Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread
Lile lilikuwa zengwe tu🙂! Simba hii ya Phiri ni moto usiozimika kirahisi!

Haya tuambie hilo zengwe lilikuwa la namna gani.
Tunaomba uweke wazi tafadhali na kama ukishindwa uombe radhi.
 
Wana Msimbazi, ikiwa SImba itasonga mbele kuna uwezekano wa kukutana na timu gani? Naona msimu huu huenda SImba ikafikia hatua ya makundi.
 
Wana Msimbazi, ikiwa SImba itasonga mbele kuna uwezekano wa kukutana na timu gani? Naona msimu huu huenda SImba ikafikia hatua ya makundi.

Sema fainali bana makundi wapi ndugu yangu!!!
 
Siwezi kushabikia Simba hasilani abadani.
na mnavyojisifia kuwafunga hao wandebele yaani utadhani mmewafunga Enyimba Musica...

Vizimbabwe vyenyewe vina njaa kuanzia kichwani mpk unyayoni...wanapata mlo mmoja tu kwa siku, halafu eti mnawafunga kisha mnajigamba....

Acheni ushamba nyieee...
Mngemfunga al-ahly si ndo mngeandika habari za Simba mpk kwenye jukwaa la siasa...

Simba ina mashabiki wengi sana wala haihitaji kushabikiwa na **** kama wewe. Tutaendelea kutamba kila tunapobamiza mtu. Wewe na kandambili wenzako mlie tu...
 
Nime- notice kuwa Wazimbambwe wana jumla ya timu nne zinazoshriki katika haya mashindano Mawili ya Champions na Confederations (Lengthens,CAPS United,Gunners & Dynamos)..Does anyone know why,na criteria inayotumika na CAF timu kuwa na timu zaidi ya moja katika shindano moja? Najua kuhusu Mabingwa kama TP Mazembe na Lupopo wote wanashiriki Champions bcoz TP Mazembe ni mabingwa watetezi,ila sielewi kuhusu huu mfano wa Zimbabwe,mwenye data pliz
 
Wana Msimbazi, ikiwa SImba itasonga mbele kuna uwezekano wa kukutana na timu gani? Naona msimu huu huenda SImba ikafikia hatua ya makundi.
Timu ya Misri (Haras el Hodoud au timu ya Ethiopia (Banks) lkn uwezekano nimkubwa wa kukutana la wa Misri kwani mechi yao ya kwanza walitoka sare ya goli moja kwa moja ugenini tuombe Mungu tuingie Makundi kwani hao wa misri hawa tishi kivile, kama sikosei ndiyo wale waliocheza na timu ya Zanzibar wakaitoa kwa tabu...
 
Nime- notice kuwa Wazimbambwe wana jumla ya timu nne zinazoshriki katika haya mashindano Mawili ya Champions na Confederations (Lengthens,CAPS United,Gunners & Dynamos)..Does anyone know why,na criteria inayotumika na CAF timu kuwa na timu zaidi ya moja katika shindano moja? Najua kuhusu Mabingwa kama TP Mazembe na Lupopo wote wanashiriki Champions bcoz TP Mazembe ni mabingwa watetezi,ila sielewi kuhusu huu mfano wa Zimbabwe,mwenye data pliz

Bila shaka inatokana na kiwango cha nchi. Kama UEFA vile si unatujua watu weusi kwa kuiga. Nchi ambayo kiwango kiko juu inatimu mbili, Misri, Moroko, Algeria, Ghana, Cote d'voire na the list goes on.
 
Bila shaka inatokana na kiwango cha nchi. Kama UEFA vile si unatujua watu weusi kwa kuiga. Nchi ambayo kiwango kiko juu inatimu mbili, Misri, Moroko, Algeria, Ghana, Cote d'voire na the list goes on.

Thanks kaka !
 
Jamani wana msimbazi nasikia Okwi na Owino kaenda zake Uganda mara Yebo yebo wana mmendea je kuna mtu ana-data au ni uzushi tu....
 
Jamani wana msimbazi nasikia Okwi na Owino kaenda zake Uganda mara Yebo yebo wana mmendea je kuna mtu ana-data au ni uzushi tu....

Okwi kaenda uganda na owina yupo dar.witw wanayo mkataba mpaka 2012 kwa hiyo kanda mbili hawana ubavu kuvunja mkataba na nilikuwa na kassim dewji juzi na kama kuuza wachezaji tutawauza ulaya na siyo tanzania.ila okwi hatujui mambo yako aje maana simu yake haipatikani lakini wanajamii hao tutakuwa nao tuu.yanga hawana mbavu kutubomoa
 
Wadau wa soka hasa wapenzi wa Mnyama, mie naomba tuangalie sana umuhimu wa mfumo wa uchezaji wa timu kuliko mchango wa mchezaji mmoja mmoja. Na hapa nataka tuwe wakweli kukubali mchango mkubwa wa benchi la ufundi katika mafanikio yetu. Hata kama wachezaji hao wataondoka,mie nasema tuombe utulivu na amani idumu klabuni na benchi la ufundi likaachwa kufanyakazi zake....Simba itaendelea kufanya vizuri na vizuri !
 
Hii thread mbona inasahulika au kwakuwa tushanyakuwa Ubingwa?
 
Date::4/13/2010 Tumejiandaa kutibua sherehe Simba- Yanga
broken-heart.jpg
Jessca Nangawe

SIKU tatu kabla ya pambano baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga wachezaji wa Yanga wameibuka na kuanza kutamba kuwa watapunguza furaha ya ubingwa ya wapinzani wao.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti,wachezaji hao walisema ili kupunguza furaha ya wanasimba na Msimbazi kwa jumla, wao wana jukumu la kuwafunga katika mchezo huo wa Jumapili usiku.

"Ni lazima tuhakikishe tunashinda mchezo huo unaosubiriwa na mashabiki wengi kwani tutakuwa tumejiwekea heshima licha ya kuwa mwaka huu tumeny'ang'anywa ubingwa," alisema mchezaji mwandalizi wa klabu hiyo.

Huku akiungwa mkono na wenzake kadhaa, alisema wanajipanga vizuri ili kuhakikisha mchezo huo wa Jumapili wanashinda kwa namna yoyote ile na mbali ya wapinzani wao kuwa tayari wamejitangazia ubingwa wamedai wanaamini kushinda kwao kutapunguza furaha kwa Simba kwani ni mchezo wa kuweka heshima.

"Tunajipanga kuhakikisha tunashinda katika mchezo wetu na Simba Jumapili na ili kulinda heshima ni kutimiza lengo letu la kuwafunga Simba licha ya wao tayari wamejitangazia ubingwa mapema, tutahakikisha tunawapunguzia furaha yao,"alisema Boniface Ambani.
Naye beki Nurdin Bakari alisema ili kulinda heshima ya Yanga katika mchezo unaohusisha timu hizo mbili kongwe, watahakikisha wanashindana kwa wao wote na kuahidi kutoa ushirikiano baina yao na kocha wao (Kostadin Papic) ikiwa ni pamoja na kuongeza juhudi baina yao ili waweze kutimiza azma yao ya kushinda katika mchezo huo.

Naye mshambuliaji Mrisho Ngasa ambaye anawania nafasi ya ufungaji bora akiwa na mabao 14 sawa na Mussa Hassan Mgosi wa Simba na John Boko wa Azam alisema ushindi dhidi ya Simba ndio utakuwa nafasi yake ya kuchukua kiatu cha dhahabu kwa kuwapita wapinzani wake hoa wawili.

Alisema atajitahidi na kuhakikisha siku hiyo anafunga goli ili kuzidi kuwakimbia wapinzani wake na kujitengenezea
mazingira mazuri ya kuvaa kiatu hicho msimu huu.

Mchezo huo uliokuwa uchezwe Jumapili iliyopita uliahirishwa kwa sababu ambazo zimekuwa zikidaiwa kuwa za kiusalama zaidi kutokana na klabu hizo kutaka kutumia Uwanja wa Uhuru huku serikali ikitaka ule wa Taifa.

Tayari Simba wametangaza ubingwa baada ya kufikisha pointi 56 ambazo haziwezi kufikishwa na timu yoyote ikiwamo Yanga yenye pointi 48.

Simba, kwa upande wao wamekuwa kambini visiwani kwa maandalizi ya mchezo huo ingawa habari zilizopatikana juzi zilieleza kuwa kocha wao, Patick Phiri amesafiri kwenda kwao, Zambia kwa sababu binafsi akiacha jukumu hilo kwa msaidizi wake,Amri Said.

Simba ambayo haijapoteza mchezo msimu huu imedhamiria kuendeleza rekodi yake.

Kiingilio cha juu cha mchezo huo kitakuwaSh 40,000 na kile cha chini kikiwa Sh5,000.
 
Yebo yebo kesho tuna mpiga mbili zina tosha ameongea sana....
 
wakuu, tic-tac! we are counting on seconds now, ready to rumble!!! all the best Simba and all the best Mgosi ulambe ile buti ya dhahabu

Prediction 3-0 to simba hahahaaaaaaaaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom