Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Dr.kigwa anakuja na hoja za msingi ila kanjibai anachomekea Mambo ya mikopo,hapa anajihidhirisha kua how weaker he is.
Watu wanachoshindwa kuelewa ni kwamba, Kingwa ametumwa na anawakilishwa baadhi wanachama na members wa bodi ambao hawakubalian na mwenendo wa uwekezaji, kutokana na power ya Mo wanaogopa kumkosoa, na Kingwa kashathibitisha hilo kwenye tweet yake ya mwisho.
 
Marefa wa Tanzania kiwango chao kipo chini sana bado. Uwezo mdogo sana. Kwa mfano jana Ihefu imenyimwa goli la wazi kabisa kwa kusema ni offside
 
Marefa wa Tanzania kiwango chao kipo chini sana bado. Uwezo mdogo sana. Kwa mfano jana Ihefu imenyimwa goli la wazi kabisa kwa kusema ni offside
Goli la kagere pia lilikuwa la wazi kabisa kwa kusema offside unasemaje kwa hili.
 
Goli la kagere pia lilikuwa la wazi kabisa kwa kusema offside unasemaje kwa hili.
Refa alishaharibu kwa watoto kile kitu kilikuwa kinamuumiza nafsi ikabidi ajifanye kusawazisha kitu ambacho kwenye mpira kule si kusawazisha kwa sababu laiti goli la yule mtoto lingekubaliwa huenda hata huyo meddie asingeingia, mana huenda atmosphere isingekuwa ile tena ilompa nafasi Mzee Kagere kuingia. Na wewe nijibu kisoka sasa
 
NAJUA WAJUA ILA NATAKA KUKUJUZA ZAIDI NA ZAIDI KUHUSU CLUB YA SIMBA

Na: Hashim Mbaga

UWEKEZAJI NA SIMBA

Simba ilipoanza mfumo wa mabadiliko wa Uwekezaji huko nyuma hapakuwa na sheria, kanuni wala Muongozo waliowataka au kuwaelekeza kufanya nini katika kupata Muwekezaji ndani ya Club hii ni kwa katiba ya Simba yenyewe na hata BMT kwa niaba ya serikali. Ndipo BMT kupitia kwa Bwana Kiganja akatoa maaelekezo kuwa katiba ya simba hairuhusu uwekezaji na kushauri kama simba wanataka kubadilisha mfumo ni lazima kwanza wabadilishe katiba ili kuruhusu uwekezaje Na klabu ya Simba wakafuata maelekezo hayo kwa kuitisha mkutano Mkuu maalum ili kufanya marekebisho ambayo sasa katiba ilikuwa inasomeka kuwa unaruhusu uwekezaji Na baada ya hapo msajili wa Vilabu Alikubali baada ya Mwaka 2016 Simba walifanya mabadiliko kwenye katiba ili kuweza Kutambua Uwekezaji katika Mkutano Mkuu uliofanyika Police Mess Dsm.

Ilipofikia 2017 wakati Simba wamempata Muwekezaji na anataka kuingia wako katika hatua za mwisho Ndipo Serikali ikaona kuna haya ya kuweka Sheria kuhusu namba ya wawekezaji katika uwekezaji.

27/10/2017 Sheria mpya ya baraza la Taifa la Michezo itatangazwa kwenye Gazeti la Serikali kuwa ndio Rasmi(Government Notice No.442), hii ni sheria 18A.

Sheria hii iliweka vitu hivi kuwa lazima vifuatwe
1. Hisa za wanachama 51% wawekezaji 49%
2. Hisa zisimamiwe na vyombo husika katika kuuza
3. Wanachama watoe Azimio la kununua hisa wenyewe

December 2017 Simba walipitisha Kwenda katika mfumo mpya rasmi katika Mkutano ambao Waziri alikuwepo na pamoja na mambo mengine aliongea.

January 2018 Uongozi wa TFF, Simba na BMT walikutana, katika kuwekana sawa kuhusu umiliki wa hisa katika Club na kuwapongeza Simba kwa Mo kukubali kupunguza hisa kurudi 49% kama Sheria inavyosema.

@simbasctanzania

INAENDELEA....... 1/3
 
Inatokea ukurasa uliyopita... 1/3

NAJUA WAJUA ILA NATAKA KUKUJUZA ZAIDI NA ZAIDI KUHUSU CLUB YA SIMBA

Na: Hashim Mbaga

SIMBA SPORTS CLUB LIMITED
Hii ni Kampuni iliyoanzishwa na kusajiliwa Brela kama Private Company na sio Public Company.

Kuna tofauti ya hivi vitu viwili sana:
Katika Sheria ya Nchi inavyosema kuhusu usajili wa makampuni COMPANIES ACT No. 12 of 2002 Ambayo ndio sheria mama ya Makamapuni Ibara ya 27 kipengele cha 1 na 2 ukisoma vyote na vipengele vidogo ambao IPO katika ukurasa wa 38 kuendelea Utaelewa sana ila kwa ufupi wacha nikufafanulie

PRIVATE COMPANY
1. Inapata wawekezaji wake wanaojuana.
2. Idadi ya wamiliki inaanza 1 hadi 50.
3. Ni marufuku kuuza hisa kwa umma Bali ni ndani tu
4. Huwezi kuuza hisa kabla ya kukubaliana wenyewe.

PUBLIC COMPANY
1. Wamiliki wake wanaanzia 3 na hawana kikomo.
2. Muda wowote unanunua hisa na kuuza bila masharti yeyote
3. Mtu yeyote anaweza kununua hisa.
4. Zinasimamiwa katika Soko la hisa

TOFAUTI IPO WAPI
1. Simba haijavunja sheria yeyote katika Uwekezaji mpaka hapa.
2. Sheria na Kanuni zilizopo awali hakuna inaposema mambo ya Uwekezaji watatu Bali ndio inatakiwa kuingiza kwa marekebisho.
3. Ukiangalia Sheria za BMT zinazungumzia kwa Public Company sio Private Company.

SIMBA SPORTS CLUB LIMITED
Ni Kampuni ambayo ni muunganiko wa Kampuni Mbili Moja toka kwa Club ya Simba inayoitwa Simba Holding Ltd (51%) ambayo Wakurugenzi wake ni Wadhamini wa Simba kwa niaba ya Wanachama kwa mujibu wa Katiba ya Simba 2018 na Mo Simba Ltd ambayo ni ya Muwekezaji (49%).
Hizi Kampuni mbili ndio zenye dhamana ya pande zote ndani Simba Sports Club limited na ili iweze kukamilika na kufuata sheria zote za nchi kuna chombo cha Serikali kinaitwa FCC ni Tume ya Ushindani katika Biashara moja ya kazi zake ni kuhulisha kampuni Tanzu katika muunganiko kuwa ni salama kwa pande zote katika kufanya Biashara.

@simbasctanzania

INAENDELEA.....2/3
 
natoka Ukurasa uliopita 2/3

NAJUA WAJUA ILA NATAKA KUKUJUZA ZAIDI NA ZAIDI KUHUSU CLUB YA SIMBA

Na: Hashim Mbaga

Ndani ya FCC kuna vitu ambavyo lazima viangaliwe navyo ni (Assets & Liability) Mali na madeni yaliyopo na kuweza kukamilisha ili mizania iwepo sawa.

Katika Mo Simba ltd sababu kampuni hii ni mpya ya muwekezaji haina Madeni bali ina Assets ambazo ni 20B ila kwa upande wa Simba Holdings Ltd ina Assets(majengo na Wanachama) ambao wanathamani ya 10% ya thmani ya jumla huku 41% ikiwa wazi kwa kuweza kujazia baadae kupata mtaji ila pia ina (Liability) Madeni ambayo haya mengi yanatokana na mfumo mbovu wa utawala huko nyuma ambayo haukuwa wenye mizania halisi ya mapato na matumizi kulikuwa na hisani na ufadhili zaidi hivyo kukosa Audited Financial Reports za miaka sio chini ya mitatu nyuma kabla ya kuanza mchakato ambazo zinaendana na Makisio ya vyombo mbalimbali mfano TRA.

MWISHO
Hakuna mtu anaweza kutoheshimu Sheria za nchi ila ni lazima Sheria ziendane na Wananchi wake ndio maana kukawepo na kanuni na Miongozo.
Tatizo kubwa hapa ni Simba kutangulia Sheria na Kanuni mbele kabla hazijakuwepo hivyo kufanya kazi kuwa kubwa sana katika kufanya kwa usahihi na uhakika katika Win Win Situation.

Lazima kuheshimu Uthubutu wa Mtu na kumpongeza katika suala la Uwekezaji ambao unamatatizo kiasi hiki bila kuwa na moyo wa Kiuwendawazimu huwezi hata kama kuna mapungufu kidogo RESPECT muhimu sana.
HONGERA SANA CHAIRMAN MO

TUNAPOTAKA MABADILIKO LAZIMA TUWE TAYARI NASI KUBADILIKA

@simbasctanzania

ITAENDELEA TOLEO LIJAYO.
 
Refa alishaharibu kwa watoto kile kitu kilikuwa kinamuumiza nafsi ikabidi ajifanye kusawazisha kitu ambacho kwenye mpira kule si kusawazisha kwa sababu laiti goli la yule mtoto lingekubaliwa huenda hata huyo meddie asingeingia, mana huenda atmosphere isingekuwa ile tena ilompa nafasi Mzee Kagere kuingia. Na wewe nijibu kisoka sasa
Mwisho wa msimu Simba bingwa, nyie endeleeni kulia tu
 
Kesho tarehe 12/9/2020.

Mtibwa Sugar v/s Simba Sc

Saa 10:00 Jioni

Point 3 muhimu zinatakiwa MSIMBAZI.
 
Shiboub
Screenshot_2020-09-11-22-59-56.jpg
 
Watu wanachoshindwa kuelewa ni kwamba, Kingwa ametumwa na anawakilishwa baadhi wanachama na members wa bodi ambao hawakubalian na mwenendo wa uwekezaji, kutokana na power ya Mo wanaogopa kumkosoa, na Kingwa kashathibitisha hilo kwenye tweet yake ya mwisho.
Km members wa BODI alafu unaenda kumwambia mtu wa kawaida akusaidie UNA AKILI KWELI?nafas na sehemu nzur ya kusemea hili ni wap?

Sent from my SM-N910F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom