha na vitendo vya ajabu ambavyo kwa namna moja au nyingine vimechangia kupoteza ubingwa huo dakika za mwisho.

Naye Rage alisema kuwa baada ya kushindwa kutetea ubingwa wao msimu huu kwa kukosa bao moja katika historia ya Ligi ya Tanzania kwani haijawai kutokea amewataka mashabiki wao kuwa watulivu na kukubali matokeo kwani huo ndio mpira.

Alisema kuwa hata hivyo amewataka Kamati ya Ufundi na kocha Patrick Phiri kuandaa ripoti ambayo itaeleza kwanini msimu huu wamekosa ubingwa na kutoa mapendekezo yao na kuiwakalisha kwenye kamati ya utendaji Alhamisi.

Alisema baada ya hapo Kamati ya utendaji ya Simba itakutana mwishoni mwa wiki hii kwa ajili ya kuipitia ripoti hiyo na kutoa maamuzi magumu ambayo hayajawahi kufanywa na mtu yoyote katika klabu hiyo.

Rage aliongeza kuwa maamuzi hayo watakayotoa yatakuwa na faida kwa klabu ya Simba na nchi nzima kwa ujumla kwa ajili ya kuondeleza soka hapa nchini.

KIPA WA MAJIMAJI
Tetesi kuwa kipa namba moja wa Majimaji, Said Mohamed amesajiliwa na Yanga zilisababisha asipangwe katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu dhidi ya Simba uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo wa mwishoni mwa wiki Simba ilishinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji, lakini hakuwasaidia kutetea ubingwa wao.

Akizungumza na Mwanachi jana Mohamed alisema viongozi na benchi la ufundi la timu ya Majimaji waliamua kutompanga kipa huyo kwa madai atavuruga mipango iliyokuwa ifikiwa dhidi ya viongozi wa Simba na wale wa timu hiyo kutoka na kudaiwa kuwa tayari ameshasajiliwa na timu ya Yanga.

"Sikuwa naumwa wala kusumbuliwa na tatizo lolote isipokuwa viongozi wangu ndiyo walisababisha nisicheze katika mechi hiyo kutokana madai kuwa tayari nishasajiliwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao hivyo nitavuruga mipango waliyokuwa waafikiana na uongozi wa Simba katika mechi hiyo.

"Hata hivyo hali hiyo kwa namna moja au nyingine haikuwafurahisha baadhi ya wachezaji na meneja wetu Steven Mapunda jambo lililozua tafrani kwenye chumba cha kubadilishia nguo, lakini majibu yake yalionekana uwanjani kulikuwa na walijituma na wasiojituma," alisema Mohamed.
 
Mkuu, si rahisi hivyo, Wekundu wa Msimbazi kujivua gamba ni sawa na kumenya kiazi, maana lazima utakata nyama . Lile gamba ni gumu sana na limeshikana na ngozi sasa utalivuaje ili kubaki salama!

Ili gamba litoke kunahitajika uvumilivu wa hali ya juu kutoka kwa wanachama na pia wanachama wajitoe kwa kiwango kikubwa na kuonesha mapenzi ya kutoka moyoni na siyo mdomoni na pia wawe tayari kukubaliana na lolote ikiwepo hatari ya kushuka daraja kama si kushuka kabisa, na kama hilo likitokea basi gamba litatoka na Simba mpya itakuja na ambayo itaweza ku-compete independently!
 
Back
Top Bottom