Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Dar Young Africans

Kocha wa zamani Yanga atishia kushtaki Fifa
broken-heart.jpg
Vicky Kimaro

UONGOZI wa Yanga unadaiwa kumpiga chenga na kutomlipa aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo, Spaso Sokolovski mishahara yake ya miezi saba, jambo ambalo limemlazimisha atishie kuishtaki klabu hiyo kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa.

Raia huyo wa Serbia ameiambia Mwananchi kuwa anadai mshahara wake unaofikia dola 6,000.

Alisema fedha hizo ni mshahara wake wa miezi saba tangu kusitishwa kwa mkataba wake pamoja na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, Dusan Kondic mwishoni mwa mwaka jana.

Sokolovski amekuwa akisota kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akitaka shirikisho hilo limsaidie kupata haki yake kutoka kwa uongozi wa Yanga.

Alisema, "Nimechoka kuvumilia, kila siku wamekuwa wananipa ahadi za uongo, ona kama leo, tuliahidiana na Mwalusako Lawrence, ambaye ni katibu mkuu waYanga, tukutane hapa (TFF) wathibitishe kwa maandishi ni lini watanilipa, lakini matokeo yake siwapati kwenye simu,"alilalama Mzungu huyo juzi.

"Nawapa siku mbili kama wataendelea kunizungusha, nitachukua hatua za kuwasiliana na wakili wangu, kisha nitashtaki Fifa, nashukuru TFF ipo upande wangu, nikiwashtaki Fifa klabu itafutwa kama ilivyofanyika kwa klabu moja ya Brazil.

Wao walimfanyia kocha kitendo kama wanachonifanyia Yanga hivi sasa, Fifa iliifuta ile klabu, ikabidi ishuke daraja na ibadili jina, nawaambia Yanga wasipoangalia,sitashindwa kuwashtaki Fifa,"alisisitiza.

Alisema tangu Yanga ivunje mkataba wake amekuwa akiishi maisha ya shida akisaidiwa na rafiki zake pamoja na TFF, kitendo ambacho kinampa simanzi kubwa ukizingatia ana familia inayomtegemea.

Hata hivyo, kocha huyo amedai kuwa tayari ameingia mkataba na timu ya Shanghai China ili ainoe timu hiyo.

Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela akizungumzia suala hilo alisema, "Tupo kwenye mazungumzo na Yanga, na tunataka wathibitishe kwa maandishi watamlipa lini kocha wa watu hizo haki yake ili aondoke kwa amani na usalama, wasiharibu sifa ya nchi,"alisema Mwakalebela. Katibu Mkuu wa Yanga, Mwalusako akizungumzia suala hilo alisema, "Tumeshaongea na TFF na tumewaambia baada ya mechi yetu na Lupopo tutafanya taratibu za kumlipa na tumeshamuarifu fedha zake atazichukulia TFF."
 
Naomba tukutane na Simba mechi ijayo tuvunje hiyo rekodi yao
tupo tayari kuzipiga na nyie anytime...tatizo lakini nyie mnaogopa....mligoma kuingiza timu last time na with our record ya sasa hivi naona mtakimbia for good....hahhahahaah..pelekeni timu congo kwanza....
 
Hawa wanaenda kutimiza ratiba tu.
 
Kocha wa zamani Yanga atishia kushtaki Fifa
broken-heart.jpg
Vicky Kimaro

UONGOZI wa Yanga unadaiwa kumpiga chenga na kutomlipa aliyekuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo, Spaso Sokolovski mishahara yake ya miezi saba, jambo ambalo limemlazimisha atishie kuishtaki klabu hiyo kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa, Fifa.

Raia huyo wa Serbia ameiambia Mwananchi kuwa anadai mshahara wake unaofikia dola 6,000.

Alisema fedha hizo ni mshahara wake wa miezi saba tangu kusitishwa kwa mkataba wake pamoja na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, Dusan Kondic mwishoni mwa mwaka jana.

Sokolovski amekuwa akisota kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akitaka shirikisho hilo limsaidie kupata haki yake kutoka kwa uongozi wa Yanga.

Alisema, "Nimechoka kuvumilia, kila siku wamekuwa wananipa ahadi za uongo, ona kama leo, tuliahidiana na Mwalusako Lawrence, ambaye ni katibu mkuu waYanga, tukutane hapa (TFF) wathibitishe kwa maandishi ni lini watanilipa, lakini matokeo yake siwapati kwenye simu,"alilalama Mzungu huyo juzi.

"Nawapa siku mbili kama wataendelea kunizungusha, nitachukua hatua za kuwasiliana na wakili wangu, kisha nitashtaki Fifa, nashukuru TFF ipo upande wangu, nikiwashtaki Fifa klabu itafutwa kama ilivyofanyika kwa klabu moja ya Brazil.

Wao walimfanyia kocha kitendo kama wanachonifanyia Yanga hivi sasa, Fifa iliifuta ile klabu, ikabidi ishuke daraja na ibadili jina, nawaambia Yanga wasipoangalia,sitashindwa kuwashtaki Fifa,"alisisitiza.

Alisema tangu Yanga ivunje mkataba wake amekuwa akiishi maisha ya shida akisaidiwa na rafiki zake pamoja na TFF, kitendo ambacho kinampa simanzi kubwa ukizingatia ana familia inayomtegemea.

Hata hivyo, kocha huyo amedai kuwa tayari ameingia mkataba na timu ya Shanghai China ili ainoe timu hiyo.

Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela akizungumzia suala hilo alisema, "Tupo kwenye mazungumzo na Yanga, na tunataka wathibitishe kwa maandishi watamlipa lini kocha wa watu hizo haki yake ili aondoke kwa amani na usalama, wasiharibu sifa ya nchi,"alisema Mwakalebela. Katibu Mkuu wa Yanga, Mwalusako akizungumzia suala hilo alisema, "Tumeshaongea na TFF na tumewaambia baada ya mechi yetu na Lupopo tutafanya taratibu za kumlipa na tumeshamuarifu fedha zake atazichukulia TFF."

Weweeee.... Tatizo la ufadhili usio sustainable na uliokosa Tija, burushi kaondoka juzi tu siri zote zitatoka

Yanga Lipeni mtu wenu pesa mjisitiri, zungusheni kombe mtaani
 
Wadau tupeane updates za kandambili huko DRC km desturi yetu. Adui mwombee njaa...........
 
Jamani msimbazi leo vipi? Si nilisikia tunacheza na Zesco au sio leo?
 
Haya wadau safari tayari inakaribia...

Tunacheza na Lengthens Fc kutoka Zimbabwe...tuwaonyeshe Kanda2 namna ya kuzipiga michuano ya Kimataifa...tumewaonyesha namna ya kuwafunga Zesco....here we come...
 
Mwaka huu Yeboyebo ama Kanda2 walie tu, manake Simba keshanguruma, hakuna wa kucheza.
 
Wekundu popote mlipo nawaombeni tubadilishane mawazo na kupeana updates kuhusu chama letu.Kuna mdau katu-update hapo down kuwa unaweza kuchangia chama letu kwa kutuma ujumbe,tuma neno SIMBA kwenda namba 15556 .maelekezo zaidi utayakuta ndani ya thread. hata kandambili mnaotukubali mnaruhusiwa.gonga basi thanks hapo down kama vipi. GUD TYM.

Du!mshikaji unapenda tu thanks!!!!!!!!! mi sikugongei ila nakupa big up.
 
Lupopo sasa wataka kupambana na Simba
broken-heart.jpg

Michael Momburi, Nairobi
KLABU ya FC Lupopo iliyoitoa Yanga katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 4-2, imeomba kucheza tena mechi ya kirafiki na timu hiyo pamoja na Simba.

Yanga iliaga michuano hiyo katika raundi ya awali baada ya kufungwa mabao 3-2 katika mchezo wa kwanza na baadaye kutandikwa bao 1-0, mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Kenya.

Katibu wa timu hiyo, Ilunga Mbala aliiambia Mwananchi jana kuwa wanazitaka Simba na Yanga kwa michezo ya kirafiki kwa kuwa ni klabu kubwa. Timu hiyo inajiandaa na mchezo wake dhidi ya Dynamo mjini Kinshasa.

Alisema kuwa mazingira ya Dar es Salaam wameyakubali na kuwa mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali. Kocha wa Yanga, Kosta Papic amekubali mchezo huo pamoja na mwenyekiti, Imani Madega aliyesema wataanza maandalizi mapema.

Wakati huo huo, Papic amewaomba radhi mashabiki wa soka kutokana na timu hiyo kufanya vibaya katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa raundi ya awali.

"Mimi ndiyo imeniumiza zaidi, ispokuwa nasikitika nimeshindwa kutimiza matakwa ya mashabiki, nawaomba radhi kwa hilo," alisema Madega.

Katika hatua nyingine, wachezaji wa Yanga, Boniface Ambani na George Owino wameomba kubaki Nairobi kuona familia zao na wanatarajia kujiunga na wenzao kesho.

Baadhi ya wachezaji wa Yanga waliwasili hapa jana jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 12:40. wachezaji wengine walifika mapema zaidi kuwahi kambi ya timu ya taifa, Taifa Stars inayocheza na Uganda Cranes kesho mjini Mwanza.
 
Lupopo wanafikiri Mnyama ni sawa na unga wa mahindi ya kitimoto! Saizi yao tutachezesha timu B.
Mkuu yaani hawa wacheza bolingo wanajua kuwa njano is equal to RED ? naona hawajui walitakalo hawa jamaa
 
Back
Top Bottom